1963: Rais wa Jamhuri ya Tanganyika, Julius Nyerere akiweka pini katika koti la Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Bw. U Thant

1963: Rais wa Jamhuri ya Tanganyika, Julius Nyerere akiweka pini katika koti la Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Bw. U Thant

..pia uamuzi wa serikali kutaifisha mashamba ya mkonge kusababisha sekta hiyo kuporomoka.
Ni uamuzi wa hovyo sana. Kwa waliokulia maeneo kama Tanga ustawi wa jamii nyingi ulitegemea sana zao la Mkonge. Katika kipindi hiki dunia ikipambana na climate change, Tanzania ilikuwa na fursa ya kutumia mkonge kuziba pengo la plastic katika maeneo mengi sana, tulifeli.
Hakukuwepo na sababu zozote zile za maana za kutaifisha mashammba yale na sasa ni mapori
..Na mpaka hivi tunavyozungumza uzalishaji wa mazao hayo haujakaa sawa kutokana na athari za maamuzi yetu huko nyuma.
The country will never recover from that epic loss

Ni moja kati ya makosa makubwa sana ya Nyerere
 
Nyerere kuna mambo mengi hata wafuasi wake hawajawahi kutoa majibu
Wafuasi wake kama wapo watakuja kujibu
Why alingo'a reli ya kusini?
Hapa ningependa kuelewa, Reli iling'olewa lini na kwa utaratibu gani?
Why aliunga mkono rebels wa Nigeria?
JokaKuu kafafanua, hata hivyo tukihoji tusiishie hapo, tujiulize kwanini aliunga mkono Wapalestina, kwanini aliunga mkono MPLA na si FNLA au Unita! Kwanini aliegemea sana ZANU na si ZAPU. Kwanini Salim Ahmed Salim , Balozi wa Tz UN alisimama kidete China kurejeshwa
Why Dodoma na si Tabora??
Hili swali linajibika kwa kutazama sababu za kuhamishia makao Dodoma! zilizotolewa
Tukizipata hizo nadhani tunaweza kuelewa ni kwanini Dodoma.
 
1. Reli ya Mtwara -- Nachingwea ilijengwa kwa ajili ya mradi wa kilimo cha Karanga wa serikali ya Uingereza. Baada ya mradi huo kufeli reli nayo ikafa na wahusika wakashawishika kuing'oa.

2. OAU na sasa AU wana mila / utamaduni mbaya wa kufumbia macho ukatili na unyama wa watawala wa Kiafrika.

Serikali kuu ya Nigeria ilishindwa kulinda usalama wa wananchi wa Biafra waliokuwa wakiuawa na ndugu zao haswa toka kaskazini ya Nigeria. Juhudi za kutafuta amani na kuitaka serikali kuu ya Nigeria iwahakikishie wananchi wa Biafra usalama wao ziligonga mwamba.

Katika mazingira hayo serikali ya Tanzania iliamua kuunga mkono maamuzi ya wananchi wa Biafra kujitenga.

NB:

Suala la Biafra limeishajadiliwa JF mara nyingi. Uamuzi wa Tanzania kuitambua Biafra haujawahi kupingwa kwa hoja zenye ushawishi zaidi ya kurudiarudia hoja ya " msimamo wa OAU. "

Lakini pia muuliza swali anaweza kuwa ame-set mtego, kwamba kwanini Nyerere alitetea Biafra hakutetea Wazanzibari.🤣

Jibu ni kwamba Mwalimu alikosea kufumbia macho unyama wa serikali ya Mapinduzi.

Lakini OAU pia ilikuwa na wajibu wa kukemea na kulaani mauaji na unyama wa serikali iliyokuwa ikiongozwa na Sheikh Abedi Karume.


Mbona unamsafisha Nyerere?
Reli iling'olewa na waingereza?..
Yaani Reli iling'olewa kwa sababu karanga hakuna?..watu sio muhimu?
 
..nadhani kwa kiasi fulani Machifu walipewa jina baya ili kuhalalisha maamuzi ya serikali ya Tanu kufuta uchifu.

..mfano mzuri ni propaganda dhidi ya Mangi Marealle kwamba alikwenda UN na kupinga petition ya Tanganyika kupata uhuru.

..USHAHIDI wa maelezo na maoni ya Mangi Marealle UN upo na alieleza mambo tofauti kabisa na ambavyo Watanganyika tumedanganywa kwa muda mrefu.

