2015-uchaguzi mkuu na hatma ya nchi


Mchambuzi:

Ulizoandika hapa hizi zote ni longolongo tu za kisiasa na hazina mshiko wowote kwa maisha ya watanzania. Umetumia muda mwingi kueleza jinsi chama tawala kilivyofanya mabadiliko ndani ya nchi.

Ukweli wa mambo, chama tawala kilifanikiwa kwenye kuleta uhuru. Baada ya hapo mipango yote iliyofuatia ilikuwa kama majaribio ya sayansi ya mtoto wa darasa la tatu.

Kitu kilichofanya chama hiki kuendelea kuwa madarakani. Ni upeo mdogo wa kielimu wa wananchi, ulaghahi wa wanasiasa na misaada kutoka nje.

Tanzania ingekuwa na wasomi miaka ya 60 na 70, Nyerere asingeweza kukaa madarakani kwa zaidi ya miaka 10. Toka nchi ipate uhuru, chama tawala ni chama chenye mipango ya kilaghahi. Unatoa mifano ya viwanda. Let's get real. Hivi Tanzania ilikuwa na viwanda gani vya maana vya kuleta ajira?

Hata kama nchi ilikuwa na viwanda, nitajie just five business executives ambao walikuwa uwezo wa kuendesha mashirika ya umma kwa ufanisi. Huwezi kusema kulikuwa na mipango ya kuweka uchumi mikononi mwa wananchi wakati wananchi wenye hawajuhi jinsi ya kuendesha uchumi.

Tukirudi kwenye data zako za uchaguzi, watu walishiriki kwa wingi wakati wa mfumo wa chama kimoja kwa sababu moja kubwa: uchaguzi wa wabunge. Uchaguzi wa wabunge ulikuwa ndio njia pekee ya watu kutumia haki zao za kidemokrasia. Uchaguzi wa rais (ndio au hapana) ulikuwa sio kivutio. Na kama uchaguzi wa rais ungekuwa unafanyika pekee yake, maudhurio ya wapiga kura yangekuwa chini. Hivyo kushiriki kwa wananchi kwa wakati hule haikuwa ni ishara ya mafanikio ya serikali.

Tukirudi kwenye uchaguzi wa 2015, wapiga kura wengi ni vijana. Mtazamo wao ni tofauti na wapiga kura wa 60, 70, 80, na 90. Vijana hawa wanataka viongozi watakaoweza kuja na ufumbuzi wa matatizo yao na ya nchi kwa ujumla. Miaka ya zamani watu walifurahi serikali kuwa na viwanda bila ya wao kufaidika. Siku hizi watu wanataka kuona wanafaidika vipi na rasimali za umma.
 

Mkuu uko sahihi ila naomba kuongezea kidogo hapo kwenye vijana wa siku hizi.

Ni kweli kuwa wanataka kuona wananufaika vipi lakini sio na rasilimali za umma tu. Vijana wa leo huanza kuangalia wananufaika vipi na mgombea. Ndio maana wananunulika kirahisi. Ukweli ni kuwa vijana siku hizi wamepoteza imani na ahadi za wagombea, wanataka ikiwezekana wamalizane naye kwa kuwalipa.

Wengine hupiga kura kwa mkumbo tu. Ni vijana wachache wanaweza kuelezea why they voted for someone. Hata nature ya mijadala inaonyesha watu hawaangalii vigezo vya uongozi rather than kusukumwa na ushabiki.
 

..THANK U!!

..yaani tungekuwa baa, ungepimwa urefu wako, halafu tungekuagizia crates za bia ya safari kulingana na urefu huo.

..that is what we used to do back in the days.

..jokes aside, umeeleza jambo zuri sana na ukweli kuhusu kinachoendelea huko vijijini.
 


