1963: Rais wa Jamhuri ya Tanganyika, Julius Nyerere akiweka pini katika koti la Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Bw. U Thant

1963: Rais wa Jamhuri ya Tanganyika, Julius Nyerere akiweka pini katika koti la Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Bw. U Thant

Ni kweli huwezi kumlinganisha Nyerere Na Abdul ,
Nyerere alikuwa kibaraka wa Waingereza Na kanisa Katoliki Hakuna siri hapo
Jagna,
Unaandika umeghadhibika na mimi naelewa hamaki zako.

Mwalimu wangu aliyenisomesha ilm ya mnakasha yaani majadiliano alikuwa akisema, ''Chunga ulimi wako lisikuponyoke neno ukajakujuta kwa nini nimelisema.''

Akawa anatufunza anasema,''Neno likitoka huwezi kulirudisha ndani kwa hiyo chukueni sana tahadhari.''

Mnakasha huu hadi sasa una watu 7732 ''and counting,'' na hii si idadi ndogo.
Tusiwapoteze.

Umewavutia watu mnakasha huu bila shaka kwa haya wanayosoma.

Juzi nimeeleza hapa jamaa walionifuata na kuniambia tufanye mjadala wa wazi kwenye ukumbi na urushwe usikike mubashara kwenye TV na FM Station.

Wameniambia, ''Mohamed sisi hatuwezi kuona hawa watu wanakutukana na wanatukana wazee wetu waliompokea Nyerere na wakapigania uhuru wa nchi hii pamoja na yeye sisi tukawa pembeni tunakutazama tu.''

Sikupenda kuingia katika haya maneno waliyonambia.
Lakini lipo jambo kubwa hapa.

Lakini moja ya mambo waliyoniambia ni kuwa siwajibu inavyotakikana.
Wao wanataka nirejesho moto kwa moto.

Kibri kwa kibri, kebehi kwa kebehi,kejeli kwa kejeli.

Jibu langu kwao lilikuwa kuwa mimi nafahamika katika duru za uandishi na nimejenga heshima yangu siwezi kufanya hivyo.

Nikawapa mfano nikawaambia hawa wenzangu ni mfano wa askari wa msituni hawana sura wala hawavai unifomu ya jeshi lolote hakuna anaewajua wanaweza wakasema lolote linalowajia.

Hawana sheria yoyote ya uungwana inayowafunga.
Hawa ni ''guerilla,'' askari wanaopigana ndani ya msitu.

Nikahitimisha kwa kuwaeleza kuwa sidhani kama wanaweza wakajitokeza sura zao zionekane tufanya mjadala.

Jagna,
Wewe unarejesha moto kwa moto.

Jambo lolote ukilitia upole linapendeza na hii ni kauli ya Mtume SAW.
Tia upole katika majibu yako yatapendeza.

Mimi ninayo majibu naweza nikayatoa lakini naogopa kuponyokwa na neno nisije nikajuta.
Kitabu cha Abdul Sykes kipo kwa Kiingereza na kwa Kiswahili huu sasa mwaka wa 23.

Sasa tunakwenda toleo la 5.
Hawa wasomaji ndiyo wakunishuhudia mimi.

Kitabu hiki kimefunika kitabu cha Kimambo na Temu (1969) na kitabu cha Chuo Cha CCM Kivukoni (1981).

Toleo moja na kitabu kimekufa.

Sina sababu ya kugombana na mtu yeyote kuhusu historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika lisinitoke neno nikajuta kwani majuto ni mjukuu.

Sikuandika maisha ya Abdulwahid Kleist Sykes ili kumdogosha Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Laiti nia yangu ingekuwa ni kumdhalilisha Julius Nyerere ningekiua kitabu changu kwani hakuna asiyejua ukubwa wa Mwalimu na mchango wake katika kupigania uhuru wa Tanganyika.

Lakini mimi naujua pia mchango wa wazee wangu kwa Mwalimu na kwa harakati ya kupigania uhuru hadi ukapatikana.

Historia hii ilifutwa na mimi nimeiandika leo inasomwa.

Yapo niliyoyaeleza hapa na yapo mengi sikuona haja hata ya kuyaeleza katika kitabu.
Hayamo ingawa ni mambo muhimu na ya kupendeza.

Nilifanya hivyo kwa makusudi kabisa kwa nia ya kuweka staha kwani wazalendo hawa wenyewe kwa wenyewe walifanyiana hisani nyingi.

Nilichelea wasije watu wakageuza kauli zangu na hapa haya yamefanywa na wakiyarudiarudia wakiamini kuwa yatashusha heshima yangu na ya wazee wangu.

Jagna,
Haya ndiyo niliyotaka kukueleza.
Fanya mnakasha lakini ondoa ghadhabu.

Aliniambia msemaji mmoja Profesa wa African History Northwestern University baada ya kusikiliza mhadhara wangu kuwa ilikuwa baada ya kusoma kitabu cha Abdul Sykes ndipo alipofahamu kuwa historia aliyakuwa akisomesha ilikuwa si kamili.

