1963: Rais wa Jamhuri ya Tanganyika, Julius Nyerere akiweka pini katika koti la Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Bw. U Thant

Hii ni kwa faida ya wasomaji ili kuondokana na kuangalia maandishi katika herufi au utamu wa lugha iliyotumika. Kuna 'between the lines'' nitakutembeza ili usimeze tu, kutafuna ni muhimu
Serikali ilimtuma kijana mmoja kutoka Masasi aliyesoma katika shule za misheni, Frederick Mchauru kuwahutubia wafanyakazi na kuwaomba wasimamishe mgomo na warudi kazini.
Shika neno Misheni
Mchauru alikuwa Mmakonde kutoka Newala.
Alielimishwa St. Joseph's College, Chidya na St. Andrewís College, Minaki.
Tazama shule kwa majina yake ya zamani na sasa. Ni makusudi kabisa
Mwaka 1946, Mchauru alikuwa amerudi kutoka LondonUniversity akiwa amehitimu masomo yake na kuanza kazi mjini Tabora kama Assistant Social Development Officer.
Hapa ndipo cheo chake kikatajwa. Katika uandishi wa kawaida ilitakiwa Mchauru awe identified kwa wadhifa '' serikali ilimtuma Assistant Social Development Office...' halafu ndio academic qualification. Haikuwa hivyo kwasababu maalumu
Wafanyakazi waliokuwa kwenye mgomo walimpigia kelele wakimtaka anyamaze huku wakimwita msaliti.
Hii sentensi ilipaswa kuungana na ile kabla ya 'kuadhibiwa'' lakini imechomekwa hapo makusudi ili kuweka neno ''Usaliti''
Inashangaza namna shule za misheni zilivyowatengeneza watumishi wa serikalini walio wasomi wawe watiifu na waaminifu kwa dola.
Ahaa hapa anafunguka, kwamba safari yote hapo juu ililenga neno Misheni. Hivyo Mchauru ''anatambuliwa kama Mmisheni, shule zinatajwa na innuendo ya Msaliti inachomekwa
Wasomi hawa mara nyingi walijikuta wanasigana na wale waliokuwa wakipinga ukoloni na udhalimu.
Well, waliokuwa wanapinga udhalimu ni Wazee wake

Kwa ufupi shughuli nzima ya hukumu ya Mchauru iliunganishwa na umishenari.
Tatizo ni pale anapodai hao wamisheni walikuwa watiifu kwa serikali ya kikoloni.
Hivi Nyerere alikuwa mtiifu? Dr Kyaruzi, akina Kirilo, akina Kasanga Tumbo n.k.!

Na mwisho anasema wasomi wa kimeshanari walikuwa wanasigana na wale waliopinga ukoloni ambao ni wazee wake kama special Branch office Kitwana Kondo na Ali Mwinyi Tambe
 
Sasa nimeelewa kwa nini Mohamed Said anasema babu yake hakupata utambuzi aliostahili kama muasisi wa TRAU. Lakini tuanze kwanza na historia.

Chama cha wafanyakazi wa reli ( Railway African Association) kiliundwa mwaka 1945 ( sio 1955) na tarehe 10 Septemba 1947 wanachama wake 2000 waliunga mkono mgomo mkubwa uliokuwa unaendelea nchini mwao. Wafanyakazi wa shirika la reli la East African Railways and Harbour( EARH) wa Morogoro, Kilosa, Dodoma na Tabora waliunga mkono juhudi hizo. Tawi la RAA Tabora lilitaka wafanyakazi wa kiafrika walipwe sawa na wahindi.

Mwaka 1957 TRAU, ikiongozwa na Katibu Mkuu wake E.N.N Kanyama kilipunguza madai ya nyongeza ya mshahara kutoka 35% hadi 15% ili kulingana na madai ya R.A.U (K). General Manager wa EARH , Bw. J.R. Farquharson,aliyakataa madai hayo akisema kuwa shirika lake halina uwezo wa kulipa kiwango hicho.

