Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
Jagna,Ni kweli huwezi kumlinganisha Nyerere Na Abdul ,
Nyerere alikuwa kibaraka wa Waingereza Na kanisa Katoliki Hakuna siri hapo
Unaandika umeghadhibika na mimi naelewa hamaki zako.
Mwalimu wangu aliyenisomesha ilm ya mnakasha yaani majadiliano alikuwa akisema, ''Chunga ulimi wako lisikuponyoke neno ukajakujuta kwa nini nimelisema.''
Akawa anatufunza anasema,''Neno likitoka huwezi kulirudisha ndani kwa hiyo chukueni sana tahadhari.''
Mnakasha huu hadi sasa una watu 7732 ''and counting,'' na hii si idadi ndogo.
Tusiwapoteze.
Umewavutia watu mnakasha huu bila shaka kwa haya wanayosoma.
Juzi nimeeleza hapa jamaa walionifuata na kuniambia tufanye mjadala wa wazi kwenye ukumbi na urushwe usikike mubashara kwenye TV na FM Station.
Wameniambia, ''Mohamed sisi hatuwezi kuona hawa watu wanakutukana na wanatukana wazee wetu waliompokea Nyerere na wakapigania uhuru wa nchi hii pamoja na yeye sisi tukawa pembeni tunakutazama tu.''
Sikupenda kuingia katika haya maneno waliyonambia.
Lakini lipo jambo kubwa hapa.
Lakini moja ya mambo waliyoniambia ni kuwa siwajibu inavyotakikana.
Wao wanataka nirejesho moto kwa moto.
Kibri kwa kibri, kebehi kwa kebehi,kejeli kwa kejeli.
Jibu langu kwao lilikuwa kuwa mimi nafahamika katika duru za uandishi na nimejenga heshima yangu siwezi kufanya hivyo.
Nikawapa mfano nikawaambia hawa wenzangu ni mfano wa askari wa msituni hawana sura wala hawavai unifomu ya jeshi lolote hakuna anaewajua wanaweza wakasema lolote linalowajia.
Hawana sheria yoyote ya uungwana inayowafunga.
Hawa ni ''guerilla,'' askari wanaopigana ndani ya msitu.
Nikahitimisha kwa kuwaeleza kuwa sidhani kama wanaweza wakajitokeza sura zao zionekane tufanya mjadala.
Jagna,
Wewe unarejesha moto kwa moto.
Jambo lolote ukilitia upole linapendeza na hii ni kauli ya Mtume SAW.
Tia upole katika majibu yako yatapendeza.
Mimi ninayo majibu naweza nikayatoa lakini naogopa kuponyokwa na neno nisije nikajuta.
Kitabu cha Abdul Sykes kipo kwa Kiingereza na kwa Kiswahili huu sasa mwaka wa 23.
Sasa tunakwenda toleo la 5.
Hawa wasomaji ndiyo wakunishuhudia mimi.
Kitabu hiki kimefunika kitabu cha Kimambo na Temu (1969) na kitabu cha Chuo Cha CCM Kivukoni (1981).
Toleo moja na kitabu kimekufa.
Sina sababu ya kugombana na mtu yeyote kuhusu historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika lisinitoke neno nikajuta kwani majuto ni mjukuu.
Sikuandika maisha ya Abdulwahid Kleist Sykes ili kumdogosha Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Laiti nia yangu ingekuwa ni kumdhalilisha Julius Nyerere ningekiua kitabu changu kwani hakuna asiyejua ukubwa wa Mwalimu na mchango wake katika kupigania uhuru wa Tanganyika.
Lakini mimi naujua pia mchango wa wazee wangu kwa Mwalimu na kwa harakati ya kupigania uhuru hadi ukapatikana.
Historia hii ilifutwa na mimi nimeiandika leo inasomwa.
Yapo niliyoyaeleza hapa na yapo mengi sikuona haja hata ya kuyaeleza katika kitabu.
Hayamo ingawa ni mambo muhimu na ya kupendeza.
Nilifanya hivyo kwa makusudi kabisa kwa nia ya kuweka staha kwani wazalendo hawa wenyewe kwa wenyewe walifanyiana hisani nyingi.
Nilichelea wasije watu wakageuza kauli zangu na hapa haya yamefanywa na wakiyarudiarudia wakiamini kuwa yatashusha heshima yangu na ya wazee wangu.
Jagna,
Haya ndiyo niliyotaka kukueleza.
Fanya mnakasha lakini ondoa ghadhabu.
Aliniambia msemaji mmoja Profesa wa African History Northwestern University baada ya kusikiliza mhadhara wangu kuwa ilikuwa baada ya kusoma kitabu cha Abdul Sykes ndipo alipofahamu kuwa historia aliyakuwa akisomesha ilikuwa si kamili.
Northwestern Universiity ndiyo wanaongoza dunia nzima katika historia ya Afrika.
Chuo hiki ukija na kitabu cheny elimu mpya lazima watakualika chuoni kwao ukazungumze.