Northwestern Universiity ndiyo wanaongoza dunia nzima katika historia ya Afrika.
Chuo hiki ukija na kitabu cheny elimu mpya lazima watakualika chuoni kwao ukazungumze.

1641096706615.png
 
View attachment 2065693
NiMekuelewa vizuri sana, Na nakuomba samahani sana,Na nimeelewa lengo lao hawa watu nalo ni uchafuzi. Shukrani sana,
 
Jagna,
Unaandika umeghadhibika na mimi naelewa hamaki zako.
Mohamed, Jagina hajaghadhabika kwa hili namtetea, na kama kaghadhabika si wewe wa kumsema au kumuonya. Jagina ni mwanafunzi mzuri tu katumia maarifa aliyopata
Juzi nimeeleza hapa jamaa walionifuata na kuniambia tufanye mjadala wa wazi kwenye ukumbi na urushwe usikike mubashara kwenye TV na FM Station.Wameniambia, ''Mohamed sisi hatuwezi kuona hawa watu wanakutukana na wanatukana wazee wetu waliompokea Nyerere na wakapigania uhuru wa nchi hii pamoja na yeye sisi tukawa pembeni tunakutazama tu.''
Kwanza, kuna misconceptions. Kukoselewa si kutukanwa.
Mathalani hoja ya kwamba AbdulWahid Sykes hajafanya mkutano wowote wa siasa nje ya Gerezani Dar es Slaam inakuwaje kauli iwe tusi?Ni wapi wazee wako wametukanwa?

Huko kwenye TV sitokei kumbe kuna shari, hapana! ''Watu hawatakaa pembeni'' na nikikumbuka kulikuwa na kuapizana 'utakufa' thank you but no thanks !
Kibri kwa kibri, kebehi kwa kebehi,kejeli kwa kejeli.
Scholars hawajui kibri au kejeli, wao wanajua ''challenge''
Nikawapa mfano nikawaambia hawa wenzangu ni mfano wa askari wa msituni hawana sura wala hawavai unifomu ya jeshi lolote hakuna anaewajua wanaweza wakasema lolote linalowajia.
Hawana sheria yoyote ya uungwana inayowafunga.Hawa ni ''guerilla,'' askari wanaopigana ndani ya msitu.
Masuala ya kitaaluma yanaongozwa na weledi si uungwana! ndiyo maana scholars wanatumia challenge katika maongezi. Kwa wale ''wanosomeshwa'' sijui taratibu zao !!
Sikuandika maisha ya Abdulwahid Kleist Sykes ili kumdogosha Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Well, Miaka miachache tulikukemea ulipoonyesha picha za Mwalimu za kumdhalilisha.

Umeulizwa Abdul Sykes alifanya mkutano nje ya Gerezani? Wapi na lini kama ilitokea?
Jibu la kwanza; Abdul Sykes alifanya na Kenyatta na timu ya Kapenguria. Tukasema si jibu

Jibu la Pili ; Abdul Sykes hakuweza kuzungumza na Mwalimu alikuwa hana pesa! ridiculous
Kwamba Mwl hakuwa na 'bank roll'' sijui hilo jibu linahusiana vipi na hoja ya Abdul na mikutano

Majibu yote yanamhusisha Nyerere si kwasababu ya hoja iliyotolewa bali kuhakikisha kuna ulinganifu wa Abdul Sykes na Nyerere na hasa lengo kubwa kumdhalilisha.

Kwamba, huyu hakuwa na pesa angefanya nini kama si ukoo wa Sykes.

Nadhani ukoo wa Sykes haufurahishwi na maneno ya kumdhalilisha Mwalimu.

Akina Sykes hawakutenda kwa ajili ya kumdhalilisha Mwalimu walikuwa na wito, tuwashukuru tusiwape mitihani isiyo na maana. Ndiyo maana nilikuambia unapokwenda si pazuri.

Huwezi kuulizwa swali la Abdul Sykes ukamuingiza Mwl na Pesa bila sababu.

Unajitahidi sana kumdhalilisha Nyerere kwa ''innuendos' lakini historia inagoma.

Hivi si wewe uliyeleta picha za Suti za Abdul na kisha kuweka picha ya Mwl na Kaptura!!
Laiti nia yangu ingekuwa ni kumdhalilisha Julius Nyerere ningekiua kitabu changu kwani hakuna asiyejua ukubwa wa Mwalimu na mchango wake katika kupigania uhuru wa Tanganyika.
Nia yako siku zote ni kumdhalilisha Mwl Nyerere, kwa wenye fikra hilo halina shaka

Hukuanza leo na hutumia sana njia za kumlinganisha Mwalimu na Abdul.
Ndiyo maana ulitumbukiza suala la pesa katika hoja ya mikutano ya Abdul Sykes!!! weird

Hukutaka kukubali Abdulwahid hakuwahi kufanya mkutano wa siasa Tanganyika nje ya Gerezani.

Kwako ukaona ni dhalili ukamtafuta mnyonge wako Nyerere ukamsukumia udhalili wa pesa na bank roll. Ni kama ule ule wa Mshume Kiyate kumpa Mwl pesa akienda sokoni bila pesa.