CHRISTOPHER Kasanga Tumbo alichaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa TRAU mwaka 1959 na akaiondoa TRAU katika chombo cha arbitration na serikali kilichoitwa ALJSAC. Katika kikao cha Agosti 1959, wafanyakazi wa TRAU walikubaliana kugoma. Kabla ya mgomo kikao cha pamoja cha vyama vya wafanyakazi wa reli Tanganyika, Uganda na Kenya kilifanyika mjini Mwanza ambapo walikubaliana kuanzisha the National Confederation of Railwaymen (East Africa). Serikali ya mkoloni ilikataa kutambua muungano huo lakini ari ya ushirikiano kati ya vyama hivi ilizidi kukua.

Mwezi Oktoba 1959, TRAU walianzisha mgomo ambao ulisababishwa na shirika kukataa viongozi wao wapya likidai kuwa hawakuchaguliwa.
Mwezi Novemba 1959, mgomo ulitokea Nairobi baada ya mnyapara wa kizungu kuwatukana wafanyakazi wa kiafrika. Ilipofika tarehe 14 Novemba wafanyakazi 26000 walikuwa kwenye mgomo. Mgomo ulitulizwa na wafanyakazi walirudi kazinini tarehe 30 Novemba. Hofu kubwa ya serikali ya kikoloni ilikuwa mgomo huo kuenea mpaka Tanganyika na Uganda.

Hata hivyo TRAU, wakiongozwa na Christopher Kasanga Tumbo walipanga kuanza mgomo tarehe 18 Desemba lakini waliusiticha baada ya kuanza mazungumzo na serikali ya kikoloni ambayo ilikuwa inakabiliwa na mgomo wa wafanyakazi 1200 wa Posta ulioanza tarehe 24 Desemba. Kwa vile wafanyakazi wa posta waliahidiwa kulipwa mshahara wa shilingi 150 kwa mwezi kama kima cha chini, TRAU walipata matumaini kuwa nao madai yao yatakubaliwa kwa sababu hayakupishana sana na ya wafanyakazi wa Posta.

Tarehe 4 Desemba EARH walipendekeza nyongeza ya sh 4 kwa mwezi. Vyama vya wafanyakazi wa reli wa Afrika Mashirika walikutana Nairobi tarehe 30 desemba na tarehe 2 Januari 1960 TRAU walikataa pendekezo la EARH. Tarehe 5 Januari EARH wakaongeza dau kwa shilingi tatu kwa wafanyakazi wa daraja la chini kabisa. TRAU wakakataa.

Tarehe 9 Februari 1960 mgomo wa wafanyakazi wa reli ulianza rasmi. Siku ya pili wafanyakazi 12,000 walikuwa katika mgomo. Mgomo huo uliendelea kwa wiki 11 na nusu ingawa tarehe 15 Februari TAGWU walikubali malipo ya sh. 107 kwa kima cha chini. TFL, chini ya Kawawa hawakupendezwa na mgomo huo kwa sabau waliona kuwa utaathiri matayarisho ya makabidhiano ya nchi na hivyo walikataa kuunga mkono na walimtaka Gavana Reginald Turnbull aingilie kati.

Christopher Kasanga Tumbo alikaribishwa Brussels kukutana na uongozi wa ICFTU ( International Confederation of Free Trade Unions). Alikuwa huko kati ya tarehe 29 Machi na 4 Aprili. Aliporudi, Charles Millard wa ICFTU na Pieter De Vries wa ITWF waliongoza majadiliano na EARH.

Christopher Kasanga Tumbo alipendwa sana na wanachama wa TRAU kwa sababu msimamo wake ulikuwa nafasi zote zinazoshikiliwa na wazungu zishikiliwe na waafrika weusi. Nyerere aliupinga msimamo huo kwa sababu alijua kuwa hapakuweko waatanganyika weusi wa kutosha kujaza nafasi zilizokuwa zinashikiliwa na wazungu. Ndio maana TANU ilihakikisha nafasi ya Christopher Kasanga Tumbo inachukuliwa na Michael Kamaliza ambae alipokuwa waziri wa kazi alishauri serkali kuwa TFL iwekwe chini ya wizara yake.

Tofauti na Mohamed Said alivyosema, Mchauru hakuwa mtumishi wa serikali ya wakoloni kwa sababu waliokuwa wanapambana na TRAU walikuwa viongozi wa EARH. Bila shaka mgalatia mmisheni Mchauru aliajiriwa na EARH. Serikali ya "kikoloni" ilikaa pembeni mpaka TANU ilipomuomba Gavana aingilie suala hilo.

