1963: Rais wa Jamhuri ya Tanganyika, Julius Nyerere akiweka pini katika koti la Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Bw. U Thant

1963: Rais wa Jamhuri ya Tanganyika, Julius Nyerere akiweka pini katika koti la Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Bw. U Thant

Shwari na ndugu zangu wengine,
Niruhusini nikupeni historia ya wazalendo watatu katika siasa za vyama vya wafanyakazi mwishoni miaka ya 1940s kuelekea 1950s mjini Dar es Salaam.

Wazalendo hawa ni Erika Fiah, Kleist Sykes na mwanae Abdulwahid Kleist Sykes.

Nafanya hivi kwa kuwa Erika Fiah katajwa mara kadhaa hapa jamvini ningependa nikuhadithieni historia yake ili mpate kumfahamu vizuri.

Kwa kuwa ni historia ndefu nitatanguliza link ambayo ni kisa kizima na baadae In Shaa Allah nitaiweka historia hii kwa ufupi:


''...tunakutana na Abdulwahid Sykes na African Association na hii ikiwa mwaka wa 1947 miaka miwili imepita baada ya yeye na mdogo wake Ally kurudi kutoka Burma walipokwenda kupigana katika Vita Kuu ya Pili.

Dhiki ilitawala mji mzima hasa kwa kuwa ndiyo kwanza Tanganyika ilikuwa inatoka katika kishindo na mkiki mkiki wa vita.

Hali hii ndiyo iliyomsukuma Abdul Sykes katika siasa na ikamfanya aelewe maana ya harakati za wananchi dhidi ya utawala wa kigeni akiwa bado kijana mdogo sana.

Kidogo kidogo baba yake alianza kumkabidhi Abdul kazi za African Association na mara akawa msaidizi wa baba yake katika siasa za Dar es Salaam.

Ilikuwa katika kutimiza haya ndipo Abdulwahid akajikuta anahusika na ule mgogoro wa makuli ulioibuka bandarini Dar es Salaam ambao ulikuwa ukichemka pole pole chini kwa chini kwa muda mrefu tangu kumalizika kwa Vita Kuu ya Pili.

Hatimaye, Abdul Sykes alihusika na harakati za siri za wafanyakazi bandarini ambao, wakiwa wamechoshwa na sheria za kazi za ukandamizaji na wakiwa wamechoka kunyonywa na makampuni ya meli, walikuwa wanapanga kuitisha mgomo.

Kleist mwenyewe alikuwa hakuwa mbali na siasa za wafanyakazi yeye akiwa mwajiriwa wa Tanganyika Railways alijaribu kuwakusanya wafanyakazi wa Railway kuasisi chama chao.

Kamati ndogo ya siri iliundwa na Abdulwahid akatiwa ndani ya kamati hiyo ili kuongoza mgomo uliokusudiwa.

Kazi ya kamati hiyo ilikuwa kupanga na kuratibu mikakati ya kuitisha mgomo ambao ungelisaidia katika kuondoa ile dhulma iliyokuwepo. Makuli waliitisha mkutano pembeni kidogo mwa mji, mahali palipokuwa pakijulikana kama ‘’Shamba kwa Mohamed Abeid,’’ katika bonde la Msimbazi.

Mohamed Abeid mwenye shamba hili alikuwa Muarabu mwenye asili ya Yemen na shamba lake lilianzia Msimbazi kuelekea Mchikichini.

Sehemu hii ilichaguliwa makhususi mbali na macho ya watu ili ipatikane faragha waweze kufanya shughuli yao waliyokusudia kwa utulivu.

Makuli walikula kiapo na kusoma Ahlal Badr ilii kujikinga na unafiki, usaliti pamoja na shari ya vizabizabina wangeokataa kugoma.

Siri ya mgomo huu ilihifadhika hakuna nje yao aliyejua nini kitatokea.

