1500 years Old Bible found in Turkey

1500 years Old Bible found in Turkey

Yesu hakuteswa, alioa na kuzaa, mke wake alifahamika kama Maria Magdalena, hakuwahi kusema popote kuwa ni Mwana wa Mungu, alikuwa mweusi tii...

..kama ambavyo Mungai(r.I.p) alitaka kuifanya elimu ndivyo walivyogeuza na kupindisha biblia ila wenye kufuatilia tunazo biblia orijino, zenye injili ya Maria Magdalena, injili ya Yuda Eskalioti(yule waliyetudanganya kuwa alimuuza Yesu kwa euro sijui vipande vya mini)
Acha bange zako ww toa ushahid sio unaropoka tu

Mbona na nyie huyo Muhammad wenu wanasema alikuwa ni kicheche tu na hata hata hayo maandiko alitumiwa na wachawi kuandika .naye alikuwa mjanja mjanja tu . na kwa kujua hilo NDIYO maana alihimiza msome Qur'an ili msiwe wadadis


Ukipenda kukashifu din ya mwenzio na ww ukikashifiwa usimaind sawa
 
Nasikia Mungu wa kiislamu anajua lugha moja tu ya kiarabu tu. Aliwezaje kuumba watu wanaoongea lugha nyingi?
 
Biblia haikuandikwa immediately baada ya kuondoka kwa Yesu. Iliandikwa baada ya zaidi ya Karne 4 kupita. Hiyo Copy iliyopostiwa ni genuine copy inayosema sawa na mafundisho ya Quran tukufu.

Kwanini ndugu zetu wakristo munaukana ukweli. Hiyo Bible imepimwa na wataalam na imeonekana ni authentic. Lazima mujiulize hivi ni kwanini muna Bible aina nyingi? Hivi maneno ya Mungu yanabadilika yenyewe kutokana na wakati au kuna mtu anayewabadilishia na wakuwataka muamini wanachokiandika??
Siyo bible hiyo bible ni tofauti ni mafundisho yao hayo. Hakuna bible tofauti tofauti. Uzuri ukristo siyo ubishani wa kubishania imani na Mungu wa kweli hatetewi kwa majibizano, na wala hatetewi na mwanadam
 
ETi. Nini? Jiulize haya maswali.

1. Kwa nini baada ya Adam na Hawa kufanya dhambi pale Eden Mungu aliwaficha utupu wao kwa kuwavisha ngozi za wanyama? Damu ilimwagika.

2. Kaini akatoa mazao ya shambani mdogo wake Abel akatoa wanyama. Damu ilimwagika na sadaka yake ikakubaliwa na Mungu.

3. Baada ya gharika Nuhu alichinja kutoa sadaka ya kumshukuru Mungu kwa Yeye na Watoto kuponywa na gharika.

4. Abrahamu akaamriwa amtoe mwanawe pekee Ishaka (pekee kwa maana ya agano lake na Mungu, sio wa makubaliona na mkewe). Mungu akampa Abrahamu kondoo akachinjwa badala ya Ishaka, damu ilimwagika.

5. Musa kuwa komboa wana wa Israel Misri kila nyumba ya myahudi alichinja na damu ya huyo mnyama ikapakwa katika vizingi vya milango ya kuingila ya nyumba za Wayahudi. Malaika wa kifo alipopita akiona damu haingii. Kwa wamisiri kila mzaliwa wa kwanza binadamu na wanyama pia wakauwawa.

6. Ndipo akaja Yesu kuhitimisha hili la msamaha kwa njia ya damu yake yenye thamani kuu kumwagika pale msalabani. Fuatilia utaona kwa siku kumi kabla ya Yesu kusulubiwa wayahudi walihangaika na Yesu na hawa kupata muda wa kumuanda myama wa kuchinjwa kama sadaka ya pasaka pale katika hekalu la kuhani mkuu. Baada ya Yesu kusulubiwa msalabani na damu yake ya thamani kuu kumwagika, umeshasikia mkristo yeyote anaye samehewa dhambi kwa kuchinja? Nani wanaendelea na kuchinja?

