Visingizio hivi
Wakati mama Samia anaingia alianzisha kikosi kazi ambacho waliwekwa wanasiasa wote na kupeleka maoni na vikao kila Mara ikulu, akaanzisha 4R , akatengua wale wote mliowalalamikia, mkasifu mkasema mambo ndio haya, barabarani mkajaza mabango mama msikivu anaupiga mwingi, siasa Safi na kila kitu kimewekwa na kuimbwa
Leo mmekwama mnarudi tena kusema nini? Acheni kuwa vipofu
Mkuu usiumize kichwa kwa Hawa wapumbavuu wadumavu wa akili.
Kila mtu anajua serikali ya Samia ilifuta mambo mengi yalioachwa na Magufuli iliyoyaona hayana manufaa au hayana maana, na ilikuwa Ina uwezo wa ku cleanse serikali nzima mpaka Bunge yaani tukachagua wabunge wapya!...Yes, huo uwezo Samia alikuwa nao kama angetaka.
Kitendo Cha Samia kuendelea kunufaika na uozo ulioachwa na Magufuli ilihali anaweza kuufuta uozo huo, tafsiri yake ni kwamba hata yeye angeweza kuwa muanzilishi wa uozo... Kwa vile wengi hapa akili zao ni dunia hawawezi kuona hili.
Magufuli hayupo, lakini CCM Bado ipo na mambo mengi ya ovyo yanayoendelea leo hii hayajaanza leo hii Wala kwa Magufuli.....
Kama ni kuvuruga uchaguzi tumeshuudia tangu mwaka 2000 walichofanyiwa CUF na serikali ya Mkapa, kama ni utekaji tumewaona walichofanyiwa akina dkt. Ulimboka kipindi Cha Kikwete, kama ni rushwa, ufisadi na wizi ni utamaduni uliokomaa ambao Wengi tumezaliwa tumeukuta.
Kwa hiyo kumbe hapa issue sio Fulani Wala nani, issue hapa ni wanainchi wenyewe
Kuendelea kulaumu wafu kwamba wao ndio waanzilishi wa hiki na hiki Kwa suala ambalo liko ndani ya uwezo wenu wanainchi wenyewe ni uwendowazimu wa Hali ya juu kabisa na kwa namna nyingine ni kutoa freedom of accountability kwa serikali iliyopo madarakani.
Binafsi Mimi hili taifa huwa naliona ni la wendowazimu, yaani raia wake hawana akili timamu na uthibitusho ni pamoja na mada kama hii.