Umenifurahisha mkuu, ni kweli vijana nao sio wa kutegemew sana wananunulika mno, hawana critical argument why do they vote, ila naamini elimu inazidi kuwafikia watabadilika
 

ZeMarc:

Tofauti kubwa kati ya wanyama wengine na binadamu ni matumizi ya intellect. Wanyama wengine wanafanya matendo yao mengi kwa asilia wakati binadamu inabidi tujifunze. Kwa mfano mbuzi akizaliwa, baada ya muda anaanza kutembea. Mtoto wa binadamu akianza kutembea baada ya kuzaliwa itakuwa alijifunza tumboni kwa mamake na tutamwita mtume.

Matendo wanayofanya vijana ni vitu walivyojifunza kutoka kwa waliowatangulia ambao wanaikumbuka siku ya kupata uhuru. Waliandamana kuunga mkono azimio la arusha. Walikuwa ni viongozi wa mashirika ya umma na taasisi za kiserikali. Walikuwepo siku ya kuzaliwa kwa chama cha Mapinduzi.

Excellency inarithishwa. Mwenye akili timamu hawezi kusema azimio la zanzibar ndilo liloondoa maadili ya uongozi. Kwani tabia za watu sio swichi ya umeme. Kama mtu ana uhakika kuwa Lowassa ni mwizi, basi hakuanza tabia hiyo 1991 baada ya kutangazwa kwa azimio la Zanzibar. Na kama mtu alikuwa mla rushwa kabla ya february 1967, hakuacha tabia yake baada ya azimio hilo kutangazwa.

Point yangu kubwa ni Tanzania inahitaji mtu jasiri au kikundi jasiri cha watu cha kubadilisha mfumo mzima wa utawala. Uchaguzi wa 2015 ungelenga kumpata jasiri huyo au kikundi cha majasiri hao.
 

Comrade Mag3,

Leo nimepitia maandiko mengi sana tuliyofanya zamani kabla hata ya awamu ya nne kuja. Nimebaki nastaajabu kuwa kila tulichosema na kujadiliana, hata kutoa mawazo mbadala na ya mtazamo tofauti kwa CCM au Upinzani, watu wameendeleza libeneke lilelile, halafu leo tunataka wagombea watakao orodhesha na kuoanisha matatizo ya Tanzania na jinsi gani yatatuliwe.

Tunarembuka macho kufuatilia hotuba ya January na Mwigulu, tunasema hizi zimetulia zimekaa kisomi na kwa mpangilio unaoeleweka.

Lakini tunasahau kuuliza, je ni kipi walichokifanya kwa miaka mitano iliyopita ya wao kuwa wabunge kwa manufaa ya majimbo yao na Taifa?

Hatuwaulizi hizo orodha walizotutajia ambazo kina Zakumi, Mkandara, Kishoka, Mwanakijiji, Kuhani Mkuu, Susuviri na JMushi wamekuwa wakizisema miaka nenda rudi wao wakisoma hayo mawazo na malalamishi humu lakini walipopewa ubunge na hata uwaziri, hawajayafanyia kazi au kupatia utatuzi au hata kuonyesha msimamo ndani ya baraza la Mawaziri na Chama kuwa lazima mageuzi ya mazoea yafanyike na kilio cha wananchi ni cha kweli.

Je u-mbuni wetu ni mpaka lini? je ujinga na sasa upumbavu wetu na kujifungwa katika utumwa wa fikra na vitendo vitaendelea mpaka lini?

Kama ni kulogwa au kupagawa, basi kipapai tulichopigwa kimekolea sana kwamba hata kuthubutu kukataa kudanganywa na kuburuzwa hatuoni.

Nguruvi kaonyesha vizuri sana jinsi gani mfumo wa mazoea ulivyojengeka na jinsi tulivyokuwa na dhamira ya kuchuna ndani ya kisoda cha CCM kupata ushindi, lakini kila mara tunaambiwa jaribu tena na tunaendelea kuamini tutapata nabii mpya wa kutuvusha jangwani.