Na washawasha!
Inaonekana hukuelewa lugha niyokuandikia. Yalaiti ungeelewa usingesema hao uliyoyasema. Bilblia inakujibu vizuri tu lakini hutaki kuelewa. Biblia na vitabu vyote vya dini vimesema kuwa kila mtu atabeba dhambi zake. Iweje Yesu asulubiwe kwa dhambie zako?? Hayo maelezo na mantiki yake yore nimeyaeleza viziri. Labda nikutafsirie kiswahili.

Na kweli wajumbe wote wa mwenyezi Mungu walichinja wanyama kutoa Sacrifice kama waislamu tunavyochinja. Iweje Mungu aruhusu Yesu ateseke na kumwaga damu yake wakati Yesu alimuomba Mungu amuokoe na mateso hayo?? Inamaana duwa za Yesu zilikuwa hazikubaliki?? hayo yote nimekuelezea kwa mantiki nzuri. Mtafute mtu wa karibu akutafsirie.
 
narudia tena dini gani inayomtambua mtu mweusi??
 
Nasikia Mungu wa kiislamu anajua lugha moja tu ya kiarabu tu. Aliwezaje kuumba watu wanaoongea lugha nyingi?
Kitabu alicholeta Jesus kinaitwa INJILI, sio Bible. Injili ipo katika Lugha moja tu, ni kiyahudi. Hakuna Lugha Nyingine zaidi ya kiyahudi, isipokuwa imetafsiriwa kwa Lugha zingine tofauti kama Kiingireza, Kijerumani, Kiswahili etc. Kwahiyo usitake kutumia Lugha ya kumkashifu Mungu wa waislamu ambaye ndio Mungu wa babu yetu Adam na Yesu na Mungu wetu sote. Kwani Mungu anaweza kukuwajibisha kwa kauli zako na akakupa adhabu kubwa hapo hapo ulipo. Kuwa makini unavyo mu address Mola wa ulimwengu.
 
Yaan nyie waabudu kaaba ambayo haijulikan hata kwa abraham mnaniacha hoi
Hakuna Muislamu anayeabudu Ka'ba. Ka'ba ni Sacred house of GOD kama ilivyo Al-Aqsa Mosque huko Jerusalem ambao ni Sacred kwa Waislamu na kwa Mayahudi pia. Ka'ba ni central point ya waislamu hukusanyika kwa ajili ya kumtukuza Mola wetu sote. Ni vyema kuuliza ikiwa hujui jambo kushinda kutumia lugha za kejeli out of your ignorancy.
 
Je sisi tunao abudu sanamu/msalaba VP inafaa mkuu
Kwanini uabudu Sanam au Msalaba wakati Mungu yupo? Mtafute Mungu wako wa kweli hadi umpate. Soma vitabu vya dini na uulize maswali kwa wasomi. Dini ni very straight forward, haina longo longo. Ukiona longo longo nyingi ujue kuna uongo. Hakutakiwi contradiction ndani ya kitabu cha Mungu. Kisha ujionee ukweli mwenyewe.
 
narudia tena dini gani inayomtambua mtu mweusi??
Ni Uislamu tu. Hakuna dini nyingine zaidi ya ISLAM inayomtambua mtu mweusi na iliyompandisha daraja mtu mweusi. Soma History ya Bilal ndani ya Islam kisha utaelewa.
 
Ni Uislamu tu. Hakuna dini nyingine zaidi ya ISLAM inayomtambua mtu mweusi na iliyompandisha daraja mtu mweusi. Soma History ya Bilal ndani ya Islam kisha utaelewa.
wewe nambie huyo mtu mweusi katambulikaje usinipejazi ya kufunua funua huko maandishi yenyewe sijawahi kuyaekewa!!Jah rastafarai
 
Acha bange zako ww toa ushahid sio unaropoka tu

Mbona na nyie huyo Muhammad wenu wanasema alikuwa ni kicheche tu na hata hata hayo maandiko alitumiwa na wachawi kuandika .naye alikuwa mjanja mjanja tu . na kwa kujua hilo NDIYO maana alihimiza msome Qur'an ili msiwe wadadis