Mapema asubuhi moja kile kilichoanza kama mipango ya siri dhidi ya makampuni ya Wazungu bandarini, kililipuka na kuwa mapambano ya dhahiri.

Watu katika mitaa jirani ya Mtaa wa Aggrey, alipoishi Abdul na baba yake walikuwa hawajatoka vitandani mwao alifajiri moja wakasikia vishindo na makelele vimetanda mtaani.

Makuli, baadhi yao wakiwa vidari wazi, walikuwa wameizingira nyumba ya Kleist, wakipiga makelele wakimtaka Abdulwahid atoke nje.

Makuli wale walipiga kwata njia nzima kutoka bandarini huku wakitoa maneno ya kupinga ukoloni na wakiimba kupandisha morali zao.

Tukio hili halikuwa na kifani. Ilikuwa ni mara ya kwanza nchini Tanganyika kwa wananchi kushuhudia katika mitaa ya Dar es Salaam uasi wa dhahiri kama huo dhidi ya serikali ya kikoloni.

Abdul Sykes wakati ule kijana mdogo kabisa wa umri wa miaka 23, akichungulia kupitia dirisha la chumba chake alichokuwa amelala, alishangazwa kuona umati mkubwa wa watu nje ya nyumba yao.

Aliweza kuwatambua baadhi ya wenzake katika kamati ile ya siri iliyokuwa inapanga mipango ya mgomo.

Alipotoka nje kuonana nao makuli wenye hasira walimfahamisha kuwa mgomo ulikuwa umeanza na wasingerudi kazini hadi madai yao yote yamekubaliwa.

Mgomo huu ulienea kama moto wa makumbi ulikumba nchi nzima kwa kasi ya ajabu.

Ilikuwa kama vile wafanyakazi wa nchi nzima wametaarifiana.

Wafanyakazi wa Tanganyika Railways huko Tabora wakiongozwa na babu yangu Salum Abdallah waliingia kwenye mgomo tarehe 11 Septemba, siku tano baada ya mgomo wa makuli kuanza Dar es Salam.

Mgomo ule ulisababisha serikali ya kikoloni kupitisha sheria ambayo iliruhusu kuundwa na hatimae kusajiliwa kwa Dar es Salaam Dockworkers’ Union.

View attachment 2068228
Abdul Sykes katika unifom ya KAR
Burma Infantry

Itaendelea...
Ndugu zangu,
Miaka zaidi ya 30 sasa imepita toka niliposoma Nyaraka za Sykes.

Hivi sasa katika mambo yanayonisikitisha ni kwa Sykes kuzirejesha hizi nyaraka kwenye ''safe,'' kuzifungia na kutoziweka wazi kwa watafiti kuzisoma.

Watafiti wangepewa fursa ya kuzipitia wangeona kuwa kila mzalendo pamoja na wakoloni Waingereza waliohusika katika siasa za kipindi kile wamo ndani ya nyaraka hizi.

MJ Molohan.
Nimemsoma ndani ya Nyaraka za Sykes.

MJ Molohan Mwingereza huyu alikuwa Kamishina wa Kazi nimemkuta katika Nyaraka za Sykes akipambana na Kleist Sykes miaka ya 1930s hadi 1950 anashughulika na watoto wa Kleist katika siasa za wafanyakazi Waafrika.

Kwanza na Abdul katika Dockworkers' Union kisha na Ally katika TAGSA.

Baada ya mgomo ule wa makuli na sheria ya kuundwa kwa vyama vya wafanyakazi kupita Molohan alianza mchakato wa kutafuta watu ambao wangeweza kushika nafasi ya Katibu Mkuu wa Dockworkers’ Union.

Islam Barakat alikuwa Labour Inspector wa kwanza Mwafrika ingawa alikuwa na damu ya Kiarabu na Kiafrika.

Molohan alimwomba Barakati amsaidie kutafuta mtu wa kusika nafasi ya Secretary General wa Dockworkers' Union.

Barakat alipeleka majina mawili.
Jina la Abdul Sykes na la Erika Fiah.