Acha! Mohamed, Nyerere anabaki kuwa Nyerere, Abdul anabaki kuwa Abdul.
Hawa watu wanastahili heshima zetu , haya maneno ya reja reja ya kuwadhalilisha hayafai!
Lakini mimi naujua pia mchango wa wazee wangu kwa Mwalimu na kwa harakati ya kupigania uhuru hadi ukapatikana.
Usiutumie mchango wa Wazee wako kama silaha ya kumdhalilisha Nyerere.
Si uungwana na nadhani wazee hawajisikii uzuri popote walipo.
Lengo lilikuwa kupigania uhuru . Tunachokifanya hapa si kuwadhalilisha ni kuweka historia sawa
Nilifanya hivyo kwa makusudi kabisa kwa nia ya kuweka staha kwani wazalendo hawa wenyewe kwa wenyewe walifanyiana hisani nyingi.
Ndio maana tunashangaa unapotumbukiza hoja za ''bank roll'' Nyerere hakuwa na Pesa n.k.

Yanahusu nini? Kama kuna hoja inayohusu hilo hakuna shida lakini wewe from no where unatafuta Nyerere unamuunganisha na Abdul Sykes halafu unamdhalilisha, si uungwana!

Kwa hili niwe katika record nimeghadhibika!
Kudhalilisha hawa wazee si jambo jema hata kidogo
 
NiMekuelewa vizuri sana, Na nakuomba samahani sana,Na nimeelewa lengo lao hawa watu nalo ni uchafuzi. Shukrani sana,
Jagina,
Kuna hofu kubwa sana katika historia ya uhuru wa Tanganyika.

Ukweli ni kuwa historia ya wazee wetu imefutwa na nimeandika historia kama ilivyostahili kuandikwa.

Historia hii ipo na inasomwa.
Yeyote akisoma kitabu ha Abdul Sykes ataona ule ukweli.

Kitabu cha maisha ya Mwalimu Nyerere ni matokeo ya mazungumzo kati ya Prof. Haroub Othman na Mwalimu kuwa historia yake imebadilishwa na kitabu cha Abdul Sykes kwa hiyo ni muhimu na yeye akaeleza nini nafasi yake katika kuunda TANU na mengineyo.

Nimehojiwa na Prof. Issa Shivji na jopo lake kuhusu Mwalimu Nyerere hasa uhusiano wake na Abdul Sykes.

Nimeeleza yote niliyokuwa nayajua na zaidi na nikawafungulia Maktaba.
Hata hivyo wameandika ambayo mimi kwa uchache naweza kusema tu si sawa.

Lakini mimi nachukulia kuwa labda hawakuniamini.
Kwa kuwa kitabu cha Abdul Sykes kipo wasomaji wataamua.

Jopo wamenipa kitabu cha Mwalimu Hard Cover kama shukurani yao kwangu kwa mchango wangu katika uandishi wa maisha ya Mwalimu.

Wakati mwingine si lazima kujibu kila kitu.

1641102899723.png
 
Historia hii ipo na inasomwa.
Yeyote akisoma kitabu ha Abdul Sykes ataona ule ukweli.
Ukweli kwa mujibu wako lakini si lazima uwe kwa mujibu wa Historia.
Una haki ya maoni lakini haki hiyo si lazima uwe ukweli wa hali halisi
Nimehojiwa na Prof. Issa Shivji na jopo lake kuhusu Mwalimu Nyerere hasa uhusiano wake na Abdul Sykes.
Nimeeleza yote niliyokuwa nayajua na zaidi na nikawafungulia Maktaba.
Hata hivyo wameandika ambayo mimi kwa uchache naweza kusema tu si sawa.
Lakini mimi nachukulia kuwa labda hawakuniamini.
Kwa kuwa kitabu cha Abdul Sykes kipo wasomaji wataamua.
Jopo wamenipa kitabu cha Mwalimu Hard Cover kama shukurani yao kwangu kwa mchango wangu katika uandishi wa maisha ya Mwalimu.
Wanataaluma siku zote huangalia jambo katika mizania ya ukweli wake na si mapokeo.
Kumbe wapo wengine!
 
Ukweli kwa mujibu wako lakini si lazima uwe kwa mujibu wa Historia.
Una haki ya maoni lakini haki hiyo si lazima uwe ukweli wa hali halisi

Wanataaluma siku zote huangalia jambo katika mizania ya ukweli wake na si mapokeo.
Kumbe wapo wengine!

Tumewazowea na hamna la kutuhadithia otherwise ungalijitokeza hapa Parwanja , kama wewe unajiamini , unaogopa kitu gani na nyinyi ndio mlio na ukweli ??
 
Nitaanza na kuzungumzia kitabu cha Dr. John Sivalon kilichoitwa "Kanisa Katoliki na Siasa ya Tanzania Bara kuanzia 1953 hadi 1985". Kitabu hiki kilichapishwa na Benedictine Publications Ndanda, Peramiho. Kilitokana na Doctoral dissertation ya Dr. Rev. John Sivalon iliyoitwa " Roman Catholicism and the Defining of Tanzanian Socialism 1955-1985" aliyoitetea mwaka 1990 katika Chuo Kikuu cha St. Michael's College, Toronto School of Theology. Dr. Rev. John Sivalon alikuwa Mkurugenzi wa Maryknoll Fathers and Brothers Africa. Ameandika sana kuhusu masuala ya Ukatoliki katika nyanja tofauti na ni Professor wa Theology. Kitabu chake kimekuwa cherry picked kuonyesha kuwa Kanisa Katoliki lilikuwa na ajenda ovu ya kutawala Tanzania na kuwanyima fursa waislamu.

