Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
"Yule anayesaini tunamjua, anafahamika, na yule anayesainiwa anafahamika vilevile kuwa ni mtoro. Hao nao vilevile tutawachukulia hatua za kisheria za kikanuni. Kuna wabunge wengine yote hayo hawafanyi, lakini ndani ya bunge hawaonekani. Huo ndio utoro uliokithiri. Kudharau mamlaka ya Ofisi ya Spika na kudharau wananchi waliowaleta humu ndani."
Kuanzia Jumatatu, hatutegemei haya kufanyika tena. Na Ofisi ya Katibu ina uwezo wa kum-trace kila mbunge alipo kwa signal za simu. Ukiwa Songwe, Katibu anajua uko Songwe. Hata ukizima simu yako, simu sasa hivi bado zinatoa signal.
Kuna mbunge anaomba kibali Ofisi ya Spika anakwenda jimboni, lakini anakwenda nje ya nchi, na sijui wanavukaje kwenye viwanja vyetu vya ndege kwenda nje ya nchi bila vibali vya Spika. Hata ukiwa nje ya nchi, Ofisi ya Katibu ina uwezo wa kujua uko nchi gani kwa signal ya simu yako."