Abdul Sykes, kijana wa mjini miaka 24, mtoto wa mfanyabiashara na mwanasiasa maarufu Dar es Salaam.

Jina lingine lilikuwa la Erika Fiah miaka 53, mwanasiasa mpevu na mtu wa makamo.

Erika Fiah alikuja Tanganyika pamoja na ma crejeshi ya Waingereza kutoka Uganda wakati wa Vita Kuu vya Kwanza.

Baada ya vita alilowea Tanganyika na kuishi Mission Quarters ambako alihariri gazeti lake, Kwetu.

Fiah alikuwa Mwafrika wa kwanza kuanzisha na kumiliki gazeti lake mwenyewe katika Tanganyika.

Mtu wa pili alikuwa Ramadhani Mashado Plantan mtoto wa Chief Mohosh Shangaan kutoka Mozambique alikuyekuwa Tanganyika na Hermann von Wissman akiongoza jeshi la askari mamluki wa Kizulu.

Tanganyika akajulikana kama Affande Plantan mkuu wa Germany Constabulary.

Watoto wake kama walivyokuja kuwa watoto wa Kleist wameacha historia kubwa katika Tanganyika.

Fiah kama wanasiasa wote wa zama zake, alikuwa Mwafrika kwanza na uzalendo ukafuatia.

Vilevile alikuwa mmoja wa wafuasi wa mwanzo wa Karl Marx nchini Tanganyika na gazeti lake Kwetu, lilikuwa maarufu kwa sababu ya ukali na vijembe vyake dhidi ya ukoloni.

Fiah alikuwa mwanasiasa aliyekuwa amepea sana katika wakati wake.

Katika miaka ya 1930 aliwahi kujaribu kuhamasisha tabaka la wafanyakazi na wakulima kuwaunganisha dhidi ya ukoloni, lakini alishindwa kwa kuwa wananchi walikuwa bado hawajaamka kiasi cha kutosha kuweza kuitikia mwito wa kuuhamasisha umma kama tabaka.

Kwa wakati ule Fiah alikuwa na upeo mkubwa wa siasa na alikuwa na uwezo wa kuhamasisha zaidi kuliko kijana mdogo Abdul Sykes.

Vilevile Fiah alikuwa mtu mzima na uzee ni dawa.

Haiwezekani kumlinganisha Fiah na Abdul Sykes aliyekuwa kijana mdogo ambaye Fiah angeweza kuwa mtoto wake.

Kati ya kipindi kile kati ya vita vya kwanza na vya pili ya dunia, Fiah alitumia kalamu yake kudhihirisha bila ya woga matatizo yanayowakabili Waafrika.

Lakini Fiah hakuwa tu adui wa serikali alikuwa pia adui wa Kleist na Waafrika wengine mashuhuri, wengi wa hao wakiwa katika utumishi wa serikali.

Huko nyuma katika mwaka wa 1933 kulikuwako na mgongano baina ya Kleist na Fiah kuhusu uongozi wa African Association.

Kupitia gazeti lake Fiah alimshambulia Kleist akimshutumu kwa kile Fiah alichokiona kuwa tabia yake isiyokuwa ya kizalendo iliyotokana na asili yake ya Kizulu.

Fiah alidai kuwa mambo yanapokuwa mazuri kwa Watanganyika Kleist atajinasibisha na Utanganyika, lakini upepo unapobadilika na kuvuma upande wa Wazulu, mara Kleist anakuwa Mzulu.

Ili kuepuka mgongano Kleist alijiuzulu kama katibu wa African Association na Fiah alichaguliwa kushika nafasi hiyo.

Kalamu ya Fiah ilikuwa haina muhali. Katika rambirambi alizotoa za kijeuri na za dharau juu ya kifo cha Martin Kayamba, Fiah aliomboleza kwa kusema kwamba Waafrika hawakunufaika kwa elimu ya Kayamba wala kwa wadhifa wake kama karani wa kaimu Katibu Mkuu katika serikali ya Waingereza.