Mimi ningependa kujua kwa wale waislamu ambao wanakubaliana na hii theory ya ubaguzi na nia ovu ya wakatoliki watuambie ni shule gani ya kikatoliki ilikuwa haipokei waislamu au watu wa madhehebu mengine. Ninavyojua mimi ni kuwa kuna wazazi wa kiislamu ambao hawakutaka watoto wao wasome katika shule hizo kwa hofu ya kuwa watarubuniwa ili waingie kwenye ukristu au watalishwa vyakula ambavyo ni haramu kwao. Hii haishangazi maana naamini hata sasa kuna wagalatia ambao hawako tayari kuwapeleka watoto wao Al Muntazir au Feza kwa hofu ya kubadili dini au kuvishwa hijab, vazi ambalo wanaliona ni ishara ya uislamu.

Watutajie vile vile vituo vya afya na hospitali ambazo zilikuwa zinakataa kuwahudumia waislamu. Ninavyojua mimi ni kuwa katika sehemu nyingi hospitali zinazothaminiwa kuliko za serikali kutokana na huduma bora na gharama nafuu ni zile zinazoendeshwa na makanisa. Mimi naamini ni haya matumizi mabaya ya maandiko ya Rev. Sivalon ndio yamewafanya publishers waache kukichapisha. Au mauzo madogo ya chapisho za awali.

Amandla...
Kijana Fundi Mchundo
Cc. Nguruvi3
Kaka Mohamed Said kijana wako Fundi Mchundo anaandika vyema sana, mbona humjibu? Mimi napendekeza mujibu wewe tupate radha
 
Mohamed Said angekuwa nchi nyingine wangemuenzi sio hapa kwetu ambako wajuaji ni wengi na mabwana wadogo, humu Moh anapicha hadi za 1970s akiwa kwenye 20s kijana mdogo mtafiti badala yake vijana wadogo kina Fundi Mchundo ambao nao wanapita njia hizo hizo wanakuja kumnanga kana kwamba hana jema, kweli? Iko wapi Nidhamu ya kitaaluma?
Huyu babu ni mhalifu tu! Anachokifanya ni kutumia udhaifu wa kundi fulani kutofikiri vizuri kuleta chuki za kidini.
Anatakiwa kulaaniwa na kufungwa kama mhalifu tu
 
Suala lingine ambalo ningependa kulizungumzia ni suala la kesi ya ardhi ya Meru ambayo Moham ameielezea kwa kirefu akisistiza ukaribu na uhusika mkubwa wa Abdul Sykes kama Katibu wa TAA na Abbas Sykes katika kuzunguka na Kirilo Tanganyika nzima kuwaelimisha watanganyika kuhusu kesi hiyo. Amesema Abdul Sykes, kama rafiki wa Easton ndie aliyezungumza nae ili kuwasaidia wameru kuandika petition kwenda UNO. Katika bandiko lote la tarehe 28 Aprili 2021, hamna alipomtaja Nyerere isipokuwa alipotoa utambuzi wa picha aliyosema ni ya waasisi wa TANU ambayo imeandikwa Dodoma 1954. Vile vile kuna picha yake na Abdulwahid Ally Sykes ambayo anasema ilipigwa nje ya nyumba ya Kirilo mwaka 1989. Nahisi huyu Abdulwahid ni mtoto wa Ally Sykes kwa sababu Abdulwahid Sykes alizaliwa 1924 na alifariki 1968.

Mimi simulizi yangu ya mgogoro wa ardhi ya wameru nita i "base" zaidi kwenye kitabu cha John IIiffe cha mwaka 1976 ambacho Mohamed amekitumia sana katika maandiko yake.

John IIiffe anasema petition kuhusu kesi hii ilitayarishwa na wameru wenyewe na kiongozi wao aliyekuwa anaitwa Raphael Mbise aliituma kwa Chief Koinange wa wakikuyu ili aipeleke Umoja wa Mataifa. Katika petition hiyo ya tarehe 9 Juni 1952, viongozi wa wameru waliomba kuwa wapewe nafasi ya kuwepo wakati inajadiliwa na Trusteeship Council. Ombi lao lilikubaliwa na wakaambiwa kikao kitakuwa tarehe 30 Juni 1952. Uliitwa mkutano wa hadhara ambao uliwachagua mwanasheria Seaton na Katibu wa Meru Citizens Union na TAA tawi la Arusha kwenda New York. Seaton aliweza kuondoka mapema lakini waingereza walimchelewesha Kirilo kuondoka. Seaton aliweza kutetea petition hiyo katika tarehe iliyopangwa lakini Kirilo alipata nafasi ya kufanya hivyo tarehe 21 July. Seaton alirudi Tanganyika moja kwa moja lakini Kirilo alipitia kwanza London, Uingereza ambako alikutana na Lord Fenner Brockway wa chama cha labour kujaribu kushawishi serikali ya Uingereza. Alikutana pia na Julius Nyerere ambae alikuwa yuko likizo kutoka Edinburg. Alikutana pia na Peter Koinange, Fred Kubai na Dr. Munyua Waiyaki na Semakula Mulumba wa Uganda kuhusu shauri lake. Wote hawa walimpa moyo na ushauri wa namna ya kuendelea