Sehemu kubwa ya historia hii nimeitoa kwenye kitabu kinachoitwa " Building A Peaceful Nation" kilichoandikwa na Paul Bjerk ili kuthibitisha sio Tandau peke yake ndie aliyeandika historia ya vyama vya wafanyakazi Tanganyika.

Ukiisoma, utaona kuwa tofauti na Mohamed Said anavyotaka kutuaminisha, wamisheni walikuwa msitari wa kutetea haki za wafanyakazi wenzao. Kinachomuuma sio kutotambuliwa mchango wa TRAU bali ni kwa nini sifa zote anapewa mgalatia Christopher Kasnga Tumbo na sio babu yake Salum Abdallah. Anachoshindwa kukubali ni kuwa wasomi wa misheni walihitajika sana kuweza kukaa meza moja kupambana na wazungu katika msingi wa usawa. Ni hasira zile zile anazoonyesha kwa mgalatia Julius Kambarage Nyerere kuenziwa kuliko Abdul Sykes. Kitu kibaya anachofanya ni kuvika vyote hivi joho la udini la wagalatia kutowatendea haki waislamu akisahau conveniently kuwa Mwalimu Nyerere aliwaweka kizuizini wagalatia wenzake wengi tu ikiwa pamoja na Christopher Kasanga Tumbo aliyediriki kuanzisha chama cha Peoples' Democratic party kupinga uanzishwaji wa mfumo wa chama kimoja. Upofu huu ndio unaotufanya tuendelee kupingana nae.

Amandla...

cc. Nguruvi3
Kama kuna majibu yanapaswa yapitie aya moja hadi nyingine.Kujibu kwa ujumla hakujibu hoja husika.

Mohamed Said hoja haipigwi rungu.
Kilichopo hapo juu ni hoja, habari za ugeni na nani anakuja kwa nani hazijibu hoja iliyopo mezani.
 
Muhimu kuandika lakini ukipatwa uvivu andika Tawasifu yako kisha umueleze kwa mapana, kwasababu Tawasifu yako ni muhimu sana ukizingatia kumekuwepo na hila na fedhuli za hawa jamaa zetu kukubehua na kukutweza kana kwamba ni mtu usie na mbele wala nyuma umetunga ngano ukazichapa, somo yako mwana wa kiqureish Muhammad Ibn Abdallah( Swalla na salaam zimuendee) yeye katika kuwasilisha kwake Amana (Qur-aan na Dini kwa ujumla) amekuwa akitweza kila Leo, baadhi wakimtuhumu alichanganyikiwa
Makala...
Watu wengi wananiambia kuwa niandike kitabu cha maisha yangu.

Wanasema kuwa nina mengi sana ambayo inafaa yakaandikwa kwenye tawasifu yangu ili yajulikane.

Lakini ajabu mimi naona kama vile sina umuhimu wa kiasi cha mimi kuandika kitabu cha maisha yangu watu wakasoma.

Labda hii inachangiwa na kuwa hapa nyumbani watu wa kawaida kama mimi hawaandiki historia za maisha yao.

Tumezoea maisha ya viongozi ndiyo huandikwa.

Lakini nimeona Nigeria ukiingia duka la vitabu au maktaba ya chuo utakuta tawasifu zimeandikwa na wanasiasa, wafanyabiashara nk.

Nimeshuhudia hili Chuo Kikuu Cha Ibadan katika duka la vitabu la chuo na maktaba ya chuo.

Lakini najua kwa nini nyinyi ndugu zangu mnataka niandike.

Nilikuwa na rafiki yangu anaitwa Salim Himidi.

Yeye ni Mngazija Mzanzibari na aliporejea Ngazija baada ya kumaliza masomo yake Ufaransa, baada ya Comoro kupata uhuru alikuwa Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje.

Kwa miaka ambayo nilifahamiana na Salim Himidi nilijifunza mengi na kila tukikutana nilikuwa namshikilia kuandika maisha yake.

Yeye kila nikilileta suala hili la yeye kuandika jibu lake lilikuwa, ''In Shaa Allah,'' lakini haandiki.