Fiah alipingana na Wazungu vilevile.

Mwaka wa 1940 aliandika tahariri iliyowalenga Wazungu waliokuwa wakimpinga kwa kueleza wazi wazi fikra zake na kwa kuchapisha gazetini makala juu ya haki za Waafrika.

Fiah alikuwa mwanaume kweli kweli hata ingawa wakati wa zile harakati za bandarini makuli wakiwa wanakwenda nyumbani kwa Kleist kumfuata mwanae Abdul kwa maandamano na hivyo kumpa hadhi ya uongozi wa harakati zile, kwa hakika Abdul Sykes hakuwa anafikia hadhi wala kiwango cha Fiah ktika siasa za nyakati zile.

Kumfananisha Abdulwahid na Fiah ilikuwa sawa na kufananisha mlima na kichuguu.

Mara kwa mara mawazo ya Erika Fiah kama ilivyotegemewa hayakupokelewa vizuri na serikali katika ya hao waliokuwa serikalini akiwa MJ Molohan.

Ndugu zangu ikiwa kama hamkumjua Fiah huyu ndiye Erika Fiah.

Erika Fiah, Kleist Sykes, Mzee bin Sudi, babu yangu Salum Abdallah kwa kuwataja wachache hawa wote wakifahamika kama ''Wakuja,'' na wenyeji wakiwasema kuwa wanapenda sana kujitia kimbelembele.

Ile ''Wakuja,'' wakiwa na maana kuwa hawana asili ya Tanganyika.

In Shaa Allah darsa litaendelea tutatazama mapambano baina ya Abdul Sykes na Erika Fiah.

1641545535150.png

Erika Fiah
 
Na uso umevaa kikoi unarusha madongo [emoji1][emoji1][emoji1][emoji1]
Janina,
Nakukumbusha tena kuwa jambo lolote ukilitia upole litapendeza.

Ingependeza kama ungeshauri pawepo na subra ijulikane mbona barza imekuwa kimya?

Sasa mtu angesoma mabezo na vicheko vya mbezaji kisha akakusoma wewe unashauri utulivu na kutaka kujua kulikoni angeona tofauti iliyoko baina yenu.

Mtego usingeteguka
Ila kwa zake haraka

Panya kuchungulia kataka
Hapo ndipo mtego ulipofyatuka

Kutoka hawezi macho yamemtoka
Panya masikini kiranga kimemtoka

Mama yake amuuliza kipi kilichokuponza
Ilhali subira nilikufunza?

Nani huyu tena?
Muyaka?
 
Sema sera ya vijiji vya ujamaa ingeundwa vizuri tungekuwa mbali.

Nahisi watu wa mikoa hii ya arusha Kilimanjaro hasa ndo waliingilia kupinga ujamaa.

Vile walijua vihamba vyao vitagawiwa.

Kufanya kazi pamoja kwa manufaa yenu wote ni nzuri.

Ni kama wasomi waliokuwepo hawakumsaidia mwalimu kuunda hivi vitu.

Mngezaliwa mjikute hivyo ni kuwa yangekuwa ndo maisha yetu.

Vita kweli vilipukuta uchumi wetu.

Akiba yote ikaishia vitani.

Ni kama tokea pale nchi haijakaa sawa tena.

Anyway nilimpenda sana Mwalimu Nyerere.
"inge" ndio haikuundwa vizuri. Uwezo ndipo ulipoishia, hata baada ya kuelezwa kuwa unaipeleka nchi pabaya, hakuelewa. Ndipo alipopata jina "haambiliki" akakasirika.
 
Kwenye kupigania Uhuru hutosikia majina ya machifu...hawa walikuwa beneti na wakoloni
Ajabu Nyerere alivyopewa nchi Tu..
Akaleta hawa machifu kwenye serikali..