..Mangi Marealle alitetea Watanganyika kupewa uhuru na alisisitiza suala la Watanganyika kupatiwa nafasi nyingi zaidi za masomo kama maandalizi ya kujitawala.

..Mangi Marealle pia aliulizwa kuhusu nafasi ya Machifu ktk Tanganyika huru na jibu lake lilikuwa anapendekeza tuige mfumo wa Machifu wa Ghana.

..Hata Nyerere alipokuwa UN ali acknowledge mchango wa Mangi Marealle kabla yake kuwa unashabihiana na msimamo wake na wa Tanu.

..Hili suala anayetaka kujiridhisha aende kwenye ARCHIVE za UN atakuta mahojiano ya Mangi Marealle, na ya Mwalimu Nyerere, mbele ya kamati ya udhamini ya UN.

..Ukiacha hilo, kuna ushahidi wa Machifu wa Usukumani kuunga mkono Tanu. Kazi ya kuwashawishi Machifu wa Kisukuma ilifanywa na Paul Bomani.

..Nyerere alimheshimu Paul Bomani kutokana na ushawishi wake na kazi kubwa alivyofanya kuipenyeza Tanu kanda ya Ziwa.

..Jambo lingine ni mchango wa FEDHA toka Kanda ya Ziwa kwa ajili ya kuendesha Tanu. Nimewahi kusoma kwamba kuna wakati kanda ya Ziwa ilikuwa inachangia 2/3 ya fedha za kuendesha chama. Kama sijakosea habari hii iko ktk kitabu cha John Illife kuhusu historia ya Tanganyika.

Cc Nguruvi3, Mamndenyi, Pascal Mayalla, Fundi Mchundo, MALCOM LUMUMBA
JK,
Huwa mara kwa mara huwaambia wasomaji wangu kuwa hakuna mzalendo aliyeshiriki katika kupigania uhuru wa Tanganyika ambae utamkosa katika Nyaraka za Sykes.

Nimekutana na Paul Bomani ndani ya nyaraka hizi hebu mtafute hapo chini:

''Uongozi wa TAA Makao Makuu ulianza kampeni ya nchi nzima kuueleza umma matokeo ya safari ya Kirilo kwenye Umoja wa Mataifa kuhusu mgogoro wa ardhi ya Wameru na vilevile kuchangisha fedha za kupeleka msafara mwingine katika Umoja wa Mataifa kuueleza umoja huo kuwa Tanganyika ilikuwa chini ya udhamini na Watanganyika walikuwa sasa na haki ya kudai uhuru wao.

Kamati ya TAA ya watu watatu iliyowajumuisha Saadan Abdu Kandoro, Japhet Kirilo na Abbas Sykes iliundwa kwa ajili hiyo.

Ally Sykes akiwa mweka hazina msaidizi wa TAA aliombwa ampelekee Kirilo hawala ya posta Usa River kama nauli ya kumwezesha kusafiri hadi Dodoma kujiunga na ile kamati ya watu watatu.

Kulikuwa hakuna huduma ya fedha katika posta ya Usa River na fedha zile zilikaa hapo kwa muda bila ya kuchukuliwa hadi hapo zilipopelekwa posta ya Arusha mjini ambako Kirilo alizichukua.

Kuanzia tarehe 26 Septemba, 1953 kwa takriban mwezi mmoja ile kamati ilitembelea na kuhutubia mikutano ya hadhara, ikikusanya fedha Dodoma, Mwanza, Bukoba, Ukerewe, Tarime, Musoma na Shinyanga.

Rais wa chama cha TAA, kanda ya ziwa, Paul Bomani aliipokea ile kamati ya watu watatu na kuhutubia mikutano pamoja nao katika jimbo lote. Bomani aliwaambia wanachama wa TAA na wananchi wote mjini Mwanza kuhusu umuhimu wa kuchanga fedha kwa kwa kusudio hilo.''

(Report ya Lake Province Kwa Kifupi Iliyotolewa na Bwana Abbas K. Sykes, Sykes’ Papers.) haina tarehe lakini ni ya mwaka wa 1953.

