nyakubonga
JF-Expert Member
- Apr 5, 2015
- 5,960
- 9,978
Kwa kesi ya Afrika ni tofauti na Marekani...Haihusiani....
Ngoja nikufafanulie vizuri uelewe.
Rudi mwaka 1900...mimi ni mmasai...sina serikali kama ilivyo sasa. Kiongozi wetu ni Leingwanan....wakaja watu wakanihamisha nilipokuwa naishi nikaenda sehemu nyingine kuwafanyia kazi. Nikaishi sehemu mpya kwa miaka nikazaa watoto ...nikafa.
Baadae kutokana na maendeleo ninapoishi pakajitawala na pakajipa jina. Serikali mpya ikampa kila aliyekuwa anaishi ndani ya hii sehemu mpya uraia baada ya kujipatia huru.
Swali je, nchi yangu ni ipi? Unataka wajukuu zangu warudi nilipotoka miaka 100 iliyopita?
Watumwa wa Marekani ni wamarekani wenye asili ya kiafrika. Ukimrudisha Rick Ross Afrika leo unampeleka wapi? Hajui chochote kuhusu Afrika....
Wale black american hawana makabila
Afrika bado tunaishi kikabila, tunajua Uganda hakuna wafipa...
So tukiona mfipa pale Uganda hata kama ni wa kizazi cha 5 huyo bado ni mtanzania...
Na tutaishi na wewe kwa kukuvumilia, ila siku ukileta ujanja tutakwambia Uganda sio ya wafipa, kwenu ni Rukwa, Tanzania...