2008-2025 JWTZ imezuia mapinduzi ya kijeshi ya Jeshi la Rwanda (RPF) mara 8 ndani ya Burundi

2008-2025 JWTZ imezuia mapinduzi ya kijeshi ya Jeshi la Rwanda (RPF) mara 8 ndani ya Burundi

Jw ilikuwa mji wa Sake kuzuia m23 wasifike Goma.
M23 wameiteka Sake yenyewe iliyokuwa inalindwa na tayari Goma iliyokuwa inalindwa na mataifa zaidi ya 10 iko mikononi kwa M23 na sasa wanaelekwa Bukavu kwa kuvimba. Sasa jiulize hao walinzi wa sake wamekimbilia wapi?
Majeshi ya serikali na washirika wake wamekimbia kuokoa roho zao.

Wakati M23 wakisonga mbele hakuna wa kuwazuia. Souz Afrika alitaka kushindana nao akapigigishwa hasara ya askari 13 saiv kuufyata anasubiri huruma za Kagame ili aokote Mairi zake na kukusanya vifaa vyake.
JWTZ hawapo Congo kupigana....ni walinda amani.

Ndiyo maana umeona Kagame amewalalamikia SANDF maana waliingizwa mkenge. ......Mlinda amani hajibizani na waasi hadi pale wanapoona maisha yao yapo Katarina....

Ndiyo maana umeona majeshi ya walinda amani wapo Goma sasa hivi na wanapishana na M23 barabarani.
 
Hebu wewe Mwenye kitu kilete.Ninyi Nguchiro mmefadhiliwa Tz na mnalipiwa mishahara kwa Kodi zetu afu mnaleta dharau. Na kwa chuki mnayotengeneza Rwanda siku pakichafuka sijui mtaenda wapi
Mkuu ulivoongea kwa hasira mpaka nimecheka kwani watakuja ndani kwako?
 
Kwa sasa mpango uliopo ni kupitisha operesheni ya kuwaondoa wahamiaji haramu wote ni kuwarudisha nchini kwao, mikoa itakayoanza ni Kigoma, Geita, Katavi, Kagera.
Rudia upya kusoma ulichoandika.
Ni kipi kinachofanya mtake kufanya operation ya kuwarudisha kwao?
It's too late mzee baba, endelea kukariri.
JWTZ ilikuwa kipindi kile cha akina jenerali Mayunga, ya sasa haiwezi fanya lolote kwa Rwanda
 
Watanzania tunaishi sana kwa historia.

Jeshi imara halinunui silaha, jeshi imara ni lile linalotengeneza silaha zake zenyewe.

Ukiwa unanunua silaha, tambua na wenzio wananunua silaha, mkipigana vita mtambue hiyo ni vita baina yenu na wale wanaowauzia silaha.

WaAfrica tuache unyumbu, tusome, tujifunze, tukuze vizazi bora, tupendane, tuache kuwa vibaraka.

Africa hakuna jeshi lenye nguvu, Africa kuna vibaraka tu wa nchi na magenge ya wauza silaha duniani kifupi waAfrica NI wanasesere.
Binafsi siamini katika uimara wa jeshi...naamini katika maudhui mazima ya kupigana.....

Jeshi imara la nchi yenye uchumi mkubwa duniani lilipigwa Vibaya na Vietnam....askari akiwa anajua anachopigania kina maslahi kwake na kwa taifa uimara wa jeshi huanzia hapa.

Tanzania hatuna sababu ya kuingia Congo....hakuna sababu yoyote.
 
JWTZ hawapo Congo kupigana....ni walinda amani.

Ndiyo maana umeona Kagame amewalalamikia SANDF maana waliingizwa mkenge. ......Mlinda amani hajibizani na waasi hadi pale wanapoona maisha yao yapo Katarina....