Tathmini yangu ya mwaka 2010 kuwa 40% ya wabunge hawakustahili, haikuwa sahihi. Nilichokiona ni kuwa 80% ya wabunge hawakustahili hata kidogo kupewa dhamana na majukumu makubwa kama hayo.

Lakini kwa ajili ya ushabiki na uzezzeta wa mawazo kama tumelishwa limbwata, tumechagua Wapumbavu watuongoze sisi Wajinga!

Sielewi ni vipi tuwe na tumaini na January au Mwigulu au Magufuli tofauti na Lowassa au Membe!
 

Imekuwaje mtu mmoja tu, aiyumbishe nchi nzima na hasa chama kizima kwa kuwa na Taswira iliyosheheni ya ufisadi? How did he manage to become an SI unit ya ufisadi?

Waliokuwa na wajibu na dhamana kumdhibiti na kumwajibisha (CC, NEC) ilikuaje wamemuachia akajijenga na kuwa mfumo kamili ulio na uhai na tegemeo lao ni kumnyima Urais pekee bila kumfikisha panapopaswa kisheria ili kukomesha na kuiondoa hii Satarani ya Ufisadi?

Kama yeye ni mzizi mkuu, kwa nini mwenye sululu, mundu na jembe hawamkati mbali na kumuondoa?

How did he become such a powerful and unstoppable force? je kumnyima kugombea Urais kupitia CCM ndio kutamwadhibisha na Ufisdai wake?
 
Mkuu Rev. Kishoka , Lowassa kama kwa sasa ndiye SI unit ya Ufisadi, basi hatuna utawala, hatuna serikali na katika msingi huo hatuna taifa, Utetezi kama anaoutoa ZeMarcopolo ndio aina ya mentality niliyoipiga vita, naipiga vita na nitaendelea kuipiga vita...ni utetezi unaotoa taswira halisi ya jinsi Mtanzania wa sasa alivyoathirika.

Waziri Mkuu Mizengo Pinda aliwahi kutamka, nanukuu, "Mafisadi wana nguvu sana, serikali ikiwachukulia hatua nchi itayumba!" Tamko hilo halina tofauti na hilo la ZeMarcopolo na ni tamko linaloweza kutolewa tu kwa wajinga! Hebu badala ya Mafisadi weka Lowassa, kwamba Lowasssa ana nguvu kiasi cha kuliyumbisha taifa kama atakamatwa.

Pinda alisema hivyo, Watanzania wakamwelewa hivyo, wananchi wakaafiki kama alivyoafiki ZeMarcopolo na hivyo kuliepusha taifa na mtikisiko! Pinda anaendelea na Uwaziri Mkuu kama kawaida, ni kiongozi mkuu wa serikali bungeni kama kawaida na hivi sasa ni moja kati ya watangaza nia wanaotuahidi kushughulikia ufisadi wakichaguliwa!

ZeMarcopolo hayuko peke yake, wako wengi. Lowassa hayuko peke yake, wako wengi. Kinachowaunganisha pamoja ni chama tawala, chama kilichokaa madarakani kwa miaka zaidi ya hamsini, chama kinachoapa kubaki madarakani hata kwa miaka mia zaidi na chama kinachotamba na kilicho na jeuri ya kuwaita wapinzani waroho wa madaraka!

Ajabu ni kwamba Watanzania tupo, tupo sana tu mimi na wewe na ingawa tupo ni kama tumepigwa ganzi na uchungu hatuusikii. Tungekuwa tunasikia uchungu leo hii Pinda asingekuwa madarakani, hii serikali haingedumu hata kwa saa moja zaidi na hiki chama kinacholea, kinacholinda na kinachokomaza maadui wetu, kingekuwa historia.

A luta continua...
 
Kuondoa Rushwa na Ufisadi Tanzania ni kazi ngumu sana: Maji, Sabuni, Dodoki, Taulo, Mafuta, Kitana, Nguo na Viatu vyote ni Rushwa tupu na Ufisadi: Tutajitakasa vipi?
Rev. Kishoka long time mkuu

Kuondoa rushwa na ufisadi si jambo gumu. Nchi zilizofanikiwa zilikuwa na rushwa kama sisi.

