Zuio la Mapadri kutokuoa ndiyo salama ya Kanisa Katoliki

Kyenyabasa

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2023
Posts
247
Reaction score
715
Ndugu zangu nimekuwa nikiwaza kwamba kanisa Katoliki linawezaje kuthibiti migogoro ndani yake? Hata kama ipo ni ngumu kuisikia mtaani kiasi cha kutitishia ustawi wa kanisa hilo, baadae nikapata jibu japo si la moja kwa moja kwamba yafuatayo yanalifanya kanisa kuwa salama;

  1. Elimu iliyotukuka kwa mapadri, haina kona kona.
  2. Mapadri kutokuoa/kutokuwa na familia. Hoja hii ni kubwa zaidi kwa sababu mtu yeyote akishakuwa na familia anakuwa tayari kufanya lolote ili familia ipate mahitaji.
Rejea migogoro ya wachungaji KKKT, Padri si rahisi kutamaika na Mali maana hakuna anayemuwazia kwamba ampe urithi au mahitaji ya msingi hivyo hali hii hupelekea utulivu ndani ya Katoliki.

Aksanteni.
 
Na matatizo mengi yanaingia ktk taasisi kupitia wanawake - hasa wanawake mamluki.
 
Kutokuoa ni kujitoa Sadaka. Padri na hat sister wao hufunga ndoa na kanisa..Lwa hiyo watawajibikia kabisa maishani mwao yote. .

Ukiona mtu kakengeuka au kapotea basi kama mwanadamu kakosea makosa ya kibinadamu hayana uhusiano na kanisa. Mapadri wanakuja na kuondolka ila kanisa litakuwepo daima😀
 
kwanini wasingekuwa wanawawezesha kutokuwa na nguvu za kiume ili waishi kwa uaminifu na kutokuwa na msongo wa mawazo?

Rijali kuzuiwa kufanya jambo hilo maisha yako yote ama utalifanya kwa kificho au utapata msongo wa mawazo

nmejaribu tu kuwaza …mtaniwia radhi mtaokwazika
 
Ukihasiwa maana ya kujitoa haitokuwepo tena.
 
nasikia mapatri wanawala masister, na pia mapatri wengi wao mashoga
 
Tangu kale, wafalme wengi waliharibikiwa kutokana na matakwa ya wake zao.

Hata Yohana mbatizaji alikatwa shingo kutokana na matakwa ya mke wake. Zipo familia hazielewani na majirani au hata ndugu kutokana na migogoro iliyoamzia kwa akina mama.

Uliwahi kuona shati la mwanaume limeandikwa, 'mtanikoma mtaa wa pili' au 'semeni mtachoka, usiku mtalala' ai ' naringia uzuri wangu, mwenye kuumia aumie'; hayo utayakuta kwenye kanga zonazovaliwa na akina mama. Watengenezaji wa kanga wanarespond kwa demand ya soko.

Lakini kikubwa kuliko vyote ni mapokeo. Mitume walipoitwa na Kristo waliambiwa waache yote, ikiwa ni pamoja na familia zao, wamfuate wakafamye kazi yake. Hata walioomba waende wakazike kwanza, aliwaambia wawaache wafu wakazike wafu wao.

Ukiwa na familia unatakiwa kuihudumia familia yako, lakini watumishi wa Mungu wanatakiwa kuwahudumia watu wote kwa usawa.
 
kwanini wasingekuwa wanawawezesha kutokuwa na nguvu za kiume ili waishi kwa uaminifu na kutokuwa na msongo wa mawazo?

Rijali kuzuiwa kufanya jambo hilo maisha yako yote ama utalifanya kwa kificho au utapata msongo wa mawazo

nmejaribu tu kuwaza …mtaniwia radhi mtaokwazika
Mtu kuwa kuhani/padre ni kujitoa sadaka. Sadaka siku zote ni lazima ikuume. Ndiyo maana huwezi kuwa padre kama itadhihirika kuwa wewe una tatizo kwenye viungo vyako vya uzazi, kwa sababu haitajulikana kama umejitoa sadaka kwa sababu ya wito au umetafuta pa kujibanza kutokana na hali yako.

Wafikirie mitume wa Kristo ambao tayari walikuwa na familia zao, lakini wakaziacha na kuamua kufanya kazi ya Mungu. Kama ni msongo wa mawazo, hao si ndiyo wangekuwa na msongi mkubwa zaidi? Fikiria kuwa mitume wote wa Kristo, usupokuwa Yohana, waliuawa. Na kabla ya kuuawa kwao walipewa nafasi ya kutamka tu kuwa hawatahubiri tena kwa jina la kristo, ukitamka hivyo, unakuwa huru, adhabu yako ya kifo imefutwa, lakini hawakufanya hivyo, mpaka mauti yaliwakuta katika imani thabiti.

Padre kutoishi kiapo chake, ni juu yake na Mungu, maana hata sisi wakristo wa kawaida tuna viapo vyetu, ña mara nyingi tumeshindwa kuviishi lakini hatujapoteza tumaini mbele za Mungu wetu.
 
Kutokuoa ni kujitoa Sadaka. Padri na hat sister wao hufunga ndoa na kanisa..Lwa hiyo watawajibikia kabisa maishani mwao yote. .