Ndiyo maana umeona majeshi ya walinda amani wapo Goma sasa hivi na wanapishana na M23 barabarani.
Mkuu humu watu wanaongea kama wamekatwa vichwa
 
Jeshi lenye nguvu haliwezi hata kushona sare zake lenyewe, halina hata tekinolojia ya kutengezea mabuti ya askari wake wala uwezo wa kutengeza hata gobore!

Acheni ujinga nyinyi na pride ya kiuwendawazimu!.

Majeshi ya waafrika yapo zaidi kulinda watawala wasipinduliwe lakini si kulinda wananchi wala rasilimali zao.

Ndiyo maana watawala wake wanaingia mikataba mibovu ya kuuza rasilimali za nchi na majeshi yapo yanakodoa macho tu!
Hivi na wewe unaamini kabisaa JW hawajui kutengeneza hata silaha kama bunduki hizi ambazo huko mapori ya hifadhi zinatengenezwa na vibabu vizee kabisaa??

Hiv umeshawahi hata kutembea workshops za jeshi la Suma au Magereza ukaona products wanazo tengeneza na ukakosa kuona hizo boots?? Au mnaoongeaga tu na wala hamjawahi kuhudhuria workshops zozote za majeshi yenu??

Au unataka uambiwe Kiwanda cha silaha ndogo ndogo au za kati cha JW hapa tz kiko mkuranga au kibaha au Mlandizi? Ndicho unachotaka ujue kupitia mitandao?

Polen sana. Shida vijana mnaongea sana kuliko kufuatilia mambo. Yan Rwanda watengeneze silaha halafu Tanzania washindwe?

Vitu vingine ni spinning tu..
 
M23 sio Rwandese ni Congolese 💯
M23 ni wanyarwanda, hao ni watusi...

Congo hatuna watusi ila Rwanda...

Ni kama watusi walio katavi kule wajiite watanzania, haiwezekani maana kwenye makabira 120 ya bongo hakuna mtusi...

Hawa watusi wanaishi kwenye nchi za watu kwa huruma tu ya wananchi wa nchi hizo....

Kwanini Jaruo na Masai hawasumbuliwi?

Mtusi ana tamaa, ubaguzi na roho mbaya.
 
Mkuu humu watu wanaongea kama wamekatwa vichwa

Internet imesaidia saana kuonyesha aina ya binadamu wanaoishi duniani.

Zamani nilidhani nikiliwa jambo basi asilimia kubwa ya watu nao wanauelewa huo huo.....Nadhani asilimia 90 ya watu hawapati taarifa sahihi ....maana kuelewa mambo lazima upate taarifa sahihi....
 
M23 ni wanyarwanda, hao ni watusi...

Congo hatuna watusi ila Rwanda...

Ni kama watusi walio katavi kule wajiite watanzania, haiwezekani maana kwenye makabira 120 ya bongo hakuna mtusi...

Hawa watusi wanaishi kwenye nchi za watu kwa huruma tu ya wananchi wa nchi hizo....

Kwanini Jaruo na Masai hawasumbuliwi?

Mtusi ana tamaa, ubaguzi na roho mbaya.
Hao ni Wacongo wenzio....bahati nzuri nimefika maeneo hayo....Vizazi na vizazi wameishi hapo.

Mwaka 1971 mlipokuwa na mgogoro wa uraia ulitokana na nini? Unajua kwamba kifo cha Lumumba viongozi wengi kutoka jamii ya Lumumba waliwalaumu wanyamlenge.

Wakoloni wa kibelgiji ilikiri kati ya mwaka 1920 iliwasafirisha watutsi wengi kwenda kufanya kazi kwenye mashamba yao Eastern Congo. Now tell me....mtu aliyeishi Congo toka 1900 leo 2025 unamwambia sio raia wa Congo does it make sense??
 
Rudia upya kusoma ulichoandika.
Ni kipi kinachofanya mtake kufanya operation ya kuwarudisha kwao?
It's too late mzee baba, endelea kukariri.
JWTZ ilikuwa kipindi kile cha akina jenerali Mayunga, ya sasa haiwezi fanya lolote kwa Rwanda
Hawana uhalali wa kuishi Tanzania na hiyo inafanyika kwa nchi zote duniani.