Nilikwenda Paris ambako alikuwa akiishi uhamishoni na tulikuwa na muda mkubwa sana wa mazungumzo ya maisha yake.

Serikali ambayo yeye aliitumikia ni ile iliyopinduliwa na mamluki kutoka Afrika ya Kusini wakiongozwa na Bob Denard.

Aliyonieleza katika siasa za Ngazija na Afrika kwa upande mmoja na dunia kwa upande wa pili yalinisisimua sana.

Nilimsihi sana rafiki yangu anyanyue kalamu.

Salim Himidi amefariki bila kuandika chochote.

Nilimwandikia taazia.

Natambua umuhimu wa kuandika lakini najiambia mbona niliyoandika yote yako katika hifadhi mimi nina kipi muhimu cha kujieleza?

1640838588690.png

Kifungua kinywa na Salim Himidi Paris katika hoteli ya rafiki yetu Muhindi kutoka Zanzibar
1640837278831.png

Fundi Mchundo kasema hivi '' Tanganyika haijawahi kuwa koloni la Mwingiereza''. Fundi yupo sahihi 101%. Mtafute Mohamed Said (PM)umuulize maana akisema utaelewa zaidi.
Hizo ni tungo tu za wakoloni, ukifahamu maana ya koloni utaelewa hizo asilimia mia na moja

Leo unamkadhibisha Moh lakini hizo propaganda za "League of Nations" unazipokea pasina kuchuja, eti Tanganyika halikuwa Koloni la muingereza,lakini hawatakueleza watanganyika ni lini walimuita Muingereza katika ardhi yao, nyinyi vijana kwakweli mnatatizo kubwa hata kama mnaghabika wakati mwingine tukiwaeleza ukweli
 
Sasa nimeelewa kwa nini Mohamed Said anasema babu yake hakupata utambuzi aliostahili kama muasisi wa TRAU. Lakini tuanze kwanza na historia.

Chama cha wafanyakazi wa reli ( Railway African Association) kiliundwa mwaka 1945 ( sio 1955) na tarehe 10 Septemba 1947 wanachama wake 2000 waliunga mkono mgomo mkubwa uliokuwa unaendelea nchini mwao. Wafanyakazi wa shirika la reli la East African Railways and Harbour( EARH) wa Morogoro, Kilosa, Dodoma na Tabora waliunga mkono juhudi hizo. Tawi la RAA Tabora lilitaka wafanyakazi wa kiafrika walipwe sawa na wahindi.

Mwaka 1957 TRAU, ikiongozwa na Katibu Mkuu wake E.N.N Kanyama kilipunguza madai ya nyongeza ya mshahara kutoka 35% hadi 15% ili kulingana na madai ya R.A.U (K). General Manager wa EARH , Bw. J.R. Farquharson,aliyakataa madai hayo akisema kuwa shirika lake halina uwezo wa kulipa kiwango hicho.

CHRISTOPHER Kasanga Tumbo alichaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa TRAU mwaka 1959 na akaiondoa TRAU katika chombo cha arbitration na serikali kilichoitwa ALJSAC. Katika kikao cha Agosti 1959, wafanyakazi wa TRAU walikubaliana kugoma. Kabla ya mgomo kikao cha pamoja cha vyama vya wafanyakazi wa reli Tanganyika, Uganda na Kenya kilifanyika mjini Mwanza ambapo walikubaliana kuanzisha the National Confederation of Railwaymen (East Africa). Serikali ya mkoloni ilikataa kutambua muungano huo lakini ari ya ushirikiano kati ya vyama hivi ilizidi kukua.

Mwezi Oktoba 1959, TRAU walianzisha mgomo ambao ulisababishwa na shirika kukataa viongozi wao wapya likidai kuwa hawakuchaguliwa.
Mwezi Novemba 1959, mgomo ulitokea Nairobi baada ya mnyapara wa kizungu kuwatukana wafanyakazi wa kiafrika. Ilipofika tarehe 14 Novemba wafanyakazi 26000 walikuwa kwenye mgomo. Mgomo ulitulizwa na wafanyakazi walirudi kazinini tarehe 30 Novemba. Hofu kubwa ya serikali ya kikoloni ilikuwa mgomo huo kuenea mpaka Tanganyika na Uganda.