1640404490982.png
 
..Ndugu yangu jitahidini msiingize Ukristo vs Uislamu.
Huyo kijana kila anapochangia lazima atumbukize udini. Hatari sana
..CCM wanapotubamiza hawaangalii dini ya mtu.
Wote ni wahanga wa mfumo ulioasisiwa na CCM
..Mimi naendelea kusisitiza kwamba bila CCM kutikiswa huku Tanganyika, Zanzibar haiwezi kuomboleza.
Tena hapa ndipo nashangaa sana! Mfano nasikia kuna tume ya kuandaa tume huru ya uchaguzi.
Mwaka 2010 kulikuwa na tume huru kule Zanzibar iliyoundwa na CCM na CUF
CUF wakaporwa matokeo mbele ya ''tume huru''


ACT, the defunct CUF hawajajifunza kosa, huwezi kuwa na tume huru ukawa na sheria zile zile ukadhani tume huru itakuwa na maana, usipobadilisha sheria kandamizi tume huru ya uchaguzi inapatikanaje na itasaidiaje?

ACT wanataka Zanzibar huru na waathirika sana wa 'Tume huru' za Bara na visiwani walikuwepo Dodoma bila kujali maumivu yaliyowakuta miaka nenda miaka rudi. Wameshiriki mchakato wa 'Tume huru' na si katiba

Bila katiba mpya, si Bara si visiwani maumivu yatakuwa yale yale

ACT na CCM Zanzibar watarudi wakituaminisha ''Nyerere ni mbaya'' fursa za kujikomboa zikipita. Nadhani katiba mpya itakayokuja na Tanganyika itakuwa mwarobani

Othman Masoud, VP wa SMZ kutoka ACT aliondoka bunge la katiba kama mwanasheria mkuu kwasababu ya Katiba mpya, leo kapewa pipi keshasahau alisimamia nini anataka 'tume kama ya Jecha'' huu kama si usalati kwa Maalim sijui uitweje. Othman kalamba asali

ACT wanachokiona kama 'neema' ni upendeleo si haki, akikalia kiti mwingine yatafutika.
Fadhila si haki, kwanini wakubali fadhila kwa kubadilisha na haki?

Wazanzibar wanadhani kero zimeisha bila kujua ni fadhila tu, chochote wanachokiona si kisheria

Katiba mpya ingesaidia pande zote! leo watapewa 'tume huru' na kubaki chini ya kivuli cha Tanganyika.

Bila uwepo wa Tanganyika Zanzibar itabaki mkoa! halafu watarudi hapa kulalamika wanaonewa n.k. wakati leo wao ndio mpini wa kusaidia shoka la CCM

Wzbar hawakumbuki walipewa fursa na JK,zimebaki hadithi ni peremende hazipo kisheria.

Sheria zinatoka katika Katiba si tume huru ya 'CCM, Vyama vya Briefcase na ACT'

Kuna tatizo la kufikiri, hili la katiba hasa kwa upande wa visiwani ACT ni tatizo kubwa.
ACT wanakubali pipi kama watoto wadogo? Wamesau Maalim (RIP) na chaguzi ?

Huku bara ACT ni wahanga wa kila uchaguzi uliyofanyika, hakuna cha kujifunza hapo?

Tume huru itakusaidiaje ikiwa umekamatwa na Polisi kabla ya kuchukua Form?
Tume huru inakusaidiaje ikiwa imeundwa na Mwenyekiti wa CCM!
Tume huru inakusaidije kama Msajili ''atafuta chama chako'' kabla ya uchaguzi
Tume huru inasaidiaje ukiwa na ''kesi'' ya kutakatisha fedha kabla ya uchaguzi na hakuna dhamana

ACT wafikiri ikiwa ushiriki wao utatoa matokeo tofauti na yale ya tume huru chini ya Jecha.

ACT wajiulize ni sheria gani inayompa Msajili nguvu za kuanzisha mchakato unaondelea?

ACT, ikiwa Tume huru itaundwa na '' Masheikh na Maaskofu na ACT'' bila CCM, hakuna kitakachofanikiwa kwasababu zipo sheria nyingi tu katika maandiko CCM watazitumia

Katiba mpya maana yake ni kutengeneza mazingira ya uwanja sawa na hilo CCM hawalitaki ndio maana wanakuja na peremende za tume huru!

Zitto watazame Mrema , Lipumba na Cheyo ni mifano hai, I know you're better than..... wewe ni smart please don't go down the rabbit hole

Samahani nimetoka katika mada lakini ni muhimu kulieleza hili

Pascal Mayalla Yericko Nyerere
 
JK,
Huwa mara kwa mara huwaambia wasomaji wangu kuwa hakuna mzalendo aliyeshiriki katika kupigania uhuru wa Tanganyika ambae utamkosa katika Nyaraka za Sykes.

