tuusan
JF-Expert Member
- Jun 30, 2016
- 17,972
- 20,221
Jk alikua anakusanya tsh 850B kwa mwez uyu jamaa anakusanya tsh 1.5T huwez kusema hakuna alichofanya!!Huyo Mkwere alikua ameona mbali sana na angeivusha Tanzania, leo hii kando na mikwara sioni nini mumeongeza juu ya alichokiacha, SGR mlisema itafanya kazi mwaka jana, mpaka mnaingia kwenye uchaguzi ni ngonjera tu.
Madubwasha yote ambayo huwa mnaringishia humu ni ya Mkwere, nitajie kitu gani kimoja awamu ya tano mumesimamisha kikaonekana na chenye hadhi ya kujadiliwa humu, usisahau hili ni jukwaa la kmataifa hivyo usinitajie chochote uchwara.
Binafsi nahisi mumefaulu kulea chuki tu baina yenu na majirani, yaani kwa kipindi kifupi tumefungiana mipaka mara kadhaa sasa.
Kufufua reli ya Dar -Arusha na Tanga - korogwe ambayo ilikufa kwa miaka 20,ujenzi wa hospitali za wilaya 71,hospitali za rufaa 10 na hosp za kanda 3,kujenga vituo vya afya 400+ na zahanati 1000+...
Jamaa ameamua kujanga bwawa kubwa la kufua umeme 2115MW ni umeme mwingi kuliko tulionao sasa mpaka hapo sijui utasema nn