Hata sasa, nchi zote zikiwemo Japan,Scandanavia, Denmark, Finland, New Zealand na kwingine zimefanikiwa kutoka na dhamira, na kutekeleza dhamira hiyo kwa vitendo


Nchi nyingine zinazokabiliwa na rushwa, zinaonyesha wazi zinavyopambana kwa nia njema ya udhati. Mfano, ni China.

Utakumbuka kiongozi wa taasisi iliyoshindwa kuzuia ‘sumu ‘katika maziwa ya watoto, alisimama kizimbani akalambwa risasi

Nia ya dhati inaanza kwa mtu, kisha uongozi na kufikia wananchi.
Uongozi wa nchi unapoonyesha kuchukizwa na rushwa na kutekeleza kwavitendo rushwa inawezekana


Kwa hali yetu, nia za dhati za za viongozi hazipo kabisa. Tena wanaonyesha kwa kuficha maovu.

Siku hizi wanatumia taasisi za umma kutetea rushwa. Tunajua PCCB ni chombo cha dagaa.
Tunasikia ofisi kubwa zikisafisha wahalifu. Hakuna kufika mahakamani, ni taarifa kwa umma
fulani msafi

Walikataa rasimu ya Warioba, kuweka maadili, na kuzondoa taasisi muhimu mikononi mwa viongozi kutaleta ‘balaa''

Kwa uhuni wakasema S3 zitaongeza gharama.
Leo wanaongeza majimbo na si kupunguza kama rasimu ya Warioba ilivyosema


Hatuwezi kufanikiwa kwasababu wanaotaka kuondoa rushwa ndio wanaotaka kuongoza nchi hii.

Yaani waliolelewa na mfumo huu mchafu ndio wanaotaka kuondoa.


Mwanajamvi Alinda ameuliza ,hivi wagombea wa CCMwanawezaje kupita katika mikono michafu,wakatueleza ni wasafi?

Wananchi wana shea yao, kuhakikisha wanachagua watu wenye nia ya dhati.

Kama watakubali kuhongwa, wajue wala rushwa wanawekeza. Tusijekulaumina watakapodai dividend ya uwekezaji wao
 
Mkuu Rev.

Mkuu Mag3kasema Watanzania ni wajinga au wana ubindamu sana.
Nguruvi
kasema, Watanzania ni mazezeta. Kishoka kasema tumelogwa au kipapai .

Alinda kasema, hivi mtu anatokaje katika mfumomchafu, tukakubali ni msafi

Alimaanisha, watu wameoga kwenye ''sewerage'wakajifuta na taulo wanalotumia wote kwa miaka yote, wanatuambia ni wasafi.Nasi tunakusanyika kuwasikiliza wakitufunza namna ya kuwa safi

Wagombea wanajdiliwa na kupewa nafasi kana kwamba wamekuja na Mworabaini.
Watanzania wamesahau, Wassira ni waziri tena alikuwa wa sera.Sera ndizo zimetifkisha hapa tulipo.


Membe ni waziri, juzi kasema akichaguliwa atahakikisha mtoa rushwa na mpokea rushwa wote wanapata kibano.
Membe amechukua kauli ya uaminifu ya wana TANU. ''Rushwa ni adui wa haki, sitapokea au kutoa rushwa''


Membe huyo huyo anayetaka kusimamia sheria, ameweka kiporo cha Radar.
Hajatuambia nani walitoa nani walipokea. Anataka Wtzn wasubiri akiingia Ikulu atawataja!
Watz wanapiga makofi kwa bidi.

January ni waziri. SI huyu January ndiye alishindwa kushughulikia tatizo la kodi za simu?
Nakumbuka
@Mzee Mwanakijiji aliendesha kampeni hapa jamvini iliyofanikiwa kubadili mwelekeo wasuala hilo kuliko naibu waziri January


Mwigulu, si naibu waziri! Misamaha ya kodi inapita mikononi mwake kila uchao.
Misamaha ni mikubwa kuliko bajeti ya wizara ya elimu.