Nimekutana na Paul Bomani ndani ya nyaraka hizi hebu mtafute hapo chini:

''Uongozi wa TAA Makao Makuu ulianza kampeni ya nchi nzima kuueleza umma matokeo ya safari ya Kirilo kwenye Umoja wa Mataifa kuhusu mgogoro wa ardhi ya Wameru na vilevile kuchangisha fedha za kupeleka msafara mwingine katika Umoja wa Mataifa kuueleza umoja huo kuwa Tanganyika ilikuwa chini ya udhamini na Watanganyika walikuwa sasa na haki ya kudai uhuru wao.

Kamati ya TAA ya watu watatu iliyowajumuisha Saadan Abdu Kandoro, Japhet Kirilo na Abbas Sykes iliundwa kwa ajili hiyo.

Ally Sykes akiwa mweka hazina msaidizi wa TAA aliombwa ampelekee Kirilo hawala ya posta Usa River kama nauli ya kumwezesha kusafiri hadi Dodoma kujiunga na ile kamati ya watu watatu.

Kulikuwa hakuna huduma ya fedha katika posta ya Usa River na fedha zile zilikaa hapo kwa muda bila ya kuchukuliwa hadi hapo zilipopelekwa posta ya Arusha mjini ambako Kirilo alizichukua.

Kuanzia tarehe 26 Septemba, 1953 kwa takriban mwezi mmoja ile kamati ilitembelea na kuhutubia mikutano ya hadhara, ikikusanya fedha Dodoma, Mwanza, Bukoba, Ukerewe, Tarime, Musoma na Shinyanga.

Rais wa chama cha TAA, kanda ya ziwa, Paul Bomani aliipokea ile kamati ya watu watatu na kuhutubia mikutano pamoja nao katika jimbo lote. Bomani aliwaambia wanachama wa TAA na wananchi wote mjini Mwanza kuhusu umuhimu wa kuchanga fedha kwa kwa kusudio hilo.''

(Report ya Lake Province Kwa Kifupi Iliyotolewa na Bwana Abbas K. Sykes, Sykes’ Papers.) haina tarehe lakini ni ya mwaka wa 1953.

View attachment 2056300
Mkuu Maalim Mohamed Said , asante kwa hii. Ili kuitendea haki hazina ya historia uliyonayo na kumbukumbu ya picha ulizonazo, dhamiria kwa mwaka huu, anzisha a weekly TV Program, ambacho ni kipindi chako, kuzungumzia historia ya uhuru wa Tanganyika na kipindi hicho kirushwe kwenye TV zetu.
Napendekeza jina la kipindi liwe
Simulizi za Historia ya Harakati za Uhuru wa Tanganyika na Mohamed Said
Heri ya Krisimasi
P
 
Mkuu Maalim Mohamed Said , asante kwa hii. Ili kuitendea haki hazina ya historia uliyonayo na kumbukumbu ya picha ulizonazo, dhamiria kwa mwaka huu, anzisha a weekly TV Program, ambacho ni kipindi chako, kuzungumzia historia ya uhuru wa Tanganyika na kipindi hicho kirushwe kwenye TV zetu.
Napendekeza jina la kipindi liwe
Simulizi za Historia ya Harakati za Uhuru wa Tanganyika na Mohamed Said
Heri ya Krisimasi
P
Pascal,
Tusaidiane Mimi sijui hata pa kuanzia.
 
Pascal,
Tusaidiane Mimi sijui hata pa kuanzia.
Unapo ila kwa vile hujijui, unajikuta haujaichangamkia fursa.
  1. Kitu cha kwanza chenye thamani kubwa katika utayarishaji wa kipindi cha TV, ni kuwa na interesting contents. Harakati za Uhuru ni interesting contents.
  2. Kitu cha pili ni kumpata msimulizi mwenye kipaji, hiki unacho.
  3. Kitu cha tatu ni cha gharama sana kwenye utengenezaji wa TV program ni Production Cost. Gharama za kuandaa kipindi zikihumuisha vifaa na location. Kwa vile kila mara nakuona ukialikwa TV mbalimbali, Azam, TBC, ITV, Imaan etc, next time ukialikwa, waeleze hao waalika wako utayari wako kufanya nao a weekly/Monthly program as a resource person, ili TV ndio igharimie production cost na kutoa airtime kurusha bure.
  4. Mimi nina vifaa vya production kupitia kampuni yangu ya PPR, ila kwa vile PPR ni an independent company, nikikufanyia production, TV watadhani nimelipwa mamilioni hivyo hawatakubali kurusha kipindi bure nao watataka kulipwa mamilioni na kugeuka ni biashara wakati lengo ni public information program.
  5. Vinginevyo wewe mwenyewe unaweza kabisa kuanzisha your own production, na ukawauzia contents hao TV, tena hadi BBC, DW na VOA wanaweza kulipia karibu mitaa huu Je, Una Kipaji cha Utangazaji? Jinsi ya Kujiajiri Utayarishaji na Utangazaji Vipindi Vyako vya TV
Kipaji hiki unacho.

