Zuio la mahindi kwenda Kenya tusiwatupie lawama Wakenya. Nchi yao inayo haki kulinda raia wake

Zuio la mahindi kwenda Kenya tusiwatupie lawama Wakenya. Nchi yao inayo haki kulinda raia wake

Hawa watu wataendelea na chuki na serikali ya Nchi hii na sababu ni kuibiwa kwa kura, wanaamini ingekuwa serikali yao haya yasingetokea, na serikali mbili zingeweza ongea kutatua shida hii, na si kama walivyofanya
Jitathimini.
 
Mkuu aflatoxins haitokani na hayo madawa mnayotumia kwenye kuhifadhi mahindi yenu,,aflatoxins zinatokea Kama utakuwa umehifadhi mahindi ambayo hayajakauka vizuri,mahindi ambayo hayajakauka vizuri ukiyahifadhi kwenye hayo magunia yako yanaanza kuvunda taratibu ,huko kuvunda ndio hiyo sumu kuvu au aflatoxins inayozungumzwa hapa.

Tatizo la aflatoxins lipo hasa kwenye namna mnavyovuna,mnavyoanika mahindi yenu maana wengi wenu mnaanika chini na namna mnavyoyahifadhi.Hayo madawa unayotumia have nothing to do with aflatoxins
 
Ni wakati mzuri wa kushirikiana na ndugu zetu wa Kenya kufanya uchunguzi Kama kweli mahindi yetu yana sumu. Tusilaumu bila kufanya utafiti.Inawezekana hii Ni kweli na Watz tunaendelea Kula sumu ndio maana cases za kansa Ni nyingi.Tuache Mambo ya siasa tusimamie ukweli
 
Serikali ya Kenya imetumwa na mabeberu ili kutuhujumu.

Au nasema uongo Ndugu zangu?

[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]
 
Swala hapa ni kuwa hizo sumu zimekua zikiwepo kwa mahindi yanayokwenda Kenya kwa muda gani ??

Tanzania nayo ikiretaliate kwa products za vyakula itamaanisha nini ??

Kama hizo sumu zilikuwepo kwa muda mrefu kwanini hawakuchukua hatua mapema ?? Na kwanini iwe sasa??

Kama Tanzania nayo ikichukua hatua kwa food products itaonekana wamefanya hivyo ili kulipa kisasi.

Maswali yatakua haya pia;

Kama sumu hizo zilikuwepo kwa muda mrefu serikali ya kenya ilikuwa zembe namna gani kuruhusu Raia wake walishwe sumu miaka yote hiyo ??

Kama sumu zilikuwepo kwenye bidhaa za vyakula ambazao Tanzania nayo itatangaza kutokuzipokea serikali yetu ilikuwa wapi kuruhusu sumu ziingizwe kwa muda wote huo mpaka kusubiri kulipiza kisasi kwa kenya.

Ina maana serikali zote mbili za Kenya na Tanzania ni zembe??

Kama sio zembe?? Hili jambo ni la kisiasa tu??

Kwanini siasa zifanyike kwenye vyakula??

Naamini kabisa ikifanyika retaliation itakuwa kulingana na maslahi mapana ya Taifa na kwa kuangalia parameters zote.
 
Crown, unadhani ni ipi iliyobora! Kuzuia mahindi yasiuzwe nje bila kuangalia athari ya wazalishaji? na walalaji? Na hii ya sasa Kenya kuzuia mahindi yetu kwa hofu ya afya za walaji?
Tatizo ni uerevu uliozidi akili zetu,hivyo tupambane na hali yetu.
 
Retaliate kwa ajili ya nini? Kwani lazima kuuza mahindi Kenya?
 
Hii dunia ina mambo, hapo wakulima wenzangu wa mahindi imekula kwao, hali isipowekwa sawa mahindi gunia 20,000
 
The reason
 
Retaliate kwa ajili ya nini? Kwani lazima kuuza mahindi Kenya?
Umesahau kwamba hayo mahindi hayauzwi kenya pekee.

Kuna madhara ya jambo hili hata kwa wateja wengine pia.

Madhara ya muda mfupi na ya muda mrefu.
 
Ok kama Kenya wanadanganya juu ya mycotoxins huku taifa lao linanjaa kwa nini tusiuze Zimbabwe?
 
Unao uhakika kwamba kwenye vikao vyao vya kazi hawajawahi kuzungumzia hilo? Wewe ambacho umeshudia ni katazo la Kenya but huna uhakika wa official correspondences kwani ni vikao vya siri.
Yani unataka kusema Tanzania tutaambiwa mahindi yetu yana sumu na lolote lisifanyike?
 
Hakuna aliyelalamikia Kenya kulinda afya za raia wake!
Wakenya siyo mazuzu kama wa Tanzania wanaodanganywa na lile zuzu kuu linalodanganya wenzake kwamba yesu wa Nazareth anawapenda wakatorik wa chato kuliko Nazareth nayo mazuzu wanaoshangilia. Kama hayawani hovyo
 
Mbona Tz ilichoma vifaranga na nyavu za uvuvi za Kenya je haya hayakuwa mambo ya kinyama, je Tz haikuwa na muda wa kuongea na balozi wa Tz/Serikali??
 
Back
Top Bottom