2021 AFCON Special Thread

2021 AFCON Special Thread

URAIA PACHA unasaidia sana, we chunguza, nchi nying wameruhusu uraia pacha, wanapata wachezaji wengi, mfano equatorial quinea wachezaji karibia 17 wote wamezaliwa Spain, unategemea nn, nchi yetu imebadili mifumo ya kizaman imepitwa na wakat,

Kumbe ni wa spain! Ina maana yule aliechukua man of the match ni mhispaniola?
 
URAIA PACHA unasaidia sana, we chunguza, nchi nying wameruhusu uraia pacha, wanapata wachezaji wengi, mfano equatorial quinea wachezaji karibia 17 wote wamezaliwa Spain, unategemea nn, nchi yetu imebadili mifumo ya kizaman imepitwa na wakat,

Uraia pacha unasaidia mno kaka
 
Tuna ligi mbovu, ushabiki mkubwa kwa timu zenye viwango duni kulinganisha na timu za nje, tuna majungu, nepotism, tunajali matumbo yetu, wachezaji wetu kuwa na miili midogo, physique ndogo, stamina dhaifu, vimo vifupi, makocha viwango duni, tunaabudu ushirikina. pamoja na lishe duni (ongeza mambo mengine yenye kikwazo) Kwa mwenendo huo usitegemee tutafua dafu mbele ya wenzetu.

Equatorial Guinea, Gambia, Gabon, Siera Leone ni vi-nchi vidogo lakini wazuri kwenye soka katika mashindano haya.

Mpira sasa ume-shift kutoka Afrika Kaskazini kwenda Afrika Magharibi.

Timu zetu zitabaki kutambiana na kufurukuta humu ndani tu, zikienda nje zinafyekelewa mbali.

Tukiondoa hayo matatizo niliyoyataja na utakayoyataja, tutasonga mbele kisoka na kuleta ushindani. Vinginevyo tutakuwa wasindikizaji tu.

Hata hawa wachezaji wageni wanaosajiliwa na timu zetu, viwango vyao vya uchezaji ni duni, mfano mwamba wa Lusaka (CCC). Amerudi Simba baada ya kiwango chake kuonekana duni, ilitakiwa asirudi Simba kwa sababu wachezaji wetu wazawa hakuna la kujifunza kwa huyo jamaa, lakini ndio hivyo tena.

Wasajiliwe wachezaji na makocha wenye viwango ili kuinua timu zetu kuweza kushindana na timu za nje.

Kwa mtindo huu, hata mabilioni ya fedha yawekezwe, kutoboa itakuwa ni ndoto za alinacha.

Ngoja nipooze koo kwa ulanzi kabla sijaendelea kusema.
Ligi ya Tanzania ni ya 8 Afrika kwa ubora.
 
Sana siyo kidogo, sisi viongozi wetu wameng'ang'ania mawazo ya kiprimitive tu, tunatakiwa tubadilike sana

Kweli kabisa, Uraia pacha ni muhimu mno kamanda....kama wataruhusu watakuja kuyaona matunda yake....kwa sasa Tanzania ni mojawapo ya nchi kumi katika Afrika ambazo bado haziruhusu uraia pacha, na huenda sasa zimebaki sita, kama Ethiopia na Cameroon wamesharuhusu. Kati ya nchi 54 za Afrika, 44 zimeruhusu uraia, na kama ina utata wasingeruhusu nchi zote hizo , washaona ina faida mno na ndio maana nchi zao zimeendelea....wenzetu waliona mbali...
 
Kabisa, viongozi wetu ni waoga kifikra, sijui uko wanakoenda kwenye ziara nchi nyingne hawajifunzi? Au kukosa exposure
 
Cameroon na Burkina Faso wamefuzu kwa hatua ya 16 bora

A77944C7-B887-443B-8C73-56324AA714A7.jpeg
 
Back
Top Bottom