09 Dec, 2019: Maadhimisho ya miaka 58 ya uhuru wa Tanganyika. Wafungwa 5,533 wapata msamaha wa Rais. Mbowe ataka maridhiano ya Kitaifa

Nilimuona lowasa amezeeka sana hawezi simama vizuri,akili za uzee ni kama unarudi utotoni.
Kwa sasa yupo vizuri. Si kama alivyokuwa chadema. Mara mahakamani, mara vikao vya nini sijui, bado wampige mizinga.
 
Siasa bhana.....! Nikikumbuka matusi, kejeli na dhihaka za wanaCcm kwa Edward kipindi kile nachoka kabisa! Wengine walimtabilia mpaka kifo! Kweli maendeleo hayana chama!
Na wale waliosema kwa miaka nane kuwa lowasa mwizi, fisadi, hana adabu, achomwe moto, azomewe, mvi zake zingekuwa na busara angemwambia mkwewe aache ushoga sababu alitoboa sikio, hafai kupewa hata ukatibu kata. Kisha wakampa tiketi ya urais na kumuombea kura unawazungumziaje?
 
Imagine 2019.
Halafu waku makofi kwah kwah kwah
 
Miaka kumi tu mbona kidogo aendelee tu nchi ilipofika ni pazuri atatuvusha kutupeleka na kutufiksha kama pale alipoiacha Baba Wataifa tutakuwa ametufikisha pazuri na nidhamu itarudi mafisadi chaliiiii
😄😄😄😄
 
Duuh labda Mulungu tu,kwa lugha ya Malawi ni Mungu, kwa Wandali wa Ileje hiyo ni surname ya watu (ukoo)...... kama ni matusi ubarikiwe sana
Nimekutakia mwisho mwema wa mwaka na Mungu akulinde ukipende kisukuma Mjomba, nahmala ni mjomba kwa kisukuma au unataka niwe bagheshi wako?
Bagheshi ni shemeji
 
Mbavu zangu jamani. Kilangila.
 
kila mwaka nasikia kauli mbiu yetu ni ileile ya miaka ya 1960... 70. ya "tutalinda muungano wetu"

Naamini kwa sasa tuko matured enough kuanza kuongelea "kulinda maslahi yetu kama Taifa".
 
Hazikuwa sherehe za uhuru bali zilikuwa mbinu za kumhakikishia jpm muhula wa pili!ndo mana kikwete hakuwepo MEMBE NDO IVO TENA BYE BYE!!!
 
Kilimanjaro karanga hawapo kwenye list! Kati ya magereza makubwa Tz hakuna!! Maana yake nini? Nijuzeni!
Kanda ya ziwa kote wamo!!??
 
stakehigh,
JESHI LA TANZANIA LILITAKIWA LIONYESHE MAMBO YALIYO KWENYE UWEZO WAO, HAWAJAWAHI KUMUOKOA MTU ALIYETEKWA NA GAIDI WANAWEZAJE KUSEMA NI RAHISI? UNAWEZAJE KUJUA KITU NI RAHISI KWA MAZOEZI TU? HUU NDIO UONGO USIOFAA. INGAWA HAKUNA UONGO UNAOFAA.
 
Jumla ya *Wafungwa 293* kutoka magereza Ya *Ukonga, Keko,Segerea na Wazo Hill* jijini Dar es salaam leo wameachiwa huru kwa *Msamaha wa Rais wa Tanzania Dkt. John Magufuli* alietoa Msamaha kwa *Wafungwa 5,533* waliokuwa wakitumikia kifungo kwenye magereza mbalimbali Nchi nzima.

Wafungwa hao wameachiliwa huru leo Mbele ya *Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es salaam Bw. Abubakar Kunenge, Kamanda Wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam Lazaro Mambosasa na Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dar es salaam* ambapo Kwa pamoja wamewataka walioachiliwa huru kwa msamaha wa Rais kuhakikisha *hawarudii kufanya makosa.*

Kwa mujibu wa Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dar es salaam *Kamishina Msaidizi wa Magereza Julius Mtambala* amesema kati ya Wafungwa hao 293 walioachiliwa huru *130 wanatoka Gereza la Ukonga,54 Gereza la Keko, 74 Gereza la Segerea na 35 wanatoka Gereza la Wazo hill.*
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…