Ukiona mtu kakengeuka au kapotea basi kama mwanadamu kakosea makosa ya kibinadamu hayana uhusiano na kanisa. Mapadri wanakuja na kuondolka ila kanisa litakuwepo daima😀
Hivi sadaka unajitoa kwa kanisa ama kwa mungu? Mungu kuna mahala amesema mtumishi wake yoyote asioe? Kama hajasema hiyo kutokuoa inatoka wapi?

Jambo la pili, soon mapadrii wataanza kuoa, kesi za kulawiti watoto na kubaka watoto zimekua nyingi sana sasa presha ya Dunia italazimisha kanisa kuruhusu mapadri kuoa ama wakabiliwe na kesi za kulawiti na kubaka watoto kila kukicha.

Jambo la 3, kanisa halitakuwepo milele, sasa hivi Ulaya kiwango cha watu wanaojitambulisha kama wasio na dini kinakaribiana na wanajitambulisha wana dini. Kwa maana kwamba kiwango cha watu kuamini kuna Mungu kinashuka kwa kasi kubwa sana. Tegemea miaka 50 ijayo ukakuta robo tu ya watu wa ulaya na Marekani ndio watakaokua wanaamini kuna mungu.

Hii hapa ni report ya Marekani ilitoka mwezi uliopita ambapo wasio na dini wanaongezeka kwa kasi isiyo na mfano.

Both Protestantism and Catholicism are experiencing losses of population share. Currently, 43% of U.S. adults identify with Protestantism, down from 51% in 2009. And one-in-five adults (20%) are Catholic, down from 23% in 2009

Kadri watu wanavyozidi kuhoji na kuona dini ni utapeli, miaka michache ijayo dini itakua historia.
 
Ukihasiwa maana ya kujitoa haitokuwepo tena.
Nimeelewa

ni hatare sana .mafuta na moto kuyaweka karibu karibu nafananisha na kuwaweka nyumba moja shmba boy na house girl halafu unachimba biti wasisogeleane

Sister na Mapadri wote wana matamanio na wapo karibu karibu kikazi na kimaisha halafu wanapaswa kujizuia

Hongera zao kwa kweli wanastahiki kupewa maua yao

waliojizuia kikweli kweli katika matamanio hawawezi kushindwa kwny kujizuia kwny ufisadi na ubadhirifu
 
Nimeelewa

ni hatare sana .mafuta na moto kuyaweka karibu karibu nafananisha na kuwaweka nyumba moja shmba boy na house girl halafu unachimba biti wasisogeleane

Sister na Mapadri wote wana matamanio na wapo karibu karibu kikazi na kimaisha halafu wanapaswa kujizuia

Hongera zao kwa kweli wanastahiki kupewa maua yao
Hata wewe unaweza kujizuia kuchapa beki tati wako hata kama mtabaki wawili kwa miezi 6.
Unajiwekea nadhiri tu.
 
Hivi sadaka unajitoa kwa kanisa ama kwa mungu? Mungu kuna mahala amesema mtumishi wake yoyote asioe? Kama hajasema hiyo kutokuoa inatoka wapi?

Jambo la pili, soon mapadrii wataanza kuoa, kesi za kulawiti watoto na kubaka watoto zimekua nyingi sana sasa presha ya Dunia italazimisha kanisa kuruhusu mapadri kuoa ama wakabiliwe na kesi za kulawiti na kubaka watoto kila kukicha.

Jambo la 3, kanisa halitakuwepo milele, sasa hivi Ulaya kiwango cha watu wanaojitambulisha kama wasio na dini kinakaribiana na wanajitambulisha wana dini. Kwa maana kwamba kiwango cha watu kuamini kuna Mungu kinashuka kwa kasi kubwa sana. Tegemea miaka 50 ijayo ukakuta robo tu ya watu wa ulaya na Marekani ndio watakaokua wanaamini kuna mungu.

Hii hapa ni report ya Marekani ilitoka mwezi uliopita ambapo wasio na dini wanaongezeka kwa kasi isiyo na mfano.

Both Protestantism and Catholicism are experiencing losses of population share. Currently, 43% of U.S. adults identify with Protestantism, down from 51% in 2009. And one-in-five adults (20%) are Catholic, down from 23% in 2009

Kadri watu wanavyozidi kuhoji na kuona dini ni utapeli, miaka michache ijayo dini itakua historia.
Corinthians 7:7–8; 32–35: "But I would have you to be without solicitude. He that is without a wife is solicitous for the things that belong to the Lord, how he may please God.
 
Mkuu huu ulikua ni ushauri wa Paulo, ilikua ni personal opinion na sio Amri ya mungu. Paulo mwenyewe anasema ni ushauri sio amri ama sheria.

Soma 1 Timotheo 3: 1-16 lakini stari wa 2 na wa 3 unataja specific kwmaba lazima awe na mke mmoja.

Basi imempasa askofu awe mtu asiyelaumika, mume wa mke mmoja, mwenye kiasi na busara, mtu wa utaratibu, mkaribishaji, ajuaye kufundisha; si mtu wa kuzoelea ulevi, si mpiga watu; bali awe mpole; si mtu wa kujadiliana, wala asiwe mwenye kupenda fedha

So masharti ya kutokuoa has no foundation from the bible.
 
Back
Top Bottom