Ukipenda kukashifu din ya mwenzio na ww ukikashifiwa usimaind sawa
Hivyo kuoa na kuwa na watoto ni kashfa?? Wajumbe wote wa mwenyezi Mungu wameoa na wamekuwa na watoto. Kama kuoa na kuwa na watoto ni kitu kibaya basi wasingeoa na pia na sisi tusingezaliwa na ulimwengu pia usingekuwepo. Haifai kukashif dini yoyote ile. Lakini kuoa sio kashfa.
 
wewe nambie huyo mtu mweusi katambulikaje usinipejazi ya kufunua funua huko maandishi yenyewe sijawahi kuyaekewa!!Jah rastafarai
Uliza swali lieleweke. Katambulikaje kivipi? Kisha uliza kama unataka kweli kuelimika na uwe na nia hiyo. Na uwe tayari kusoma. Usiwe spoon feeded information. Ni vizuri ukisoma mwenyewe.
 
Uliza swali lieleweke. Katambulikaje kivipi? Kisha uliza kama unataka kweli kuelimika na uwe na nia hiyo. Na uwe tayari kusoma. Usiwe spoon feeded information. Ni vizuri ukisoma mwenyewe.
kitabu gani mtu mweusi katajwa kama nabii au mteule wa mungu
 
Watu watajiunga na dini yako kwa kuona mafanikio yatokanayo na neema as Mungu wako katika maisha yako. Sii kwa kejeli wala kubeza imani za wengine.
 
kitabu gani mtu mweusi katajwa kama nabii au mteule wa mungu
Anaitwa Bilal(Radhi za Mola Zimfikie). Awali Alikuwa mtumwa. Wakati alipokuwa akiteswa kwa kumuamini Mtume, basi Mtume aliposikia kuwa anateswa akamnunua kutoka kwa wamiliki wake kwa thamani kubwa ambao waislamu waliokuwa wachache wakati huo walitoa. Na baada ya hapo Bilal kuachiwa huru na hatimaye Bilall akawa ni kati ya wafuasi wakubwa wa Mtume na ametukuzwa kwa sifa nyingi. Bilal ni mtu wa kwanza kuadhini. Adhana unazozisikia misikitini waislamu wanapoitana kuswali ilianzia kwa Bilal.
 
Watu watajiunga na dini yako kwa kuona mafanikio yatokanayo na neema as Mungu wako katika maisha yako. Sii kwa kejeli wala kubeza imani za wengine.
Uislamu inakataza kubeza na kukejeli dini yoyote. Hakuna ukejeli nilioufanya bali nimezungumza ukweli tu. Sema wako watu wanaonikejeli mimi.
 
he was crusifised, he died and after 3 days risen among ded,
ALISULUBIWA
AKAFA
AKAZIKWA
SIKU YA 3 AKAFUFUKA kati ya WAFU..

HII NI AMINA NA KWELI.


Na hii ndio imani inayokufanya uitwe mkristu
 
Maana nib1500 years old ambayo ina maana miaka ya karne ya 5 yaani 500 AD.
Sasa jiulize yesu aliishi 500 years before that .na ilikiwa written katika biblia kuwa alisulubiwa sasa inakuaje mtu aje abadilishe.
Mfano mzur nyerere amefariki london na kuzikwa butiama baada ya miaka mia tano 500 wanaibuka watu wanasema alikufa butiama na kuzikwa london
Unaakili sana mkuu, chukua like ya nguvu[emoji106]
 
Na hii ndio imani inayokufanya uitwe mkristu
Ni kweli. Lakini according to Bible yote hayo hayakutokea. Ushahidi upo kamili kwenye thread. Hivi vitu ni vizuri kuwa addressed kwani ni wajib kutafuta ukweli. Na imani lazima iwe na foundation ya ukweli isiyokuwa ya shaka.
 
Back
Top Bottom