1 Timotheo 2:12 una maana gani? Je kwa leo hii bado mstari huu una mashiko?

😂😂😂😂Kwamba ni ayya za vita ? Kwahiyo sasa hazina kazi?
Zitatumika yakitokea mazingira yale yale yaliyosababisha kushuka hizo aya. Na uwezekano wa kutokea hayo mazingira ni mkubwa sana.
 
Zitatumika yakitokea mazingira yale yale yaliyosababisha kushuka hizo aya. Na uwezekano wa kutokea hayo mazingira ni mkubwa sana.
Acha porojo kijana ,Aya zote za Qur’an – iwe za amani au vita – ni muongozo wa milele. Kusema “hazifai tena” ni kujivika mamlaka ambayo hata Mtume hakuwa nayo

Wanazuoni wakubwa wamekubaliana kuwa Qur’an ni ya kila zama,Imamu Al-Shafi’i, Al-Ghazali, Ibn Kathir n.k. wamesisitiza kuwa Qur’an ni sheria kwa kila zama. Hakuna Aya yenye muda wa matumizi kama chakula cha muda.
 
Sasa nani kasema hazitumiki tena?

Nimesema kila aya itatumika katika mazingira yale yale yaliyosababisha kushuka aya hizo.

Kama zilishuka kwa muktadha wa vita basi kukitokea vita tutazitumia tena hata leo hii au kesho na Kuendelea.

Kama aya ilishuka katika jambo fulani tutazitumia kuhukumu jambo hilo mfano wa hilo leo likitokea tena hadi Qiyama.

Lakini ni makosa na ni upotoshaji kuzitumia aya zilizotelemshwa kwa muktadha mmoja kuzipeleka katika muktadha mwengine usio fanana na huo.

Mfano aya zilizotelemshwa kuwapa maelekezo waislamu wakiwa vitani kwamba wawaue makafili kwa sababu nao wamekusudia kuwaua wao,, kuzitumia Aya hizo katika mazingira ya amani na utulivu ni makosa.
 
Acha UPOTOSHAJI ,Leo anayeuacha uislamu kwa mujibu wa Quran na Hadith zenu ,adhabu yake ni ipi ?

Mfano mm niliukana uislamu,je dini yenu inasemaje
 
Pigia tiki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…