SIKU moja baada ya kumalizika kwa msimu wa 2021/22, Yusuf Bakhresa, mmoja wa wakurugenzi wa Azam FC alitangaza vita kwenye mbio za ubingwa katika msimu unaofuata, 2022/23.
Majina ya wachezaji wenye hadhi kubwa pamoja na wataalamu kwenye benchi la ufundi wakashushwa Chamazi kwa mbwembwe kubwa...