uchaguzi

Uchaguzi Tanzania
Uchaguzi hasa wa viongozi katika nchi ni utaratibu (mchakato) rasmi unaoendeshwa kwa mujibu wa sheria kuwawezesha wananchi kufanya maamuzi kwa njia ya kuwapigia kura kuwachagua watu ambao wanawataka kuwaongoza kwa kipindi maalum.

Uchaguzi ni utaratibu wa kawaida wa demokrasia wa kuwapata wawakilishi wa kisiasa ambao umekuwa ukitumika tangu karne ya 17. Kuna aina tatu za msingi za uchaguzi zinazotumiwa kuwapata viongozi kulingana na mfumo unaotumiwa na nchi husika.

Aina hizo ni uchaguzi wa Rais, Uchaguzi wa Wabunge na Wawakilishi katika Baraza la Kutunga Sheria na Uchaguzi wa Viongozi wa Serikali za Mitaa.

Vyama vya Siasa kwa upande wao navyo huendesha chaguzi ambazo zinajulikana kwa jina la “Chaguzi wa Msingi” zinazotumika kuwachagua wateuliwa wa vyama katika aina za uchaguzi ambazo zimetajwa hapo juu.

Endapo Tume haitaridhika kabla ya kutangaza matokeo ya uchaguzi kwamba kulikuwa na kutokufuatwa kwa taratibu, matumizi mabaya au ukiukwaji wa taratibu za uchaguzi au pale ambapo kura za wagombea waliopata kura za juu imelingana, Tume itasimamisha au kufuta uchaguzi au sehemu yoyote ya uchaguzi na itatangaza siku nyengine ya kurudiwa kwa uchaguzi huo.
  1. T

    JamiiForums Tanzania Mbinu za CCM zinazowaacha hoi wapinzani kila uchaguzi ukifika

    Ni wazi kwamba kama hukujiandikisha kwenye daftari la mpiga kura, hauna sifa ya kushiriki zoezi hilo. Na hapa ndipo CCM wamekua mabingwa wa kuvuna ushindi kwa njia nyepesi Sana. Tofauti na vyama vingine CCM wanawekeza sana kushawishi watu wao kujiandikisha, ambapo wale mabalozi wa Nyumba kumi...
  2. beth

    JamiiForums Tanzania Tume ya Uchaguzi Zanzibar: Kura ya mapema (Oktoba 27) haitahusisha Askari wote

    Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC), Jaji Mkuu mstaafu Hamid Mahmoud amesema kura ya mapema haitawahusisha wapiganaji wote wa vyombo vya ulinzi ikiwemo majeshi na Polisi, kama inavyodaiwa na watu wanaojaribu kupotosha ukweli na madhumuni ya kura hiyo. Alisema hayo wakati...
  3. Sky Eclat

    JamiiForums Tanzania Kibonzo: michakato wanayopitia wagombea kuelekea uchaguzi mkuu

  4. Mwanamayu

    JamiiForums Tanzania GE2020 Je, Tume ya Uchaguzi ya Tanzania haijandaa karatasi zenye majina ya wagombea za kupigia kura? Au zimeandaliwa za namna nyingi?

    Leo asubuhi nemesikia kwenye redio ya East Africa, kwenye kipindi cha Supa Breakfast mambo ya tume ya uchaguzi ya kustaajabisha. Mkurugenzi wa tume ya uchaguzi akiwa Mara na kusema wagombea wanaotumia lugha ya matusi na uchochezi kwenye kampeni wataondolewa kwenye karatasi ya kupigia kura. Yaani...
  5. T

    JamiiForums Tanzania GE2020 Marekani yawasihi NEC na Magufuli kujali misingi ya demokrasia kwenye Uchaguzi Mkuu 2020

    Kamati ya bunge la Marekani la seneti ya mambo ya nje imeisihi tume ya uchaguzi Tanzania kujirekebisha, kuondoa makosa yaliyofanyika ndani ya miaka 5 iliyopita, kuacha kumshitaki Lissu kwa hoja ya kijinga. Kamati hiyo inamtuhumu Magufuli kuminya Demokrasia, utawala bora, uhuru wa kujieleza toka...
  6. M