Hata hivyo TRAU, wakiongozwa na Christopher Kasanga Tumbo walipanga kuanza mgomo tarehe 18 Desemba lakini waliusiticha baada ya kuanza mazungumzo na serikali ya kikoloni ambayo ilikuwa inakabiliwa na mgomo wa wafanyakazi 1200 wa Posta ulioanza tarehe 24 Desemba. Kwa vile wafanyakazi wa posta waliahidiwa kulipwa mshahara wa shilingi 150 kwa mwezi kama kima cha chini, TRAU walipata matumaini kuwa nao madai yao yatakubaliwa kwa sababu hayakupishana sana na ya wafanyakazi wa Posta.

Tarehe 4 Desemba EARH walipendekeza nyongeza ya sh 4 kwa mwezi. Vyama vya wafanyakazi wa reli wa Afrika Mashirika walikutana Nairobi tarehe 30 desemba na tarehe 2 Januari 1960 TRAU walikataa pendekezo la EARH. Tarehe 5 Januari EARH wakaongeza dau kwa shilingi tatu kwa wafanyakazi wa daraja la chini kabisa. TRAU wakakataa.

Tarehe 9 Februari 1960 mgomo wa wafanyakazi wa reli ulianza rasmi. Siku ya pili wafanyakazi 12,000 walikuwa katika mgomo. Mgomo huo uliendelea kwa wiki 11 na nusu ingawa tarehe 15 Februari TAGWU walikubali malipo ya sh. 107 kwa kima cha chini. TFL, chini ya Kawawa hawakupendezwa na mgomo huo kwa sabau waliona kuwa utaathiri matayarisho ya makabidhiano ya nchi na hivyo walikataa kuunga mkono na walimtaka Gavana Reginald Turnbull aingilie kati.

Christopher Kasanga Tumbo alikaribishwa Brussels kukutana na uongozi wa ICFTU ( International Confederation of Free Trade Unions). Alikuwa huko kati ya tarehe 29 Machi na 4 Aprili. Aliporudi, Charles Millard wa ICFTU na Pieter De Vries wa ITWF waliongoza majadiliano na EARH.

Christopher Kasanga Tumbo alipendwa sana na wanachama wa TRAU kwa sababu msimamo wake ulikuwa nafasi zote zinazoshikiliwa na wazungu zishikiliwe na waafrika weusi. Nyerere aliupinga msimamo huo kwa sababu alijua kuwa hapakuweko waatanganyika weusi wa kutosha kujaza nafasi zilizokuwa zinashikiliwa na wazungu. Ndio maana TANU ilihakikisha nafasi ya Christopher Kasanga Tumbo inachukuliwa na Michael Kamaliza ambae alipokuwa waziri wa kazi alishauri serkali kuwa TFL iwekwe chini ya wizara yake.

Tofauti na Mohamed Said alivyosema, Mchauru hakuwa mtumishi wa serikali ya wakoloni kwa sababu waliokuwa wanapambana na TRAU walikuwa viongozi wa EARH. Bila shaka mgalatia mmisheni Mchauru aliajiriwa na EARH. Serikali ya "kikoloni" ilikaa pembeni mpaka TANU ilipomuomba Gavana aingilie suala hilo.

Sehemu kubwa ya historia hii nimeitoa kwenye kitabu kinachoitwa " Building A Peaceful Nation" kilichoandikwa na Paul Bjerk ili kuthibitisha sio Tandau peke yake ndie aliyeandika historia ya vyama vya wafanyakazi Tanganyika.

Ukiisoma, utaona kuwa tofauti na Mohamed Said anavyotaka kutuaminisha, wamisheni walikuwa msitari wa kutetea haki za wafanyakazi wenzao. Kinachomuuma sio kutotambuliwa mchango wa TRAU bali ni kwa nini sifa zote anapewa mgalatia Christopher Kasnga Tumbo na sio babu yake Salum Abdallah. Anachoshindwa kukubali ni kuwa wasomi wa misheni walihitajika sana kuweza kukaa meza moja kupambana na wazungu katika msingi wa usawa. Ni hasira zile zile anazoonyesha kwa mgalatia Julius Kambarage Nyerere kuenziwa kuliko Abdul Sykes. Kitu kibaya anachofanya ni kuvika vyote hivi joho la udini la wagalatia kutowatendea haki waislamu akisahau conveniently kuwa Mwalimu Nyerere aliwaweka kizuizini wagalatia wenzake wengi tu ikiwa pamoja na Christopher Kasanga Tumbo aliyediriki kuanzisha chama cha Peoples' Democratic party kupinga uanzishwaji wa mfumo wa chama kimoja. Upofu huu ndio unaotufanya tuendelee kupingana nae.