Lowassa, si alikuwa waziri mkuu. Richmond ilipoanza EL alisimama bungeni na kusema taarifa ya PCCB haikuona tatizo. Baadaye tukagundua madudu. Akakaa kimya miaka 7

Wote hao wapo katika CCM kama viongozi. Wapo serikalini kama viongozi.

Wanafanya maamuzi yanayohusu rushwa zote. Wamekaa kimya, hakuna anayeonyesha kuchukulizwa na rushwa kama yule mama Linda wa Uingereza aliyeachia uwaziri kwa huruma ya pesa za radar zinavyochotwa.

Wote hao hakuna anayetuonyesha amefanya nini kupigana narushwa.

Ajabu kubwa, Watanzania wanawawajadili kana kwamba ni kundi la malaika lililoteremeshwa ili kutupatia nabii mmoja.

Hivi kweli miaka 10, na 50 Watz hawaoni sababu zozote nakujiuliza, kufanya jambo lile kila siku bila matokeo tofauti ni ujinga,uzezeta, kipapai au Limbwata !
 

Mimi ninachoona ni CCM kutumia nguvu nyingi kutuaminisha kuwa ndani ya CCM ni Lowassa tu ndo mla rushwa,

Kwamba ikitokea Lowassa akahama chama au akaachana na siasa basi CCM itakuwa safi,

Kwamba CCM inachafuliwa na Lowassa tu?

Hivi kweli ndani ya CCM fisadi ni Lowassa? au ni nguvu nyingi zinazotumika kutuaminisha hilo? Vp Magufuli na bil.200 zilizopotea bila maelezo? Vpi Membe na pesa za Gadafi? Vp Sitta na chenji ya bunge la katiba (maana ni lazima chenji irudi baada ya wapinzani kujitoa) au ile nyumba ya Spika jimboni kwake (pesa haikutoka kwenye mshahara wake bali ni kodi za walalahoi) Vp Kinana na meli? na je tunasemaje kuhusu Werema na ushauri wake wa mabilioni ya Esrow?

Ukiangalia haya yote unaona ndani mwa CCM hakuna mtu msafi kila mtu ana makando kando yake tena yanaweza kuzidi hata ya Lowassa na hiki ndo kinampa Lowassa kichwa cha kutaka kuwa rais wa Tanzania maana anafahamu kabisa kwa viongozi tulionao ndani ya chama cha mapinduzi hakuna anayeweza kudhubutu kumyoshea kidole..

Na kama CCM wanania ya dhati ya kujisafisha hawana budi kuchukua maamuzi magumu ya kuwavua uongozi watuhumiwa wote wa rushwa, ufisadi, mikataba mibovu, Nyara za serikali na baada ya hapo wakifishwe katika vyombo vya sheria.

Ila sasa swali lina kuja nani mwenye hudhubutu wa kufanya haya? Ni kikundi gani ambacho kinaweza kuwachugulia hatua viongozi wote tangu awama ya Mkapa hadi kwa Kikwete? Maana tunaposema viongozi wote, kwa bahati mbaya hata hawa marais wetu wanatuhumiwa kula rushwa.

Pia kwa bahati mpaka sasa hivi kati ya watangaza nia zaidi ya 30 sijaona mtu mwenye uchungu na matatizo ya watanzania, Sijasikia mtu akielezea mafanikio yake katika sekta aliyosimamia zaidi ya kusikia "Nitapambana kuodoa rushwa na bla bla lakni si Nimepambana na rushwa ... Sasa kiongozi wa namna hii kwanini achaguliwe tena? Maana tumempa "Chance" aonyeshe umahili wake lakini ameshindwa sasa anachotaka ni nini tena?
 