    JamiiForums Tanzania TFF mtuache tumalize uchaguzi mkuu wa rais

    TFF msije kusema hamukuambiwa, Mechi ya Simba na Yanga kuchezwa tarehe 18/10/2020 siku 9 kabla ya siku ya Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani unaofanyika tarehe 28/10/2020 hapa kuna jambo litazua jambo! Machungu yanayotokana na hizo Mechi za watani yana athari zinazodumu kwenye jamii kwa...
  7. D

    JamiiForums Tanzania GE2020 VIDEO: Wachambuzi wa siasa Kenya washangazwa na muundo wa uchaguzi wa Tanzania, wasema walitoka huko kitambo sana

    Hawa ni wachambuzi wa kisasa nchini Kenya wakishangazwa na namna Tanzania ilipo bado kwenye ukoloni japo ni wa watu weusi.
  8. M

    JamiiForums Tanzania GE2020 Kamati ya Maadili yatolea ufafanuzi adhabu dhidi ya Lissu kumfungia kampeni. Yasema ameadhibiwa na Kamati ya Vyama 15 vinavyoshiriki Uchaguzi Mkuu

    KAMATI YA MAADILI: Baadhi ya watu kutaka kuwaaminisha umma wa Watanzania kwamba mgombea huyo ameadhibiwa na tume ya Taifa ya uchaguzi, ukweli ni kwamba bwana Lissu ameadhibiwa na kamati ambayo inajumuisha wawakilishi wa vyama vya siasa vinavyoshiriki uchaguzi wa kiti cha Rais. Wajumbe 15...
  9. T

    JamiiForums Tanzania GE2020 Ili kuondoa utata kuwe na mawakala wa vyama vyote vinavyoshiriki uchaguzi katika vituo vyote na wapewe 'nakala' za matokeo

    Pamoja na kwamba Magufuli amepiga kampeni kwa miaka mitano na miezi hii miwili ya NEC lakini ukifuatilia vizuri kampeni zake, utagundua kuwa ana hofu zaidi ya kushindwa kupata kura za kumuwezesha kushinda uchaguzi ikiwa na maana kwamba asilimia kubwa anaamini anaweza kushindwa. Hii...
  10. J

    JamiiForums Tanzania GE2020 Dkt. Magufuli: Uchaguzi huu ndio utaamua kama tuendelee au tusiendelee na Muungano

    Mgombea urais wa JMT, Dkt. Magufuli amesema watanzania wawe makini wanapopiga kura kwani uchaguzi huu ndio utaamua kuendelea kuwepo kwa Muungano au kuvunjika. Chanzo: Wasafi tv Maendeleo hayana vyama!
  11. Sky Eclat

    JamiiForums Tanzania CCM kitakuwa chama bora cha upinzani na Uchaguzi wa 2025 utakua mgumu

    CCM ikikosa dhamana ya kuongoza nchi, kama haitasambaratika kitakua chama bora cha upinzani kupata kutokea Tanzania. Kuna makosa machache yakifanyiwa kazi na CCM kuingia kwenye tanuri kitatoka kama dhahabu safi inayo ng’ara. CCM Ina uzoefu wa kuiongoza nchi, hivyo itakua mkosoaji mkubwa wa...
  12. Mystery

    JamiiForums Tanzania Ni kwanini CCM idai kuwa Tundu Lissu anatoa lugha ya uchochezi pale anapoihimiza Tume ya Uchaguzi iendeshe Uchaguzi ulio huru na wa haki?

    Nimemsikiliza mara nyingi sana tena kwa makini sana mgombea wa Urais kwa tiketi ya Chadema, Tundu Lissu, mara zote amekuwa akiisisitiza Tume ya uchaguzi nchini, iendeshe uchaguzi mkuu ujao, katika njia ya uwazi, Uhuru na Haki. Amezidi kusisitiza kuwa wanachowataka Tume hiyo ya uchaguzi ni...
  13. kavulata

    JamiiForums Tanzania GE2020 Uchaguzi huo unakaribia, ambae hajasema aseme asikike