Amandla...

cc. Nguruvi3
Bwana Nguruvi3 kijana wako pendwa Fundi Mchundo katika gazeti lake hapa ameandika "serikali ya Mkoloni" nawe unasema aliposema Tanganyika halikuwa Koloni la muingereza alikuwa sahihi 101%, sijui tumuelewe lipi! Eti Jagina wewe umemuelewa?
 
Hivi huu upupu mnaoandika na kumpachika Mohamed Said ni kwa dhamira ipi?

Kuna mahala katika hitimisho la hili gazeti umeandika "anachoshindwa kukubali ni kuwa wasomi wamisheni walihitajika sana kuweza kukaa meza moja kupambana na wazungu katika msingi wa usawa"

Hakuna mahala Moh hajakubali, bali ndani ya Kitabu chake kaeleza mengi, kwa uwazi namna Mkoloni alivyojipandia mbegu ya kumpinga yeye mwenyewe na hii ni tamathali maaruf hata huko mashuleni, mashuhur kwamba wapigania uhuru walipatikana kutoka katika veterani wa vita vya dunia, wasomi wa shule za kimisheni na wafanyakazi wa serikali za wakoloni ' inashangaza wewe kujitutumua eti kubainisha kanakwamba Moh anafanya khiyana kueleza hayo, Moh hakumuacha mtu katika Kitabu chake, na iko siku aliandika "hakuna katika wapigania uhuru ambae alikosa katika nyaraka za sykes kutoka katika pembe za Tanganyika" na nyaraka hizo ndizo Moh alizitafiti na Akazichapa katika Kitabu chake
 
Bwana Nguruvi3 kijana wako pendwa Fundi Mchundo katika gazeti lake hapa ameandika "serikali ya Mkoloni" nawe unasema aliposema Tanganyika halikuwa Koloni la muingereza alikuwa sahihi 101%, sijui tumuelewe lipi! Eti Jagina wewe umemuelewa?
Kenya ilikuwa koloni la Uingereza. German East Africa ilikuwa koloni la Uingereza. Uganda haikuwa koloni la Uingereza. Zanzibar haikuwa koloni la Uingereza.

Amandla ..
 
Kuna sehemu nilisema niliandika Kasnga. Nilikosea. Nilimaanisha Kasanga. Na kuna wakati naandika Kassanga wakati namaanisha Kasanga. Kuna mahali nilisema Mchauru alikuwa muajiriwa wa EARH. Kwa vile sina taarifa za ajira yake inawezekana alikuwa kweli muajiriwa wa serikali ya wakati ule na alitumwa kwenda kuwatuliza waliokuwa wamekusanyika.
Sikukosea niliposema kuwa Mohamed Said alitumia uwepo wa Mchauru kujenga hoja yake ya kuwa wamisheni walikuwa vibaraka, wasaliti na waislamu ndio waliokuwa wakiongoza mpambano dhidi ya serikali ya wakati ule. Nguruvi3 ameeleza vizuri sana jinsi anavyoleta hoja hiyo.

Amandla...
 
Makala...
Baada ya historia ya akina Prof. Kimambo, John Illife na mfano wao kuandikwa ilikuwa hapo pahitimishwe.

Mimi kuandika kitabu cha Abdul Sykes nilikuwa nimegeuza kila kitu.

Niliwaudhi watu wengi kupita kiasi.

Wangekuwa na uwezo wangeweza kuniita muongo lakini mtu yeyote wa akili za kawaida akisoma kitabu cha Abdul Sykes anajua haraka kabisa kuwa huu ndiyo ukweli wenyewe.

Huyu kijana vipi atajua haya yote?

