2021 AFCON Special Thread

2021 AFCON Special Thread

Mashabiki wa Cameroon waliojitokeza kwa wingi uwanjani wamejikuta wakiishabikia Senegal😂
Senegal inaonewa huruma sana...maana mzimu wa kufungwa fainali unawatesa.

Ila wanavyopoteza nafasi muhimu wanatupa wasiwasi
 
Hii fainali itakuwa tuu kama Simba vs Mbeya kwanza,Misri watazuia wee lakini watatobolewa..

Kipindi cha kwanza Misri huwa wanacheza hovyo Sana kama tuu mechi na Cameron
 
Michuano ya Afcon imefika, ni hapo kesho ndio inatarajiwa kuzinduliwa. Itafanyika kuanzia kesho Januari 9 mpaka Februari 6 mwaka huu.

Michuano hii ilibidi ifanyike mwaka jana 2021 ila kwasababu ya Covid-19 ikahairishwa. Hivyo inafanyika mwaka huu ila ina jina la mwaka jana.

Mwenyeji wa michuano hii ni Cameroon, huku Algeria akiwa ni bingwa mtetezi!

Jumla ya timu 24 zitapambana kutafuta bingwa mpya katika michuano itakayifanyika katika majiji matano yenye viwanja sita ndani ya Cameroon.

Mechi hizo zitakuwa live kupitia ving'amuzi vya Azam, Dstv, Star times, Canal.
Wale wadau wa kustream basi pitieni hesgoal.com

Hivyo, kwa updates zote za michuano hiyo utakuwa unazipata kwenye uzi huu karibu sana mwanamichezo!
Mwenye kombe lake ndo anachukua
 
Barbara akiwa uwanjani

132AC36F-AC24-46C1-BF61-0EF2CB2A30EA.jpeg
 
Back
Top Bottom