Swala la Lowassa kuwa na nguvu ni uwoga tu wa serikali yetu..

Hivi tujiulize swali rahisi hivi katika sakata la Escrow ni nani achukuliwa hatua zaidi ya watu kujiudhuru uwaziri na kubaki na ubunge. je hata hawa wananguvu? kwamba Jaji Werema ananguvu sana hawezi kuguswa pamoja na kutoa ushauri mbovu kwa serikali?

Halafu watu wale wale katika serikali ile ile ambao ni waoga wa kuchukualia wala rushwa hatua ndio hao hao watangaza nia.. mtu kama Pinda eti naye anataka kuwa rais kwa lipi alilofanya? Hata swala la Albino lilimshinda kulishughulikia zaidi ya kumwanga chozi tu hakuna alichofanya! Ila naye anataka kuwa rais...
 
ZeMarcopolo,

Asante kwa mchango wako. Hakuna research niliyowasilisha zaidi Ya hoja iliyoambatana tu na takwimu ambazo ni secondary data from a variety of sources. Suala juu Ya kwanini wananchi wanatafuta hati Ya kupiga Kura, hilo sikuligusa kwa sababu sikuona mantiki Ya kufanya hivyo. Kama zoezi husika ni la kuandikisha wapiga Kura lakini mwananchi Yeye analenga kupata Kitambulisho kwa ajili Ya matumizi nje Ya kupiga Kura, Bado mwananchi huyo atahesabiwa kama mpiga Kura Ambae alijiandikisha kupiga Kura lakini hakujitokeza. If that's what you call an interpretation, it's actually more than that, it's a fact.
 
Last edited by a moderator:

Orodha ya machungu na machozi ya mamba kulia uchungu si tija. Mbona Kikwete alikuja na mbwembwe za kuelewa matatizo na kilio cha Watanzania na akatoa kipaumbele kwa wawekezaji?

There is no time to measure or try to study their emotions or sympathy to makali ya maisha! We need to measure their past performance and commitment that they have demonstrated in last years as individual to rid poverty, kusimamia haki, kuleta uadilifu na uwajibukaji na kuwa wabunifu wa kuongeza tija na ufanisi.

Haya mambo ya watu wanajidai wanayajua machungu lakini do not have know how or any way to show they have achieved success iwe ni udiwanik ubunge, au walio ma DC na mawaziri is waste of time!

We have spent years learning our emotions and they are still same: machungu na matatizo ni bado yale yale : Ujinga, Umasikni, Njaa na Maradhi!
 
Rev.Kishoka suala la EL kuwa na nguvu lianonyesha udhaifu wauongozi wa CCM uliopo.
Mrema alikuwa maarufu sana, wakati ulipofika walimuondoa, CCM ikabaki


Udhaifu huo tunauona katika serikali. Nyerere aliposema chama lege lege huzaa serikali lege lege ndicho kinachotokea

Kundi linalosumbua taifa halizidi watu 25. Ili liendeleeku-survive ni lazima liwe na kiongozi, ndiye anafanyiwa kila mbinu.Kundi linapesa, limeshanunua chama na serikali.

Linanua wanachama wenye influence na nyadhifa.
Limeshatishia kutenga nafasi za Uenyekiti na Urais.
Kwa kutumia pesa kununua hadi media, viongozi wa dini na taasisi, EL anaonekana tishio kwa CCM.

Ukweli ni kuwa si tishio kwasababu nguvu yake si ya wanachama,ni ya wanachama walionunuliwa.

EL akiondolewa katika chama, hakuna atakayemfuata.Biashara kati yake na watumishi itafikia ukingoni.

Tatizo linalowakabili CCM si EL ni mfumo mzima . Huwezi kumwajibisha wakati wanunuzi wanaangalia na ndio wafadhili wenye chama.

Mfumo mzima umelegea kuanzia enzi za mtandao. Kila mmoja anaanzisha mtandao na kudai anapiga vita rushwa ili kupata sympathy za wananchi.