Mwezi Septemba aliandika barua ya pili TAA kuwauliza kama kuna kitu ambacho wangependa kiongezwe kwenye petition yake. Abdulwahid Sykes akamjibu na kumuambia kuwa hilo suala ni muhimu kwa waafrika wa Tanganyika lakini TAA hawana pesa yeyote ya kumsaidia. Iliffe anasema " In terms of political action TAA was a broken reed" ( ukurasa 502). Ikumbukwe hii ni TAA ya Abdul Sykes kabla Nyerere hajachaguliwa kuwa rais wake. Kirilo akajirudia nyumbani.

Kirilo na Seaton walirudi tena New York mwezi Novemba mwaka huo lakini hawakupata mafanikio waliyotegemea. UNO ilikubali kuwa kweli Muingereza alikuwa mkosaji lakini hamna haja ya wao kuwarudishia ardhi wameru. Kirilo alirudi Tanganyika mwaka 1953 ambako alikutana na Nyerere. Kirilo amesema kuwa ni Julius Nyerere na Kandoro ndio waliomshauri kuzunguka Tanganyika nzima kuwaelezea watanganyika kuhusu ukatili wa waingereza. Nadhani wakati huo Nyerere alikuwa tayari Rais wa TAA. Watu wengi wanaamini kuwa ni safari hii ya wakina Kirilo ndio ilibadilisha muelekeo wa siasa Tanganyika kuelekea kwenye kudai uhuru badala ya masuala ya mishahara na uwakilishi katika Legislative Assembly. Wakina Kirilo walijenga hoja kuwa njia pekee ya kuepukana na dhulma kama walizofanyiwa ni kupata uhuru. Tume kutoka UNO zilizotembelea Tanganyika kabla ya hii kesi zilishangazwa jinsi watanganyika walivyokuwa hawana habari na masuala ya uhuru. Migomo iliyokuwa inaendelea mara nyingi ilitokana na dhana ya kuwa mwenzao ametukanwa/amenyanyaswa kwa sababu ya rangi yake na /au kudai nyongeza za mshahara, au kulipwa mshahara sawa na wahindi.

Ikumbukwe pia kuwa Japhet alikuwa mgalatia na wameru wengi walikuwa waluteri. Hii inathibitisha kuwa ile dhana ya kuwa wagalatia walikuwa ni vibaraka wa waingereza kuwa ni ya uongo. Inathibitisha kuwa moto wa kudai uhuru ulishika kasi baada ya kuwashwa na wagalatia wa Meru. Moto huu usingekuwa na mafanikio kama ungebakia Gerezani peke yake.

Ukisoma maelezo ya waandishi wengine wa historia utatambua kuwa ingawa wakina Sykes walichangia sana juhudi za ukombozi wa nchi hii lakini sio kwa kiasi ambacho Mohammed anataka kutuaminisha. Aidha, juhudi hizi hazikufanywa na watu wa dini fulani au kabila fulani peke yao. Hawa mashujaa walijitambua zaidi kama sehemu ya ukombozi wa mwafrika na mtanganyika kuliko kujiona sehemu ya jeshi la dini yao dhidi ya wale wenye dini tofauti.

Amandla...

Cc: Nguruvi3
Kadhalika hapa Mohamed Said , Lakini nyinyi hamuelewi Moh yeye huyu ni mmanyema kadhalika ni mtu wa "riwaya" amesoma toka utotoni, amesikiliza na kuingiza, katika uandishi wake utagundua "wahusika" wake huwachora kwa ustadi sana kiasi cha kuwapa medali za shaba vitani, nachelea isije kuwa hilo ndilo lilimpelekea kuonekana anawainua sana wazee ijapokuwa hakushusha mtu hivyo hastahili kubagazwa kwakuwa mara zote kusudi lake ameandika ni kuandika historia ya wazee wake, yaani anatumia ile "poetic license" kustarehesha na kuelezea wazee jambo ambalo ni maaruf kwenye ulimwengu wa uandishi, Tawasifu ikikolezewa chumvi yavutia

Nimeandika hayo Kwa namna nilivyoelewa lakini kimsingi Mohamed Said Ana hoja ya kujibu hapo, japo katika kuweka sawa mizani ni wazi kila mpigania uhuru anastahiki kuwemo katika historia, unajua Fundi Mchundo kuna wakati najiuliza hivi hapakuwepo wanafunzi huko mashuleni ambao walishiriki namna moja au nyingine? Hapakuwepo viongozi wa kiroho kwa upande wa wakristo? Ni wazi kuna gap Moh kaliacha na vipi tutambana nae anadai kusudi lilikuwa ni kuwaonyesha waislam (wazee wake) waliosahaulika katika historia.
 