    Kila anaeiita Tanzania kwetu kuna vile anapenda iwe na atendendewe. Muda wako ni huu wa kusema kupendekeza, kushauri, kushawishi, kuonya, kutahadharisha, kulaani, na kulaumu na kuunga mkono yale unayoyapenda/usiyoyapenda, maana hakuna mwenye haki miliki ya Tanzania ni dhamana tu tunawapa wafanye...
  14. S

    JamiiForums Tanzania Zanzibar kurudisha kiti chake cha UN baada ya Uchaguzi Mkuu - ACT Wazalendo

    Baada ya ushindi wa dhoruba unaoonekana bila ya chenga kuiangusha CCM, Maalim Seif Sharif amezidi kutoa matumaini ya uhakika kuwa kiti cha Umoja wa Mataifa cha Zanzibar kitahakikishwa kinarudishwa kama ilivyo katika mpira, maendeleo yameonekana ndani ya Afrika Masharikii, Zanzibar inatoa timu...
  15. Analogia Malenga

    JamiiForums Tanzania GE2020 Jaji Mutungi avitaka Vyama vya Siasa kuheshimu Sheria na Taratibu za Uchaguzi

    Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi amewataka viongozi wa vyama vya siasa na wadau wote kuheshimu Sheria na Taratibu za Uchaguzi kama zilivyoainishwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), ili kuepuka migogoro isiyo ya lazima. Akizungumza Jijini Dar es Salaam, katika kikao kati ya...
  16. jitombashisho

    JamiiForums Tanzania GE2020 Ili kufuta kidomo domo cha kina Lissu, nashauri Tume ya Uchaguzi ihesabu kura zote kwa njia ya uwazi

    Hata ikiwa kama nilivyoshauri bado Magufuli atashinda tena asubuhi mapema. Tume ya uchaguzi amueni moja ili kuwakosesha hoja hao mamluki nalo ni kuhesabu kura hasa ngazi ya u Rais kwa uwazi. Ukweli ni kwamba Tundu hana uwezo wa kushinda uchaguzi mkuu na kuendelea kujiamini kwake kuhusu hilo ni...
  17. DR HAYA LAND

    JamiiForums Tanzania Naomba uchaguzi huu tuitunze Amani kwa kutoa haki kwa vyama vyote bila upendeleo.

    I urging (NEC) to deal with provision of Justice fairness, and respectful of decisions making. Most of NEC workers appointed by current president As well the current president is presidential candidate. Tz for now Tz for future tuitunze Amani yetu.
  18. William Mshumbusi

    JamiiForums Tanzania Chadema Rasimisheni tuhuma zenu na hofu zenu juu ya UCHAGUZI nec.

    Napenda hizi ishu zisitupeleke kubaya au kugombana. Mnahofu nyingi juu ya kuibiwa Kura kwa namna tofauti kupitia uzoefu wa chaguzi ndogo za marudio. Ipo haja ya kurasimisha hofu hizo kwa kupitia taarifa za itelejensia mlizonazo. 1. Msibitishiwe mawakala kutotolewa kwa nguvu vituoni na...
  19. Mwanahabari Huru

    JamiiForums Tanzania Hukumu dhidi ya Tundu Lissu yadhihirisha Tume ya Taifa ya Uchaguzi ni Wakala wa CCM

    Niliahidi wiki iliyopita kwamba nitaandika tena baada ya hukumu dhidi ya Tundu Lissu ambayo tayari ilikwishavuja hata kabla ya mashtaka kuandikwa. Hatimaye Tume ya Taifa ya Uchaguzi imetangaza rasmi kumfungia mgombea Urais wa Chadema Tundu Lissu kutojihusisha na kampeni kwa siku 7. Wiki...
  20. S

    JamiiForums Tanzania NANI wa KUIDHIBITI TUME YA UCHAGUZI ?

    Jawabu ni CCM. Je ni CCM pekee ? Tulikubali hilo na tukilikubali nini matokeo yake ? Tegemeo kuu ni mwitikio wa wananchi katika majimbo yao majimbo ambayo kwa sasa inakaribia Tanzania nzima wananchi yameshaikataa CCM,uhakika ni kuzuka kufukuzwa wagombea wa CCM mchana kweupe,tumeona baada ya...
Back
Top Bottom