Anataja hadi no. ya kadi ya TANU ya Abdul Sykes na ya mdogo wake Ally na za Wakenya na za Wanyasa ndani ya TANU.

Hata Irving Wallace asingeweza kutunga hadithi kama hii.

Swali wanalobakianalo ni kwa nini historia ya hawa wazalendo imefutwa na kwa amri ya nani na kwa sababu gani?

Hebu fikiria ingekuwa sijakuonyesheni picha za TRAU za babu yangu akiwa na Kassanga Tumbo nani angeniamini?

Fikiria ningekuwa sina taarifa za Special Branch zinazoeleza mkutano wa Abdul Sykes na Jomo Kenyatta Nairobi 1950 au barua alizokuwa anaandika Ally Sykes kwenda kwa Kenneth Kaunda 1953.

Ninapoweka historia hizi hakika panakuwa na ukimya na hakuna atakae hata kuuliza maswali ili ajue zaidi wote huwa kimya.

Hawaipendi historia hii.

Wanachofanya wanaangukia kwenye, "Bashing."

Nisingeyajua haya ninayokuwekeeni hapa kama nisingezaliwa na watu hawa na katika kipindi kile.

Mimi tofauti yangu na wengine ni kuwa siji hapa na kile alichoandika Mzungu mimi nakuja hapa na nakala za wahusika wenyewe.

Hawa Wazungu wanakuja kwangu kwanza.

Babu yangu alimtupia usoni posa mshenga aliyeileta nyumbani kwetu kwa Salum Abdallah kutoka kwa kijana aliyetaka kumuoa shangazi yangu Mwalimu Tatu bint Salum.

Huyu mposaji yalimfika yale kwa kuwa alikuwa kibaraka hakugoma mgomo wa 1960.

Babu alimwambia yule mshenga kwa hasira, "Nendeni mkaoe kwa vibaraka wenzenu."

Kuitwa kibaraka wakati wa kupigania uhuru lilikuwa jambo baya kabisa.

Nina mengi.
 
Mwalimu kuna Mahala unanikosha sana ni kama daktari ambae amekwisha tambua ugonjwa wa mteja wake baada taarifa kutoka maabara, kuna hoja unawajibu kwa akili sana, hakika umebarikiwa Kaka na umetoka kwenye mifupa ya wazazi wenye akili
 
Hebu tupitishe pande zote mbili kuhusu hichi kikao cha sykes na kenyatta, upande wa mpigania uhuru na huu wa ujasusi namna walivyokimulika kikao hiki na mfano wa hiki
 
Kenya ilikuwa koloni la Uingereza. German East Africa ilikuwa koloni la Uingereza. Uganda haikuwa koloni la Uingereza. Zanzibar haikuwa koloni la Uingereza.

Amandla ..
Hizo ndizo ngano wanasomeshwa watoto wa sekondari kwamba Tanganyika halikuwa Koloni na muingereza, nimekuuliza nani aliwaita waingereza? Na kwanini waliwaandama wapigania uhuru
 
Mwalimu kuna Mahala unanikosha sana ni kama daktari ambae amekwisha tambua ugonjwa wa mteja wake baada taarifa kutoka maabara, kuna hoja unawajibu kwa akili sana, hakika umebarikiwa Kaka na umetoka kwenye mifupa ya wazazi wenye akili
Makala...
Ngoja nikufahamishe kitu.
Mimi nimesomeshwa mlango wa mnakasha na maalim wangu Sheikh Haruna.

Kwanza kaniambia kuwa ingia kwenye mjadala kwa nia ya kusoma na kusomesha.
Soma kama unajadiliana na mjuzi na somesha kama unaejadiliananae hana elimu ya mnachojadili.

Usiingie katika mjadala kwenda kushinda.
Muheshimu mwenzako ili na yeye akuheshimu.

La umemtambua kuwa hana adabu basi nendanae kwa tahadhari na jaribu kumfunza adabu kwa hekima.

Mjadala ukigeuka matusi, kebehi na kejeli acha jua keshashindwa.
Mengi kanisomesha na akisisitiza sana kwenye adabu ya elimu.

Jambo lingine na hili ndilo linalonipa nguvu mimi.
Mimi Dar es Salaam ndiyo kwetu.

