Zuhura Yunusu wa BBC, ambana maswali Bob wine

Zuhura Yunusu wa BBC, ambana maswali Bob wine

Mwanadada mtanzania,ambaye anafanya kazi n.a. shirika la utangazaji la Uingereza BBC amekuwa mahiri katika kufanya mahojiano ya kuchokonoa , na kufanya duku duku la msikilizaji kuisha endapo anayehojiwa atatoa majibu fasaha,

Mwaka 2015 alimbana Lowassa kwa maswali baada ya Lowassa kujitapa akiwa rais atafuta rushwa na ufisadi, aliulizwa swali moja tu kwamba "Ulipata kuwa waziri mkuu Moja ya ngazi kubwa za uongozi Tanzania na ulikuwa na nafasi kwanini hukuyafanya kipindi hicho na useme utafanya sasa?"

Ngoyai aliishia kusema unanionea

Mwaka huu kaulizwa maswali bwana Tundu Antipass Lissu kwamba unaituhumu serikali kwamba ndo wamekushambulia na serikali hiyo hiyo kupitia wabunge wa CCM walichangia mpaka kukueezesha kufika Nairobi wakati chama chako hakijapata hela inakuwaje hii, Lissu akasema unajua mazingira yanaonesha ni serikali,

akaulizwa mbona alipokutembelea Mama samia Hassan Nairobi hukukataa na ukasema amsalimie rais na unashukuru kwa ujumbe wake hii imekaaje? Lissu mnajua alochojibu


Sasa ni zamu ya Bob Wine anaulizwa hapa sikiliza

anaulizwa unataka kumpindua M7? Bob anajibu hapana sitaki, je una mpango wa kuwa rais? Bob anasema tunachoangalia siyo nani ni rais, tunaangalia waganda kuwa free,
zuhura anauliza utasemaje uganda si free wakati uhuru wa mahakama ndo umeipinga serikali na kusema utibiwe nje?? Sikiliza majibu ya Bob Wine



Unawapenda madikteta?
 
Alijibu kuwa mahakama na serikali wameruhusu kwa sababu ya presha ya wananchi ndani ya Uganda na nje ya Uganda, kitu ambacho ni kweli, sasa sijui huko kubana kukoje!
 
Awali wanaume walikuwa wanamuogopa kwa kuwa anajiamini ila ni mke wangu wa ndoa. nani aliyekuambia hajaolewa?
 
Maswali yanaandaliwa kwa msaada wa mhariri kwenye postmortem ya waandishi huku mwandishi mtarajiwa aliyechaguliwa kwenda kufanya interview akiwepo kuchangia haina ya MASWALI atakayokwenda kumuuliza mgeni wake.

Naona wengi wa wadau humu mnamuona Zuhura Yunus kama ni kichwa kutokana na maswali anayo wahoji wageni wake, kumbukeni BBC siyo Blog kwamba mhariri, mpiga picha, mwandishi, mrusha story ndiye huyo huyo, hana postmortem.
 
Hao ndio waandishi wanaojua wanachokifanya. Sio wakina kitenge wanaobwabwaja tu
 
Waandishi wa Tanzania wana la kujifunza toka kwa bibie Zuhra Yunusi.

Unakuta mwandishi / mtangazaji wa habari anauliza maswali ya kipumbavu mpaka unatamani kuvunja TV!!

Wajifunze.
 
We huna akili kwani wabunge wa ccm kumchangia lisu matibabu ndo kunaiondolea tuhuma selikari, mbona mume akimuumiza mke kwenye ugomvi humpeleka hosipitali atibiwe, kwa hiyo mume hana.Hatia,
Zuhura au alietoa post?
 
anajitahidi ku balance story . radio inasikilizwa na makundi mawili wanaopinga na wanaoafiki . maswali yote lazima uulize
 
Huyu Dada ana maswali magumu sana,alushawahi kunihoji asee nlpata tabu sana...ila uctake kujua alnihoji kama nani...
tushakujua Eddo, ila pole sana maana ulipata tabu sana
 
Back
Top Bottom