P
 
OK nadhani ulikuwa hujazaliwa CCM walipoandamana na mabango!
Sidhani kama una hoja !

Umeandika kitu chengine Na unajibu vyengine

Rudi kwenye post yako Soma baadaye ujibu swali
 
Ni hivi, ukristo au Uislam havihusiani na mapinduzi.
Swali ni rahisi sana '' Je mapinduzi ya Zanzibar ni Halali au Haramu'? Ni kitu gani kigumu hapo

Havihusiani kwani hakuna mtu aliyeuwawa?
 
Sijui ninachokuuliza ni rahisi, ikiwa '' Nyerere anatuhumiwa kuleta mapinduzi'' je, mapinduzi ya Zanzibar ni HALALI au ni HARAMU?
Ninaweza kukuuliza maswali juu ya kiwango chako cha elimu, please nifahamishe .

Huu mjadala ni mzito na watu waliopo ni wazito, Mohamed Said anajua.

Mi nadhani ukamalizie homework ya sayansi kimu wakati ukifika urejee hapa.
Kama unadhani bado una mtima, hebu tueleze Mapinduzi ya Zanzibar ni Halali au ni Haramu?

Halali maana yake ni nini kwa unavyofahamu wewe Na haramu maana yake nini kwa elimu yako wewe
 
Collectiveness au Ujamaa unahitaji nidhamu ya hali ya juu. Kuwaamini wachache watunze pesa za wengi inahitaji kuweka kanuni madhubuti za adhabu itakayowapata wabadhirifu. Bila hivyo yanatokea yaliyotokea Urusi na hata hapa kwetu.
Nidhamu km ya china ukizingua kidogo tu kitanz kinakuhusu
 
Sijui ninachokuuliza ni rahisi, ikiwa '' Nyerere anatuhumiwa kuleta mapinduzi'' je, mapinduzi ya Zanzibar ni HALALI au ni HARAMU?
Ninaweza kukuuliza maswali juu ya kiwango chako cha elimu, please nifahamishe .

Huu mjadala ni mzito na watu waliopo ni wazito, Mohamed Said anajua.

Mi nadhani ukamalizie homework ya sayansi kimu wakati ukifika urejee hapa.
Kama unadhani bado una mtima, hebu tueleze Mapinduzi ya Zanzibar ni Halali au ni Haramu?

SHEREHE ZA MAPINDUZI ZICHUNGUZWE

Na Sheikh Ponda Issa Ponda

IFIKAPO Januari 12, 2022, tutashuhudi watu wakisherehekea Mapinduzi yaliyofanywa visiwani Zanzibar mwaka 1964. Ni vizuri tujadili japo kwa ufupi tukio hilo.

Zanzibar ilifanya uchaguzi wa nne wa kidemokrasia (wa vyama vingi), Julai 1963. Chama kilichoshinda uchaguzi huo kilikuwa Zanzibar Nationalist Part (ZNP-ZPPP).

Uchaguzi huo ulihusisha vyama kadhhaa kikiwemo chama kikubwa cha Afroshiraz Part (ASP).

Tarehe 10, Desemba 1963, Waingereza kwa idhini ya Umoja wa Matafa, walitoa Uhuru wa Zanzibar kwa chama kilichoshinda uchaguzi huo (ZNP-ZPPP)

Siku 30 baada ya Uhuru huo, yalifanyika Mapinduzi yakidaiwa kuongozwa na chama kilichoshindwa katika uchaguzi (ASP).

Waandishi nguli wa historia, na watu mashuhuri wameeleza kuwa siku ya Mapinduzi hayo, dawati la ufundi lilishikwa na Watanganyika pamoja na Waingereza.