Vile vile usisahau sisi tunapokea wakimbizi wengi kutoka Congo, Burundi na Rwanda.
RPF ni weak sana kwa JWTZ.
 
Internet imesaidia saana kuonyesha aina ya binadamu wanaoishi duniani.

Zamani nilidhani nikiliwa jambo basi asilimia kubwa ya watu nao wanauelewa huo huo.....Nadhani asilimia 90 ya watu hawapati taarifa sahihi ....maana kuelewa mambo lazima upate taarifa sahihi....
Mkuu hili tatizo naona kama limezidi kwenye majukwaa ambayo watoa maoni ni watanzania. Taarifa sahihi inaweza kuwa sababu japo sioni kuwa ni mara zote. Watu wanapenda upotoshaji zaidi kiasi kwamba watu wenye uelewa wa mambo hawatoi maoni yao kutokana na upotoshaji habari kuwa mkubwa.
 
Unajiandikia tu km huna kichwa...
Deep states haziendeshwi hivyo duniani pote. Ukiona majaribio ya mapinduzi yanafeli basi hayo ni maandalizi ya kuingia mapinduzi kamili, ref. Syria.
Unataka kunambia JWTZ ni bora kuliko RDF?. Kwa sasa Rwanda ni nchi yenye intelejensia kali kuliko nchi yoyote Central & East Africa na mbaya zaidi imeweka watu wake katika kila serikali kwenye sekta za maamuzi... Anzia ikulu ya Samia, TISS, JWTZ, JKT, POLICE, mashirika yote muhimu yote ya umma pote huko kuna wanyarwanda kibao wamejazana.
We kuweza Rwanda na JWTZ yako?
Sasa mbona mtazamo wako unakua openly biased?
Kama wao wameweka watu wao kwetu, nini kinakufanya uamini sisi hatuna watu wetu kwao?
Labda nikujuze tu, pale washington na pentagon wamejaa warus kibao. Na pia pale Kremlin na Lubiyanka wamejaa Americans wa kutosha..
Hivi ndivyo game ya intelligenve inachezwa. Tumia akili
 
Hawana uhalali wa kuishi Tanzania na hiyo inafanyika kwa nchi zote duniani.

RPF ni weak sana kwa JWTZ.
Ila hao hao wahamiaji haramu wana uhalali wa kufanya kazi ikulu na taasisi zote nyeti na wana uhuru wa kuuziwa viwanja na kuwa na vitambulisho vya NIDA km watanzania sababu ninyi siyo wabaguzi?
Nasema hv; It's too late, na Kagame sasa anainyemelea bukoba, ni suala la muda tu!😂
 
Hao ni Wacongo wenzio....bahati nzuri nimefika maeneo hayo....Vizazi na vizazi wameishi hapo.

Mwaka 1971 mlipokuwa na mgogoro wa uraia ulitokana na nini? Unajua kwamba kifo cha Lumumba viongozi wengi kutoka jamii ya Lumumba waliwalaumu wanyamlenge.

Wakoloni wa kibelgiji ilikiri kati ya mwaka 1920 iliwasafirisha watutsi wengi kwenda kufanya kazi kwenye mashamba yao Eastern Congo. Now tell me....mtu aliyeishi Congo toka 1900 leo 2025 unamwambia sio raia wa Congo does it make sense??
Kama nimeipata hoja yako ni kwamba wewe(assume ni mfipa) ukienda Rwanda ukaishi mda mrefu utaitwa Mnyarwanda?

Nakuhakikishia utaendelea kuitwa mtanzania na hutokua na haki za msingi kwenye nafasi nyeti serikalini...

Sasa kama ukienda Rwanda inakua hivyo kwanini iwe tofauti kwetu?
 