Mang'enya
Fundikira na wengineo

Aliwaleta for strategic reasons sawa na wale Viongozi wa cooperatives kama Kasambala, Bomani, Kahama etc. Machief na hawa viongozi wa ushirika walikuwa na ushawishi na wafuasi wengi seheme walizotoka.

In hindsite, hivi vinavyoitwa VIKOBA sio modified form of COLLECTIVES?
 
Nilijua kimbilio lako ni mdini mwenzako Mohammed Said. Utamuamini vipi mtu anayedai kuwa waarabu hawakuua waafrika wala kuwatesa!

Ili upate balance, nakushauri usome kitabu cha Ali Sultan Issa, kinachoitwa Walk on Two Legs, aliyezaliwa Wete, Pemba mwaka 1932, mwanachama wa ZNP ambae alihamia chama cha Umma. Anazungumzia waafrika waliojiita washirazi ili kujitofautisha na wale walioletwa kama watumwa au wafanyakazi. Anazungumzia watumwa walioletwa kutoka Congo. Anazungumzia mjomba wake aliyerithi mtumwa kutoka kwa babu yake. Aliwajua watu waliokuwa watumwa. Anazungumzia jinsi waarabu wa Pemba walivyozaa na waafrika. Yeye mwenyewe upande wa mama yake asili yao ilikuwa Yemen, upande wa baba Oman. Hata hivyo mama wa bibi yake mzaa mama, ( aliitwa Bibi Ruzuna Binti Tamim, aliyewahi kuwa mke wa Sultan Ali bin Hamoud) alikuwa mzaramo na bibi huyo huyo alikuwa na damu ya wanandi kutoka Kenya. Huyu bwana alikuwa rafiki mkubwa wa Babu na anaelezea kuhusu ushirikiano kati ya chama cha Umma na ASP kuandaa mapinduzi ya Zanzibar. Anaelezea jinsi wao wakommunisti waliwaachia shughuli nzima ASP Youth League kwa sababu wao hawakuwa wengi na serikali iliwahofia zaidi UMMA kuliko ASP. Anaelezea jinsi Yusuf Himidi, Said wa Shoto, Abdullah Said Natepe, Khamis Darweshi, Ramadhan Haji, Pili Khamis, Seif Bakari na Saidi Iddi walivyoongoza uvamizi wa armoury iliyokuwa Ziwani. Hawa walivamia pia Police Barracks zilizokuwa Mtoni. Ukitaka kujua zaidi kuhusu Mapinduzi soma dissertation ya Ph. D ya Ann Lee Grimstad aliyoitetea mwaka 2018 katika Chuo Kikuu cha Florida. Kama nilivyokuambia hapo awali, udini unakupa ujinga. Usiwasikilize wakina Mohammed Said peke yao. Fanya utafiti wako mwenyewe ndio utajua ukweli.

Kwangu mimi sina zaidi ya kuchangia kuliko haya. Una uhuru wa kuamini utakacho.

Amandla....
Sasa hiyo Shirazi iko Afrika? Eti "Waafrika wanojiita Washirazi", labda ungeandika Waafrika waliochanganya damu na Washirazi (Afro Shirazi, kina Thabit Kombo) Kama vile tunavyowafahamu "Afro Americans".


Nakuona una jitahidi kutaka kuutetea ukweli usioujuwa, ingawa unausoma na kuusikia ukweli kwa wanaoujuwa na wenye ushahidi wa tafiti na wenye mashiko, lakini, bila aibu moyo wako uliojaa chuki za kijinga hautaki kuamini.

Hutoweza kuutetea ukweli kwa uongo wa chuki zako za kujazwa ujinga. Hauna mashiko.
 
Mabepari walipata faida kubwa enzi za utumwa na tangu pale mshahara wa kima cha chini sikuzote ni wa kumtosha mtu wa hali ya chini kununua chakula tu na kesho aende kazini.