Wahandisi wa pande hizo mbili wakiwa Unguja, upande wa Tanganyika uliwakilishwa na Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa, Bwana Emil Mzena na upande wa Waingereza uliwakilishwa na Balozi wao T. S. Crossthwit.

Pia wamethibitisha mipango, silaha (bunduki, mapanga) na majeshi ya Mapinduzi viliandaliwa na kuingizwa Zanzibar kutoka Tanganyika. Pia majeshi (ya majini), ya Waingereza yalionekana yakishiriki moja kwa moja katika Mapinduzi Zanzibar.

Kwa namna hiyo, Tanganyika na Uingereza walishiriki Mapinduzi hayo ya kuiondoa madarakani serikali halali ya taifa huru la Zanzibar (1964).

Aidha mwaka huohuo (1964), Jeshi la Wananchi Tanganyika lilipanga na kutekeleza Mapinduzi yaliyomuondoa Ikulu Rais Julius Kambarage Nyerere kwa zaidi ya siku mbili kabla ya kurejeshwa tena.

Mwalim Nyerere akihutubia mkutano wa hadhara Januari 25, 1964, jijini Dar es Salaam, alieleza namna alivyorudishwa madarakani:

“Nililazimika kuomba msaada wa Mwingereza. Kwa bahati akakubali. Kikosi kikawasili sasa ni shwari. Nasikia maneno ya wajinga kwamba eti Waigereza wamerudi Tanganyika.”

Kwa muktadha huo, mwaka 1964, Waingereza walishiriki kupindua serikali ya Zanzibar na kuzuia Mapinduzi dhidi ya Serikali ya Tanganyika.

Mapinduzi ya Zanzibar yamehusisha mambo mengi mazito yakiwemo haya:-

Moja: Kuondolewa madarakani serikali iliyochaguliwa na wananchi.

Pili: Kuondoshwa kiti cha Taifa hilo (Zanzibar) katika Umoja wa Mataifa (UN).

Tatu: Kuonfolewa Uhuru wa Wazanzibari kujiamulia mambo yao wenyewe.

Nne: Mauaji ya kinyama, makubwa, yaliyowaathiri wataalamu wa taifa hilo pamoja na viongozi wengine wakiwemo Maulamaa wakubwa wa Kiislamu.

Tano: Ufisadi wa ubakaji wa mabinti, wake za watu na dhulma ya ardhi, mashamba, majumba na mali nyingine mbalimbali za raia.

Mmoja wa mamluki wa Mapinduzi hayo kutoka nchini Uganda, John Okelo anasema, katika Mapinduzi hayo waliwauwa Wazanzibari wapatao 11,995.

Izingatiwe kwamba, Zanzibar kabla na baada ya Uhuru palikuwa na utawala wa kikatiba na vyombo vya maamuzi ya kisheria na kisiasa kama vile Mahakama, Tume ya Uchaguzi na vingine vilikuwepo.

Serikali ya Waziri Mkuu Mohamed Shamte (ZNP-ZPPP), iliyopinduliwa na Wazanzibari waliouliwa, hawakuwa na tuhuma wala hatia yoyote iliyowasilishwa na kuthibitishwa katika mamlaka hizo za serikali.

Sasa kwanini katika Twitter yangu ya tarehe 23, 2021, nilihoji Je ni nani aliyeruhusu Mapinduzi Zanzibar na kuzuia Mapinduzi Tanganyika? Pia nikauliza “alifanya hivyo kwa idhini na maslahi ya nani?

Nilihoji hayo kwa sababu mwezi ujao Januari 12, 2022, waliofanya Mapinduzi ya Zanzibar wanatarajia kusheherekea Mapinduzi yao.

Na wanahamasisha wakitaraji kuungwa mkono na watu mbalimbali wakiwemo Waislamu na Wakristo.

Mimi kama kiongozi wa dini nalazimika kuangalia matukio na sherehe hizo katika mizani ya haki, uadilifu na ubinadamu.

Katika mizani hiyo, sioni haki yoyote wala busara ya mtu anayejali hisia za utu na umoja wa umma kujifaharisha kwa Mapinduzi ya namna hiyo.

Nadhani busara ni kufanya kama waliyofanya Kanisa Katoliki nchini Rwanda kujuta na kuwaonba radhi Wanyarwanda kwa maovu yaliyofanywa na baadhi ya viongozi wake katika mauwaji ya kimbari mwaka (1994).