Tunamuelewa sana Mohammed. Ndio maana tunasema hatuna shida na yeye kuandika historia ya ndugu na jirani zake wa Gerezani. Tunasema anastahili pongezi na shukrani zetu kwa hilo.

Tatizo tulilo nae ni yeye kujipa hati miliki ya historia yetu na kutaka kuiandika upya kwa misingi ya udini na ukabila ambao wengi wa wazee wa Gerezani hawakuwa nayo. Hawa walijua nguvu zao na mapungufu yao ndio maana waliwakubali wagalatia wasomi na wenye vipaji kama Vedasto Kyaruzi na Julius Nyerere. Mimi sidhani kama babu yake Salum Abdallah alimuangalia Christopher Kasanga au Mchauru kwa jicho la udini. La hasha, aliwaona ni vijana ambao usomi wao umewaweka katika nafasi katika jamii yake. Anapofanya hivyo ndio anatutia hofu kuwa nia yake ni kupandikiza chuki katika jamii yetu ambayo haikuweko.

Jambo hilo ni hatari sana kwa sababu tofauti na hapo zamani vizazi vya sasa vinaweza kuishi bila kushirikiana kwa karibu na watu wa dini tofauti. Watu wanaweza kupata elimu yao kuanzia chekechekea hadi chuo kikuu katika shule zenye mlengo wa dini zao ( wagalatia wana zao na waislamu wana zao). Ule ushirikiano uliojengwa baada ya elimu kutaifishwa ili tusome kwa pamoja unazidi kupotea. Ndio maana ni muhimu kuwazukataza wakina Mohammed wanapochezea kiberiti sheli.

Amandla...

Cc: Nguruvi3
 
Huyu babu ni mhalifu tu! Anachokifanya ni kutumia udhaifu wa kundi fulani kutofikiri vizuri kuleta chuki za kidini.
Anatakiwa kulaaniwa na kufungwa kama mhalifu tu
Umeifufua Id hii ,naikumbuka mr Azarel
 
Tunamuelewa sana Mohammed. Ndio maana tunasema hatuna shida na yeye kuandika historia ya ndugu na jirani zake wa Gerezani. Tunasema anastahili pongezi na shukrani zetu kwa hilo.

Tatizo tulilo nae ni yeye kujipa hati miliki ya historia yetu na kutaka kuiandika upya kwa misingi ya udini na ukabila ambao wengi wa wazee wa Gerezani hawakuwa nayo. Hawa walijua nguvu zao na mapungufu yao ndio maana waliwakubali wagalatia wasomi na wenye vipaji kama Vedasto Kyaruzi na Julius Nyerere. Mimi sidhani kama babu yake Salum Abdallah alimuangalia Christopher Kasanga au Mchauru kwa jicho la udini. La hasha, aliwaona ni vijana ambao usomi wao umewaweka katika nafasi katika jamii yake. Anapofanya hivyo ndio anatutia hofu kuwa nia yake ni kupandikiza chuki katika jamii yetu ambayo haikuweko.

Jambo hilo ni hatari sana kwa sababu tofauti na hapo zamani vizazi vya sasa vinaweza kuishi bila kushirikiana kwa karibu na watu wa dini tofauti. Watu wanaweza kupata elimu yao kuanzia chekechekea hadi chuo kikuu katika shule zenye mlengo wa dini zao ( wagalatia wana zao na waislamu wana zao). Ule ushirikiano uliojengwa baada ya elimu kutaifishwa ili tusome kwa pamoja unazidi kupotea. Ndio maana ni muhimu kuwazukataza wakina Mohammed wanapochezea kiberiti sheli.

Amandla...

Cc: Nguruvi3
Na mbona mnakuja Na mask ? mnaogopa Corona?, hapa jf haipo. Kama hamwogopi ukweli mnamwogopa nani?
 
Kaka Mohamed Said kijana wako Fundi Mchundo anaandika vyema sana, mbona humjibu? Mimi napendekeza mujibu wewe tupate radha
Atajibu kitu gani hapo? Kuwa Rev. Sivalon alikuwa na ajenda ya siri ya kuharibia Kanisa Katoliki kwa kuweka wazi uovu wake?
Kuna mjadala mmoja wa suala kama hili ambapo kuna mtu aliye jitambulisha kama muislamu alieleza kisa kilichotokea wakati mihadhara ya waislamu ilipamba moto. Alisema kuna watu walifunga kambi nje ya hospitali iliyokuwa ikiendeshwa na watawa na walishina usiku kucha wakitangaza kwa sauti kubwa "Yesu sio Mungu" na maneno mengine ya kejeli kwa wagalatia. Walisema kuwa wanawajua sana hao watawa na kuwa wao ni mahawala wa mapadri ambao wanashinda wakilewa nao na kufanya vitendo vya aibu. Asubuhi, dispensari ilipofunguliwa, masista wakawa wagonjwa kwa kulingana na majina yao. Wakina Asha, Abdallah, Mudi na Sikuzani wakawekwa upande mmoja na wakina John, Maria na Joyce upande mwingine. Wakina Sikuzani wakaambiwa waende wakapate huduma maana hawawezi kuhudumiwa na mahawala wa mapdri. Kuona hivyo wenye mtaa wakawafukuza waliokuwa wanaendesha mhadhara na kuwaambia wanawaharibia. Kesho yake wakina Mudi wakaendelea kuhudumiwa kama awali na jamii ikarudi katika hali yao ya kawaida.