Nchi zilizoendelea wasomi na wanaharakati ndiyo wana lobby kuweka hali za watu wa kima cha chini katika mazingira bora kwani vifo vyao kwa wingi vinaathiri hata uchumi wa nchi.

Ujamaa wa China angalau waliweza kujenga nyumba kwa wanavijiji, ujamaa wetu hatukujiandaa vyema kuweka mazingira ya vijiji yawe yakukalika.
Hata China haukufanikiwa ujamaa na ndio maana mpaka leo wanauana sana. Dont judge the book by its cover. Wachina kila walipopata nafasi ya kuutoroka ujamaa walitoroka, mpaka sasa hivi wakipata fursa za kuishi nje ya kwao hawana hamu ya kurudi. Katazame walivojazana US, Canada na Europe. Sasa wameanza kujazana Afrika na Asia nje ya China. Jiulize kama huko ni neema, wakikimbia nini?
 
Sidhani kama anaweza hata kusema kama kulikuwa na utumwa Zanzibar. Kwake yeye kila kitu anakiangalia kwa darubini la dini.
Tulijadiliana nae sana kuhusu imani yake kuwa ni waislamu wa Gerezani peke yake ndio wanaostahili kuenziwa kama waasisi wa madai ya Uhuru. Ukimsikiliza utadhani ni wakina Sykes peke yao ndio waliominywa na Nyerere ( kitu ambacho si kweli kwa sababu kwa muda mrefu ni wakina Sykes, Munanka na wachache wengine ndio walioruhusiwa kuwa mabepari wakubwa Tanzania) akisahau wakina Oscar Kambona, Christopher Kassanga Tumbo na wengine.

Amandla...
Utumwa si Zanzibar tu, hata bara ulikuwepo na bado upo. Au huelewi kuwa mpaka leo utumwa upo?
 
JokaKuu kilimo cha karanga kilifanikiwa sana Dodoma, baada ya WWII Uingereza ilikumbwa na recession na makoloni yaliwajibika kuikomboa nchi mama. Hapa madini yetu yalichotwa sana na kwa sana.

Karanga ilileta mafanikio makubwa na ziliokwa na kufingwa kwenye foil na lable ya groundnuts from British East Africa. Ziliuzwa sana hasa katika makoloni ya Uingereza kuanzia Zambia, Malawi mpaka Australia na Canada.
Madini mpaka leo "yanachotwa", nini kinazuwia? Mtayala wenyewe?

Kuhusu kilimo kabla ya Uhuru, ukiisoma vizuri historia, wakati tunapata Uhuru Tanganyika ilikuwa namba 1 katika Afrika kuuza mazao nje. Jiulize ilikuwaje miaka 7 tu baadae tukawa omba omba namba moja duniani?
 
Sijui ninachokuuliza ni rahisi, ikiwa '' Nyerere anatuhumiwa kuleta mapinduzi'' je, mapinduzi ya Zanzibar ni HALALI au ni HARAMU?
Ninaweza kukuuliza maswali juu ya kiwango chako cha elimu, please nifahamishe .

Huu mjadala ni mzito na watu waliopo ni wazito, Mohamed Said anajua.

Mi nadhani ukamalizie homework ya sayansi kimu wakati ukifika urejee hapa.
Kama unadhani bado una mtima, hebu tueleze Mapinduzi ya Zanzibar ni Halali au ni Haramu?
Halali na Haramu ni subjective. Halali kwako ni haramu kwa mwengine.


Wewe uhalali wako unaupata kutoka kanisa alilokuanzishia mzungu. Mimi uhalali naupata kutoka kitabu cha Allah.

Hapo sasa.
 