Waingereza, Watanganyika (na Wazanzibari-ASP), hawakuwa na uhalali wowote kwa yale waliyowafanyia Wazanzibari na taifa lao mwaka (1964).

Ndio maana tunasema “Mapinduzi yachunguzwe”.

25. 12. 2021
 
Kuzungumza ukweli ndani ya jamii iliyozea kuishi kwa wongo na ulaghai ni sawa na kutupa lulu kwa nguruwe.
Suala siyo tu kuzungumza, bali kufanya mjadala ambao unaweza kujenga na kulibadilisha vema taifa letu.
Kama watanzania tungekuwa ni watu wa kupenda ukweli basi tungekuwa tumeshabadilika zamani sana.

Watanzania sio exception. Dunia nzima iko hivyo tangu enzi za kale. Kristo alisulubiwa kwa kusema na kuishi ukweli. Kusema na kusimamia kweli ni kujitoa mhanga. Ndio maana whistleblowers wanafanyiwa mpango wa ulinzi.

Wewe sema ukweli uwe huru one day itasaidia taifa kupigania kujenga na kusimamia misingi ya demokrasia na utawala bora kama jinsi the American dream (among others) ilivyopambaniwa.
 
Sidhani kama anaweza hata kusema kama kulikuwa na utumwa Zanzibar. Kwake yeye kila kitu anakiangalia kwa darubini la dini.
Tulijadiliana nae sana kuhusu imani yake kuwa ni waislamu wa Gerezani peke yake ndio wanaostahili kuenziwa kama waasisi wa madai ya Uhuru. Ukimsikiliza utadhani ni wakina Sykes peke yao ndio waliominywa na Nyerere ( kitu ambacho si kweli kwa sababu kwa muda mrefu ni wakina Sykes, Munanka na wachache wengine ndio walioruhusiwa kuwa mabepari wakubwa Tanzania) akisahau wakina Oscar Kambona, Christopher Kassanga Tumbo na wengine.

Amandla...
Hata habari za wamisheni (wakristo) kuvamia na kuua babu zetu pwani ya Africa mashariki si ajabu akashindwa kueleza, yeye kwake ni kina bibi titi tu, yaani habari za wakatili wa kireno na kijerumani katu hatokueleza
 
Nimeandika nimefuta, nimeandika tena nikafuta, nikaandika tena nikafuta, mwishowe nikaona niache tu!
Ningeandika nilichokusudia ningeonekana mzandiki na mtu mwenye chuki dhidi ya Baba wa taifa...
Ukiandika uzi kuhusu hiyo ishu usisahau kunitag mkuu
 
Hata habari za wamisheni (wakristo) kuvamia na kuua babu zetu pwani ya Africa mashariki si ajabu akashindwa kueleza, yeye kwake ni kina bibi titi tu, yaani habari za wakatili wa kireno na kijerumani katu hatokueleza
Hizo atazieleza sana kwa sababu anaamini uovu wote umeletwa na wazungu. Kwake yeye wote waarabu hawakufanya lolote baya na babu zetu walijipeleka wenyewe sokoni kujiuza.

Amandla...
 
Mbona unamsafisha Nyerere?
Reli iling'olewa na waingereza?..
Yaani Reli iling'olewa kwa sababu karanga hakuna?..watu sio muhimu?

..tuko hapa kueleza facts vile ambavyo tumezielewa.

..sio suala la kumsafisha au kumchafua mtu yeyote.

..kwa uelewa wangu reli iling'olewa mwaka 1963 na sababu zinazoelezwa ni kufeli kwa mradi wa karanga maeneo ya kusini.

..utakumbuka malengo ya ujenzi wa reli hiyo ilikuwa mradi wa karanga.

..labda kujiridhisha zaidi tungetafuta taarifa za matumizi ya reli hiyo by the time serikali inaamua kuing'oa. JE, ilikuwa inatumika au ilikuwa imekufa?
 
Hizo atazieleza sana kwa sababu anaamini uovu wote umeletwa na wazungu. Kwake yeye wote waarabu hawakufanya lolote baya na babu zetu walijipeleka wenyewe sokoni kujiuza.

Amandla...
Kwamba huchagua madhila baina ya mjerumani alichinja kichwa cha Mkwawa na muarabu wa pembe za ndovu?
 
Back
Top Bottom