Tunauliza, hivi mtu aliyelelewa, kukulia na kufanikiwa ndaniya mfumo wa rushwa anawezaje kuupinga mfumo huo?

Watangaza nia wanajua mfumo warushwa ndio unaongoza CCM na serikali, wamo hawajapinga!
Majukwaani wanaonyesha hisia na uchungu wa rushwa! Huu utapeli tuna ukubali kila siku, lini tutafunguamacho!


Wananchi wafungue macho, mtu akisema anapinga rushwa,wamuulize lini alipinga rushwa hiyo?

Huwezi kuwa mtumishi wa CCM na serikaliyake ya sasa ukasema unapingana na rushwa.

JK alikuwepo kuanzia madudu ya mtambo wa Tegeta ulipotiwa sahihi kwa mara ya kwanza.
Amekuwepo katika mfumo madudu ya meremeta, Tangold,Kagoda n.k. yakitendeka.
Anaondoka akiacha orodha kubwa kuliko aliyoikuta.


Mfumo uliotumika kumpa ushindi ndio alioutumikia. Hawa wanaokuja leo wanawezaje kuukana mfumo uliojikita na kuhodhi serikali na chama?

Waulizeni kwanza, wamepinga vipi rushwa na siyo watapingavipi rushwa
Waulizeni, wamepigana vipi na umasikini, na si watapiganavipi na umasikini
Waulizeni, wamepigana vipi dhidi ya ujinga, na si watapiganavipi na ujinga

Tusemezane
 
Ishu ya USAFI wa Wagombea isiishie CCM tu,imulike kwa wanasiasa wote bila kujali vyama,watanzania ni walewale,tumeona Zambia,Rais wa upinzani ulipoingia KATIKA Dora alifanya ufisadi,maana wengi wao wakishaongoza Dora wanajua wamepata ulinzi,na kuanza yaleyale ya ufisadi,tunaona ruzuku zinavyoliwa upinzani,upinzani ninaoutaka kwa sasa ni wakumiliki bunge,ili kuidhibiti serikali,ila tatizo upinzani hawaaminiki,tunaona KATIKA baadhi ya halimashauri wanashirikiana na CCM kufanya yaleyale
 

Hapana @Rev.Kishoka , Simaanishi kulia majukwaani kwa ajili ya kupata kura.. Ninachomaanisha ni ile hali ya mtu kuwa "in touch" na matatizo ya watu anawaogoza..

Na nafkiri kila mtu anaelewa ili utatue tatizo fulani,ni lazima uone kwanza kuwa hapa kuna tatizo, baada ya hapo unapiga hatua ya pili ni kutaka kulitatu na hatua ya tatu ni jinsi ya kulitatua hilo tatizo.


Kwa mantiki hiyo utaona kuwa tuko pamoja, maana haileti maana Mwanasiasa kuja kutulilia kuhusu ubovu wa barabara na baada ya miaka 5 karudi na kilio kile kile cha barabara hali alikuwa na uwezo wa kushirikisha wananchi na kutatua swala hilo, labda si kwa kiwango cha lami lakini kwa kiwango cha uwezo wa wananchi. Na hiki ndicho ninachomaanisha kuwa uguswe na matatizo ya jamii inayokuzunguka, na ili kuuguswa na haya matatizo ni lazima uishe/uwe na ukaribu na watu wa eneo husika. huyatafutie ufumbuzi na baada hapo tukupime kwa matendo yako, kwa jitihada zako na nk.

Labda nituo mfn kidogo tu.
Wakati wa Bunge la Katiba, Ukawa walijitoa, na walipojitoa inamaana hawakulipwa fedha ambazo zilishaidhinishwa na serikali katika bajeti ya Bunge la katiba.

Baada ya hapo kuna watu (sikumbuki kama ni wahandishi wa habari au nani) walimuuliza Mh. Sitta kuwa zile pesa za Ukawa zitarudishwa serikalini? Mh. Sita alijibu kuwa hizo pesa hazitarudi serikalini bali watazigawana wao na baadhi ya pesa hizo watafanyia shehere..

