Kuna kitu kinaitwa CREATIVITY ukishindwa kuelewa upana wa hili neno basi utateseka sana na unaweza ukawa unakisema vibaya kila kitu.
Tatizo Tanzania huwa tunacomplicate kwenye kila kitu kwa kutaka kulinganisha na akina fulani.
Unatakiwa kwanza kuelewa LENGO la huo wimbo ni lipi? Hizo ni aina ya nyimbo zinazo takiwa sana TIKTOK hasa kuburudisha....lengo lake sio Elimu, kukosoa, nk ila KUBURUDISHA na ndiyo maana ukienda tiktok unakuta inaenda saaaaana....Lengo lake limetimia kwa 100% na unakuta anapiga pesa zake safi.
Watu wako stressed vibaya mno wanahitaji furaha, vitu kama hivyo vinawaletea furaha wengine na kuwapa tabasamu kwa vile vituko vinavyo onekana ndani na ndiyo sababu kwenye Fasihi kuna MELO DRAMA ambayo kazi yake ni kuentertain.
Sijui bongo wakisikia CREATIVITY huwa wanatafsiri kwamba lazima utoe Calm Down kama ya Lema?
Unahisi why imeenda sana? Yes ofcoz POWER OF BRANDING inahusika lakini je kwa walengwa wake ambao aliwakusudia imekuwaje? Lengo limefanikiwa.
Kuna kitu kinaitwa TARGET CUSTOMER kwenye business....ndo hapo huyo dada na bosi wake sijui mumewe wanawazidi watu kwenye upigaji wa pesa.....
Ukiona hauielewi TEKNO usiconclude kwamba ni mbaya jua wewe sio mtu husika wa Tekno na ambaye ndiye target customer atainunua tu au ataipenda [emoji28]
Take easy mkuu....SANAA ni pana sana....so far Zuhura ni artist mzuri sana ila usitegemee kila muda atakuletea Cheche, mara no body.....let's enjoy maisha hayataki uwe serious kupita kiasi.