Ila hao hao wahamiaji haramu wana uhalali wa kufanya kazi ikulu na taasisi zote nyeti na wana uhuru wa kuuziwa viwanja na kuwa na vitambulisho vya NIDA km watanzania sababu ninyi siyo wabaguzi?
Nasema hv; It's too late, na Kagame sasa anainyemelea bukoba, ni suala la muda tu!😂
Wewe ni mgumu sana kuelewa.

Lakini pia, hilo haliwezekani na haitakaa litokee hadi wewe mwenyewe unaingia kaburini.

RPF ni weak sana kwa JWTZ.
 
Kama nimeipata hoja yako ni kwamba wewe(assume ni mfipa) ukienda Rwanda ukaishi mda mrefu utaitwa Mnyarwanda?

Nakuhakikishia utaendelea kuitwa mtanzania na hutokua na haki za msingi kwenye nafasi nyeti serikalini...

Sasa kama ukienda Rwanda inakua hivyo kwanini iwe tofauti kwetu?
Haihusiani....

Ngoja nikufafanulie vizuri uelewe.
Rudi mwaka 1900...mimi ni mmasai...sina serikali kama ilivyo sasa. Kiongozi wetu ni Leingwanan....wakaja watu wakanihamisha nilipokuwa naishi nikaenda sehemu nyingine kuwafanyia kazi. Nikaishi sehemu mpya kwa miaka nikazaa watoto ...nikafa.

Baadae kutokana na maendeleo ninapoishi pakajitawala na pakajipa jina. Serikali mpya ikampa kila aliyekuwa anaishi ndani ya hii sehemu mpya uraia baada ya kujipatia huru.

Swali je, nchi yangu ni ipi? Unataka wajukuu zangu warudi nilipotoka miaka 100 iliyopita?

Watumwa wa Marekani ni wamarekani wenye asili ya kiafrika. Ukimrudisha Rick Ross Afrika leo unampeleka wapi? Hajui chochote kuhusu Afrika....
 
Kama nimeipata hoja yako ni kwamba wewe(assume ni mfipa) ukienda Rwanda ukaishi mda mrefu utaitwa Mnyarwanda?

Nakuhakikishia utaendelea kuitwa mtanzania na hutokua na haki za msingi kwenye nafasi nyeti serikalini...

Sasa kama ukienda Rwanda inakua hivyo kwanini iwe tofauti kwetu?
Tatizo la Wanyarwanda wameishi na kukua katika propaganda za ukabila, hivyo hawawezi kuacha ni asili yao.
 
Sasa mbona mtazamo wako unakua openly biased?
Kama wao wameweka watu wao kwetu, nini kinakufanya uamini sisi hatuna watu wetu kwao?
Labda nikujuze tu, pale washington na pentagon wamejaa warus kibao. Na pia pale Kremlin na Lubiyanka wamejaa Americans wa kutosha..
Hivi ndivyo game ya intelligenve inachezwa. Tumia akili

Yaani unaongea as if unaamini wabongo wana akili nyingi za kufanya hivyo.

Mambo ya kijinga kama kuwa na bajeti ya kununua V8 nyingi kuliko bajeti ya wizara ya kilimo inaonyesha wazi kuwa bongo haina mental sophistication ya kuinfiltrate jeshi la PK au usalama wa Taifa wa RWNDA.

PK alisema akipewa hiyo bandari tu anaweza kuigeuza Bongo kuwa kama ulaya. Sisi hata kuendesha bandari hatuwezi tumempa mwarabu.

Nakushauri, ili usipate stress, bongo usiichukulie serious kivile. Kama vitu basic hatuwezi, usifikiri kama complex mission za kuinfiltrate majeshi ya Rwanda tunaweza!.

May be uwezo wa bongo unaishia kwenye kuwapoteza akina Soka, Ben Saanane, kudeal na akina mzee Kibao, watu wasio na threat yoyote kwa nchi! basi!
 
Back
Top Bottom