Anayeongea hivyo ni kiongozi tena ni kiongozi wa Tanzani ambao ni masikni, ambayo kuna watoto wa shule hawana hata dawati, kuna walimu hawana hata chaki za kuandikia wanaandika kwa kutumia mihogo, kuna manesi hawana hata gloves za kuzalishia mama wajawazito, kuna wajawazito unaotakiwa kwenda na vibatari wakati wa kujifungua, kwenda na nyembe, kwenda na ndoo za maji. Kuna wazee wasio na msaada wowote wanaishi kwa kudra za mwenyezi Mungu na nk.,

Nilitegemea kiongozi anayeguswa na matatizo ya mtanzania basi angesema hizi hela tutanunulia madawati au madawa mahospitalini au gloves, au hata chaki tu. Lakni alichoona ni muhimu ni kufanya sherehe, na kujigawia hizo hela.

Na kwa bahati mbaya zaidi huyu mtu anaye amechukua fomu, na kibaya zaidi kuna watu wanapanga foleni kwenda kumdhamini. Sasa sijui kama hii ujinga wa watanzani au ni uelewa mdogo au kutojali kwa watanzania, au ile kutaka kuonyesha na mimi nipo na nimemdhamini Mh. Sitta.????????????

Mf. huu wa Sita unaonyesha jinsi Sita hasivyokuwa na uchungu na matatizo ya mtanzania, unaonyesha kuwa ameishakula amevimbewa hata hajui kuwa kuna watu wana njaa kali hawajala siku mbili mfululizo, akili zake ndo zimekomea hapo hapo hawezi kuwaza zaidi.

Yeye anachowaza ni rushwa ya Lowassa tu. Na kama tukimchangua ataikomesha rushwa. SWali la kujiuliza je huyu mtu anatufaa??

Jimboni mwake kitu cha maana alichowafanyia watu wake ni kujenga jengo lenye thamani ya mil.500 (sijui ni lake au la serikali??) Wakati watoto wa shule katika jimbo lake hawana madawati..

Hivi kweli huyu anaguswa na matatizo ya Mtanzania??
 

Ni kweli kuwa "issue" ya usafi hisiishie kwa CCM tu bali iende hata kwa wapinzani.
Kwangu mie sijui madudu wa wapinzani ila kama wewe kuna chochote unachofahamu kuhusu ufisadi wa ruzuku basi ingekuwa vizuri kama ungetuweka chochote unachofahamu kuhusu ruzuku za vyama vya siasa na matumizi yake.

Inaniwia vigumu kuingia katika jukwaa la "Great thinker" na kuanza kujadili hisia hisia tu. Siwezi kusema Pro. Lipumba ni fisadi hali sijui kama kuna ukweli wowote, hivyo hivyo kwa Dr. Slaa, Mbowe au hata Zitto.. Principle ambazo nimejiwekea ni kuandika kitu ambacho nina uhakika nacho, sipendi majungu, sipendi fitina, sipendi matusi na sipendi kumsingizia binadamu mwenzangu.. Ndivyo nilivyo na ndivyo inavyoilea famila yangu.

Una maoni gani kuhusu uchanguzi wa mwaka huu?
 
Vyama vyote vya siasa kwa mujibu wa sheria vinawajibika kuwasilisha ripoti ya mahesabu yao kwa msajili wa vyama (au CAG kama sijakosea) na mpaka sasa sijawahi kusikia msajili wa vyama au CAG akihoji juu ya matumizi ya vyama hivi vya siasa kwamba hayako sawa! Hata hivyo hio haizuii kujadiliwa kwa ufisadi wowote ule kwenye vyama (kama upo). Hakuna sababu ya kupindisha mjadala wa ufisadi kwa viongozi waliopo sasa kwa vile tu hata upinzani nako kuna ufisadi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…