Mwingine alisimulia jinsi wazee wake walivyokataa kuwapa kiwanja wagalatia kujenga kanisa, shule, kituo cha afya n.k. kwa sababu ya hofu ya kulishwa nguruwe. Wagalatia wakaenda kwenye kijiji kingine ambao ingawa nao wengi walikuwa waislamu waliwapa eneo. Alisema vijiji hivyo mpaka wakati ule vilikuwa na tofauti kubwa ya maendeleo.
Sisi tumeishi katika jamii ambayo mgalatia akitaka kula kuku anamuita jirani yake Athumani amchinjie. Na Athumani wakati wa mwezi wa Ramadhani anamkaribisha jirani yake Robati afuturu nae. Sio sehemu nyingi duniani zinazoishi hivi. Tukipoteza upendo huu na kuanza kuangaliana kwa macho ya chuki za kidini, hatutaurudisha kamwe. Mwalimu Nyerere alitambua hilo ndio maana alipinga ubaguzi wa aina yeyote. Kwa hilo anastahili shukrani zetu za dhati na sio kebehi na kupakwa mafuta kwa mgongo wa chupa kama wengine wanavyofanya.

Amandla...

Cc: Nguruvi3
 
Hapo

Je ni kweli hakuna ubaguzi wa wakristo kwa waislam? Ile mizani yako ikae sawa na uwe miadilifu? Maana umemkana padre John S sijajua lililomo nafsini mwako, lakini umekuja kueleza makosa ya "Waislamu" sijajua nawe unapita njia ileile ambayo unamkataza Mohamed Said asipite? Yaani unawaandika kina Vedasto kyaruzi na Kasanga Tumbo kwa wino wa dhahabu kisha unamkataza kwa mtutu Moh asieleze "untold Muslims struggles" kuelekea uhuru? Vipi utawashawishi watu kwamba humo humo unamokataza wengine wasiwemo?

Shaykh Hassan bin Ameir unamvisha medani gani? Baada ya kutambua nafasi yake kama kiongozi wa kidini kipindi hicho na mkono mwingine ni mpigania uhuru? Au utamficha na kumvisha koti la udini kama alivyovishwa Suleiman Takdir na Mwl J K? Hebu kuwa wazi Amandla na uondoshe hutu tudoa tudogo, wewe ni muelewa na unakitu kichwani
 
Mimi sijamkana Padri Sivalon. Ndio kuna wagalatia waliokuwa na bado wanawabagua waislamu kama vile bila shaka walikuwepo na bado waislamu ambao wanawabagua
wagalatia. Ninachopinga ni kusema kuna mfumo mahsusi umewekwa ili kuwabagua waislamu. Ingekuwa hivyo, Nyerere asingeruhusiwa kutaifisha shule na hospitali za makanisa. Ingekuwa hivyo tusingekuwa na Chief Minister aliyeitwa Rashidi na marais wenye majina ya Ali, Jakaya na Samia. Ubaguzi uliokuweko ni wa watu binafsi na sio wa kimfumo.

Amandla...
Cc. Nguruvi3
 
Kaka Mohamed Said kijana wako Fundi Mchundo anaandika vyema sana, mbona humjibu? Mimi napendekeza mujibu wewe tupate radha
Makala...
Nimemnyamazia kwa kuwa nimeona hii si mada yetu iliyopo mezani.
Kwa hakika pia nilishahitimisha na wao.

Nadhani umeona pia hata katika hii mada yetu nawakwepa hawa jamaa zetu ila nakuja kwenu kutoa darsa kwenu nyie na kwa wasomaji wengine.

Bahati mbaya wenzangu hawajakubali kuniachia wananifuata huku vilevile.

Kwangu naona hii ni bughdha kwani kama nisemavyo siku zote mimi si mtu wa mabishano mimi hupenda kusomesha.

Kusomesha faida yake unawafunza watu yale ambayo hawakupata kuyajua.
Wengi hapa hamkupata kumjua Abdul Sykes si yeye wala wadogo zake na baba yao.

Leo hawa wote mnawafahamu na nini walifanya katika siasa za Tanganyika kuanzia mwaka wa 1929 hadi uhuru kupatika mwaka wa 1961.

Kubwa ni kuwa si lazima niaminike mtu ana uhuru wa kubakia na historia rasmi.

1641122654499.png

Kushoto waliokaa Kleist Sykes na kulia ni Abbas Sykes
Nyua kulia ni Abdul Sykes katika unifom ya KAR na Ally Sykes.