Wazee wangu ni wapigania uhuru na ndiyo waasisi wa African Associatio na Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika na TANU na ndiyo waliompokea Julius Nyerere.

Kama Mwalimu alikuwa na ndugu hapa Dar es Salaam na kama alikuwa na watu anaoweza kusema nikipatwa na lolote nitawakimbilia basi hao walikuwa wazee wangu.

Kama alikuwa Mwalimu ana mama hapa Dar es Salaam mama huyo alikuwa Bi. Mruguru bint Mussa, mama yake Abdul Sykes.

Kama Bi. Mugaya Nyang'ombe mama yake Mwalimu alikuwa na ndugu hapa Dar es Salaam basi ndugu huyo alikuwa Bi. Mruguru bint Mussa.

Uhusiano haukuwa wa kupambana na Mwingereza peke yake bali watu hawa waliishi kidugu kabisa.

Sasa hawa wenzangu wao hawana historia niliyonayo mimi.

Wao wananiletea mimi nakala za watu wala hawahusiki kwa nasaba wala utafiti wa historia hii.

Mimi wazee wangu walifutwa kwenye historia ya TANU chama walichokiasisi na kukijenga na wakapigania uhuru wa Tanganyika chini ya chama hicho.

Hao wanaoletwa hapa kwangu wazee wao waliunda TANU na historia yao kufutwa?
Hii ndiyo tofauti baina yetu.

Nitakuwekea hapa visa viwili.

Kisa cha kwanza taharuki iliyotokea siku ilipodhaniwa Nyerere kalishwa sumu katika chakula nyumbani kwa Abdul Sykes anataka kuuliwa na maadui zake.

Hii katika miaka ya 1950.

Kisa cha pili siku Nyerere aliposimamaisha msafara wake Mtaa wa Sikukuu na Lindi akatoka ndani ya gari yake kumsalimia Mama Abdul, Bi. Mruguru.

Hii ilikuwa miaka ya 1970.

Mimi ndiyo mtafiti pekee ulimwenguni kote ukimtoa John Iliffe aliyesoma Nyaraka za Sykes.

Historia hii ninayo mimi peke yangu.
Mtafute hata mtu mmoja wa dawa aliyesoma nyaraka hizi upone maradhi yako.

Hutompata.
Utakufa.

1640876584269.png
 
Huyu ni mtanganyika mwingine aliyeandika historia ya Tanganyika kutokana na experience zake na za rafiki na ndugu zake lakini hajadai kuwa ndugu zake au wagalatia wenzake wanahitaji kuheshimiwa zaidi ya wengine kutokana na michango yao.

Kijana Fundi Mchundo

Amandla....

cc. Nguruvi3
Ahsante sana, kwa kitabu , Shukran sana. Nilikitafuta na umekileta kwa wakati mujarabu

Nimekipitia tena kuna sehemu nikashtuka. Mwenzetu alituambia gazeti la kwanza Tanganyika ni Zuhura.
Kulikuwa na Tanganyika Times 1926 Nyerere akiwa na miaka 4 na kisha Dar es Salaam Times

Muhimu sana huyu bwana kaandika experience yake na waliomzunguka, hana madai ya kwamba alichoandika ndio alfa na omega na wala hajadai hati miliki ya Historia
 
Kaka Mohamed Said nadhani kuna haja yakukisoma hichi Kitabu, huyu muandishi nadhani atawafunza hawa wenzetu wakaidi wa historia, nimefurahi sana kimeletwa na huyu Fundi Mchundo kuna mengi naimani yatambadilisha fikra zake akiwa "open minded na open hearted"
 
Ahsante sana, kwa kitabu , Shukran sana. Nilikitafuta na umekileta kwa wakati mujarabu

Nimekipitia tena kuna sehemu nikashtuka. Mwenzetu alituambia gazeti la kwanza Tanganyika ni Zuhura.
Kulikuwa na Tanganyika Times 1926 Nyerere akiwa na miaka 4 na kisha Dar es Salaam Times

Muhimu sana huyu bwana kaandika experience yake na waliomzunguka, hana madai ya kwamba alichoandika ndio alfa na omega na wala hajadai hati miliki ya Historia

Screenshot_20211230-184058_WPS Office.jpg
 
Back
Top Bottom