Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Huduma za Usimamizi wa Dharura kutoka Jiji la Johannesburg, waumini 16 kati 33 waliokolewa huku watu 8 wakiwa hawajapatikana hadi sasa
Mchungaji aliyekuwa akiendesha Ibada ya Ubatizo huo ni kati ya waliokolewa kutoka eneo hilo pamoja na waumini wengine...
Chama Tawala cha ANC kimerudisha nyuma mkutano wake uliopangwa kufanyika Dcember 16, 2022 badala yake utafanyika Dec 4, 2022 Jumapili, mkutano huo unalenga kujadili mustakabali wa Rais Cyril Ramaphosa ambaye amekuwa akishukiwa kuvunja Katiba ya nchi hiyo.
Uchunguzi uliofanywa na jopo huru la...
Huenda ni uvivu tulionao ndio unasababisha umasikini wetu na tumebaki kutafuta visingizio visivyo na idadi.
Suala nyeti kama wimbo wa taifa, ambao ndio kitambulisho chetu, iweje tuukwapue wimbo wa Afrika Kusini na kuufanya wetu?
Je, kwanini hatukuufanya wimbo wa Tazama ramani utaona nchi...
Familia moja ya Kigogo, Dar es Salaam, inaomboleza kifo cha mtoto wao nchini Afrika Kusini. Ericky Ismael Ngobei, 22, aliuawa kwa kupigwa risasi Alhamisi iliyopita usiku katika eneo la biashara lenye watu wengi baada ya kuzozana na washambuliaji.
Ndugu wa marehemu amesema kuwa shambulio hilo...
Ripoti ya Uchunguzi wa Sumu kuhusu chanzo cha vifo vya vijana 21 waliofariki dunia wakati wakinywa pombe eneo la #Tavern mwezi Juni, 2022 imeonesha kuwa walikosa hewa kutokana na msongamano wa watu.
Mmiliki wa eneo lilipotokea tukio hilo anakabiliwa na mashtaka ya kukiuka sheria za Pombe za...
Rais wa Afrika kusini Cyril Ramaphosa Jumanne amekabiliwa na maswali makali bungeni, wakati wabunge walipotaka majibu jinsi anavyokabiliana na wizi wa mamilioni ya dola kutoka kwenye shamba lake.
Kwa mujibu wa shirika la habari la AP Ramaphosa alipigiwa kelele na wabunge wa upinzani wakimtaka...
Waendesha wamewakamata Watendaji wa zamani kutoka kampuni ya Usafirishaji ya Umma ya Transnet ambayo inachunguzwa juu ya kuhusika na ufisadi wakati Jacob Zuma akiwa Rais.
Mamlaka ya Taifa ya Mashtaka (NPA) imesema Mkurugenzi Mtendaji wa zamani wa Transnet, Brian Molefe na Mkurugenzi wa Fedha...
Wafanyakazi nchini humo wameitisha maandamano nchi nzima kupinga kupanda kwa gharama za maisha na ukosefu wa ajira wakati ambao mfumuko wa bei ukifikia kiwango cha juu tangu mwaka 2009.
Maelfu ya wafanyakazi waliingia mitaani katika majimbo yote tisa kudai ruzuku ya msingi ya mapato, kima cha...
Taarifa iliyotolewa na Waziri wa Polisi nchini humo, Bheki Cele imeonesha kuwa mauaji yaliongezeka kwa 11.5% katika robo ya kwanza ya mwaka wa Fedha 2022/2023 kupitia takwimu za uhalifu.
Cele amesema watu 6,424 wakiwemo Askari 18 waliuawa katika robo ya kwanza ya mwaka 2022 ambayo ni ongezeko...
Nimepokea hivi karibuni voice note kutoka kwa Mtanzania anayeishi Afrika Kusini. Sauti hiyo ya Dudula Master ambaye ni mhamasishaji mkubwa wa Xhenophobia ametoa onyo dhidi ya wageni wote kuondoka Afrika ya Kusini kuanzia tarehe 02 Septemba 2022 hadi Machi 2023.