Picha hii ilipigwa mwaka wa 1942 Abdul aliporudi Dar es Salaam
kutoka Lower Kabete alipokwenda kufanya mafunzo ya jeshi alikuja
kumuaga baba yake kabla ya kwenda vitani Burma.
 
Mimi sijamkana Padri Sivalon. Ndio kuna wagalatia waliokuwa na bado wanawabagua waislamu kama vile bila shaka walikuwepo na bado waislamu ambao wanawabagua
wagalatia. Ninachopinga ni kusema kuna mfumo mahsusi umewekwa ili kuwabagua waislamu. Ingekuwa hivyo, Nyerere asingeruhusiwa kutaifisha shule na hospitali za makanisa. Ingekuwa hivyo tusingekuwa na Chief Minister aliyeitwa Rashidi na marais wenye majina ya Ali, Jakaya na Samia. Ubaguzi uliokuweko ni wa watu binafsi na sio wa kimfumo.

Amandla...
Cc. Nguruvi3
Unakijua kisa cha shaykh Hassan bin Ameir baada ya Uhuru? Kaka Mohamed Said naomba utupitishe Kitabuni kunako miaka ya 1960 baada ya kupatikana uhuru nini kilitukia?
 
Unakijua kisa cha shaykh Hassan bin Ameir baada ya Uhuru? Kaka Mohamed Said naomba utupitishe Kitabuni kunako miaka ya 1960 baada ya kupatikana uhuru nini kilitukia?
Makala...
Unatonesha kidonda.

Kila shughuli mji huu wa Dar es Salaam wakiwarehemu masheikh jina la kwanza ni la Sheikh Hassan bin Ameir.

Saigon Club kila mwaka inafanywa khitma na jina la kwanza huwa la Mufti Sheikh Hassan bin Ameir.

Mwaka wa 2004 nilialikwa Zanzibar University kutoa mada kuhusu Sheikh Hassan bin Ameir.

Nilifungua mhadhara wangu kwa mukadama huo hapo chini baada ya Bismillah Rahman Rahim:

''The name of Mufti Sheikh Hassan bin Ameir like the names of many other Muslim patriots is omitted from the political history of Tanzania.[1]

There is no place in the official history in which his name is mentioned even in passing.

Hassan bin Ameir’s name began to feature in early 1980’s when Muslims privately began to research and document their role in the independence struggle as a reflection to their marginalisation in distribution of power.

As a result of this Sheikh Hassan bin Ameir’s name soon came to the fore and was associated not only with politics and equal power sharing between Muslims and Christians but also with efforts by Muslims to build educational institutions.

Having accomplished his role as a patriot and a symbol of mass mobilisation under TANU during the struggle he resigned from politics soon after Tanganyika achieved its independence in 1961 and through his organisation Dawa’t Islamiyya concentrated on serving Islam and Muslims.

This shift was to create an unprecedented confrontation between himself and the then President of Tanzania Julius Nyerere.

On the order of the President, Sheikh Hassan bin Ameir was arrested for ‘subversion’ and deported to Zanzibar and the EAWMS of which Sheikh Hassan bin Ameir was among its leaders declared an ‘illegal’ society.

In its place BAKWATA was formed to replace the EAMWS.

The reverberations of this clash between these two giants of titanic magnitude are being felt as we speak today likewise the vacuum left by the EAMWS has not been filled.

Consequently the political climate and relations between Muslims and the government was not to be the same again.

In the same breath relations between Muslims and BAKWATA to say the least has been lukewarm.

Muslims perceive BAKWATA as a puppet organisation and just to mention the name leaves a bad taste in the mouth.

To refer to a Muslim as a BAKWATA Muslim is like calling a Christian a disciple of Judas Iscariot who betrayed Jesus for thirty pieces of silver.

As to Nyerere, history is yet to judge him.

But one can not be knowledgeable to all this in the absence of the political history of Sheikh Hassan bin Ameir.

There are however, contrary voices disputing Sheikh Hassan bin Ameir’s political carrier.

These voices are originating from some of his students questioning his role in politics.

Students of Sheikh Hassan bin Ameir prefer to remember him as a brilliant ‘ulamaa’, an outstanding translator of the Qur’an[2] and not as a politician.

Sheikh Hassan bin Ameir’s ‘silsila’ goes back to Sayyidna A’li b. Abu T’alib and Rasuli Lahi (SAW).

Understandingly his students do not want to taint this with what they perceive as ‘trifles’.

But reality and history takes exception to this.

This stand if allowed to flourish would wipe out and obscure an important period in Sheikh Hassan bin Ameir’s life and hence erase a significant chapter in the nation’s history.

Along with it, the country will also lose his thoughts, teachings and aspirations, which made him what he is in the history of Tanganyika.

We will also not be able to uncover the forces behind marginalisation of Muslims.

This information is vital to Muslims and has to be accessible to all and sundry.

The truth however still remains that Sheikh Hassan bin Ameir was in deed a politician who played a leading role in Tanganyika’s struggle for independence.[3]

Muslims or his obedient students should be the last persons to question Sheikh Hassan bin Ameir’s political carrier.''

Mhadhara mzima huo hapo chini:

1641125959136.png
 
Back
Top Bottom