Fundi Mchundo
Platinum Member
- Nov 9, 2007
- 10,448
- 8,705
Kwa hiyo unaangalia unaona afadhali ya watu waliowaswaga ndugu zetu kama ng'ombe ( na kubonda vichwa vya watoto walioshindwa kutembea) mpaka Bagamoyo, wengine wakatubebesha hizo pembe za ndovu,halafu wakatuvusha kama dagaa na kutupiga mnada kama vile wanauza maharage. Baada ya hapo wengine tukapelekwa kulima, wengine kazi za nyumbani na wengine walipelekwa uarabuni, Mauritius ( kufanya kazi kwenye mashamba ya miwa), wengine walihasiwa ili waweze kuwahudumia wake na vimada wao bila kuingia tamaa, kuliko mtu aliyemkata kichwa mtu mmoja ( kwa maelezo yako)? Wazungu wa magharibi hawakuwa malaika, nao walitufanyia uovu mwingi sana lakini katika eneo letu uovu waliotufanyia haufikii ambao walitufanyia waarabu na uzao wao. Kufungia macho uovu huo kwa sababu za kidini sio sawa.Kwamba huchagua madhila baina ya mjerumani alichinja kichwa cha Mkwawa na muarabu wa pembe za ndovu?
Amandla...