Ni uamuzi wa hovyo sana. Kwa waliokulia maeneo kama Tanga ustawi wa jamii nyingi ulitegemea sana zao la Mkonge. Katika kipindi hiki dunia ikipambana na climate change, Tanzania ilikuwa na fursa ya kutumia mkonge kuziba pengo la plastic katika maeneo mengi sana, tulifeli.
Hakukuwepo na sababu zozote zile za maana za kutaifisha mashammba yale na sasa ni mapori

The country will never recover from that epic loss

Ni moja kati ya makosa makubwa sana ya Nyerere
Hilo ni moja tu ya "makosa makubwa", kama ulivyoandika. Tuainishie makosa mengine kwa mtazamo wako, pia tuainishie na Mafanikio yake ni yepi?



Hapo sasa!
 
"inge" ndio haikuundwa vizuri. Uwezo ndipo ulipoishia, hata baada ya kuelezwa kuwa unaipeleka nchi pabaya, hakuelewa. Ndipo alipopata jina "haambiliki" akakasirika.
Humpendi Mwalimu Nyerere kwa kuwa siyo dini yako.

Wewe ni mbaguzi with no shame.

Kama siyo mwalimu ukapata walau elimu ya hiyo ungekuwa flat over.
 
Humpendi Mwalimu Nyerere kwa kuwa siyo dini yako.

Wewe ni mbaguzi with no shame.

Kama siyo mwalimu ukapata walau elimu ya hiyo ungekuwa flat over.
Hayo yako na uliyesema "inge.." ni wewe. Au kabadili kauli yako.

Dini yangu wewe inakuuma nini? Au ndio unapotaka kujifichia huko, kuubadili mjadala kuufanya wa kidini?
 
Sasa hiyo Shirazi iko Afrika? Eti "Waafrika wanojiita Washirazi", labda ungeandika Waafrika waliochanganya damu na Washirazi (Afro Shirazi, kina Thabit Kombo) Kama vile tunavyowafahamu "Afro Americans".


Nakuona una jitahidi kutaka kuutetea ukweli usioujuwa, ingawa unausoma na kuusikia ukweli kwa wanaoujuwa na wenye ushahidi wa tafiti na wenye mashiko, lakini, bila aibu moyo wako uliojaa chuki za kijinga hautaki kuamini.

Hutoweza kuutetea ukweli kwa uongo wa chuki zako za kujazwa ujinga. Hauna mashiko.
Ndio maana nimesema waafrika wanaojiita washirazi. Waliochanganya damu ya kiafrika na kishirazi walijiita washirazi sio Afro Shirazi. Hata hao wanaojiita waarabu wengi wao ni waafrika waliochanganya damu ya uarabu na hawajiiti Afro Arabs. Hoja za kubuni kama hiyo ya Afro Shirazi ndio inayonifanya nikuone mpumbavu. Mpumbavu hana tiba. Ni kipaji.

Afro Shirazi Party kiliundwa tarehe 5 Februari mwaka 1957 baada ya vyama vya African Association kuungana na cha Shirazi Association. Thabit Kombo Jecha Al Shiraz alikuwa mwanachama wa Shirazi Association na mwaka 1956 alichaguliwa kuwa Katibu Mkuu wake. Siku zote alitambulika kama mshirazi na sio mafro shirazi. Chama cha Afro Shirazi hakina uhusiano na watu kuchanganya damu.

Ushahidi upi wa kuokoteza? Mimi nahoji kwa sababu huo unaouita ushahidi hauna mashiko. Ndio maana tukiwahoji mnakimbilia kudai tunawachukia.
Ujinga wangu utaondoka mkinielimisha lakini kwa vile mpaka sasa hivi hamjafanikiwa nitabaki kuwa mjinga.

Amandla...
 
Utumwa si Zanzibar tu, hata bara ulikuwepo na bado upo. Au huelewi kuwa mpaka leo utumwa
Nazungumzia Chattel Slavery ambapo mtu na uzao wake ulihesabiwa kuwa bidhaa na ulimilikiwa na binadamu mwenzake. Afrika bado upo Mauritania na Sudan. Labda uniambie Tanzania ni wapi watu wanawamiliki wenzao na uzao wao na wanawauza kama bidhaa nyingine.

Amandla...
 
Back
Top Bottom