Ninaandika ili iwe kumbukumbu kwa vizazi vilivyopo kwamba.
Mwaka 2020 utaweka historia ya vilio na majonzi kwa watu wa kada zote
Uwe Ccm, uwe chadema, uwe hauna chama, watoto, vijana wazee, wake kwa waume hakika ni mwaka wa majonzi.
Uwe mwanasiasa, uwe mfanyabiashara, uwe mkulima uwe mfanyakazi wa serikali au private mwaka huu utakugusa tu kwa namna yeyote.
Ndio mwaka utakaotawaliwa na siasa chafu kuliko kipindi chochote toka tupate uhuru naomba Mungu angalau atuepushe.
Naomba ili chapisho liwe kumbukubu kwa watu wa kada zote tuweze kuchukua hatua kuzuia machafuko kwa namna yeyote ile ili tuendelee kuwa kisiwa cha amani yajayo hayafurahishi hata kidogo.
Happy New Year 2020
Mungu Ibariki Tanzania.