Nchi zetu hususan Tanzania...
Walinzi waliokuwa kwenye doria katika Hifadhi ya Wanyamapori ya Kruger, wameripoti kugundua mzoga wa nyati, ambaye alionekana kuwekewa sumu, baada ya hapo walikuta Tai 100 na Fisi mmoja waliokufa kwa kuhisiwa kula mzoga huo
Tai wengine 20 waligunduliwa katika eneo la tukio wakiwa katika hali...
Wanaume 14 wamefunguliwa mashtaka ya kuwabaka wanawake wanane baada ya kuwavamia wakati wakirekodi video ya muziki katika mgodi uliotelekezwa Johannesburg Nchini Afrika Kusini
Mtuhumiwa mdogo zaidi katika kundi la wahalifu ana umri wa miaka 16 ambapo amepelekwa kituo cha watoto kuhukumiwa...
Polisi nchini Afrika Kusini wamewatia mbaroni watu 20 wanaoshukiwa kuanzisha machafuko ya Julai 2021 yaliyopinga kukamatwa kwa Rais Mstaafu Jacob Zuma.
Takriban watu 350 waliuawa kwenye machafuko hayo yaliyozuka muda mfupi baada ya aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Jacob Zuma kufungwa jela kwa...
Waziri wa mambo ya nje wa South Afrika kamchana Blinken kuwa South Afrika na Afrika kwa ujumla hawataki siasa za kipumb2vu za Marekani za kulazimisha kuchaguliana maadui au marafiki.
Maneno hayo yamejiri baada ya Biden wa Marekani kumtuma waziri wake wa mambo ya nje Bwana Blinken aende South...
Mkurugenzi wa Sera na Mipango Bwana Haji Janabi (kushoto) akiongea na wajumbe wa Kamati ya Maandalizi kutoka Tanzania na Afrika Kusini katika kikao awali kufikia kwa maandalizi ya Tamasha la Msimu wa Utamaduni wa Afrika Kusini nchini Tanzania ambalo linatarajiwa kufanyika kuanzia mwishoni mwa...
Mamlaka katika jimbo la Gauteng zimeongeza operesheni zao dhidi ya wachimba migodi haramu katika siku za hivi karibuni kufuatia ripoti za ubakaji wa wanawake wanane na genge la watu na kuwaibia wafanyakazi wa kutengeneza video wakiwa na silaha.
Kamishna wa Polisi wa Gauteng Luteni Jenerali...
Genge la Wanaume 82 wanatarajiwa kufikishwa katika mahakama ya Afrika Kusini leo wakihusishwa na makosa mbalimbali yakiwemo kuwabaka kundi la Wanawake waliokuwa wanarekodi video ya Muziki katika moja ya migodi nchini humo siku ya Alhamisi
Shuhuda wa tukio hilo, lilitotokea huko Krugersdorp...
Kawaida Benki Kuu Duniani huwa zinamilikiwa na Serikali za nchi husika zikiratibu sera mbalimbali za kifedha ikiwemo kudhibiti kiwango cha fedha kinachoingia kwenye mzunguko na kuzisimamia benki binafsi zilizopo kwenye nchi husika. Benki kuu huwa zina nafasi ya kipekee kuimarisha uchumi wa nchi...
Kila Julai 18, Siku ya Mandela au Siku ya Kimataifa ya Nelson Mandela inasherehekewa duniani kote kuenzi mafanikio ya Kiongozi huyo
Kwa mwaka 2022, Maadhimisho haya yanaangazia Usalama wa Chakula na Mabadiliko ya TabiaNchi
Mandela alizaliwa Julai 18, 1918 na kufariki dunia Desemba 5, 2013...
Watu wenye silaha wameshambulia na kuua watu 14 mapema leo, ikielezwa 12 walifariki papo hapo na wawili walipoteza maisha baada ya kufikishwa Hospitalini kwa matibabu. Vilevile, watu wengine 10 wamejeruhiwa
Kamishna wa Polisi Gauteng, Elias Mawela amethibitisha kutokea tukio hilo akisema...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.