Tuna ligi mbovu, ushabiki mkubwa kwa timu zenye viwango duni kulinganisha na timu za nje, tuna majungu, nepotism, tunajali matumbo yetu, wachezaji wetu kuwa na miili midogo, physique ndogo, stamina dhaifu, vimo vifupi, makocha viwango duni, tunaabudu ushirikina. pamoja na lishe duni (ongeza mambo mengine yenye kikwazo) Kwa mwenendo huo usitegemee tutafua dafu mbele ya wenzetu.
Equatorial Guinea, Gambia, Gabon, Siera Leone ni vi-nchi vidogo lakini wazuri kwenye soka katika mashindano haya.
Mpira sasa ume-shift kutoka Afrika Kaskazini kwenda Afrika Magharibi.
Timu zetu zitabaki kutambiana na kufurukuta humu ndani tu, zikienda nje zinafyekelewa mbali.
Tukiondoa hayo matatizo niliyoyataja na utakayoyataja, tutasonga mbele kisoka na kuleta ushindani. Vinginevyo tutakuwa wasindikizaji tu.
Hata hawa wachezaji wageni wanaosajiliwa na timu zetu, viwango vyao vya uchezaji ni duni, mfano mwamba wa Lusaka (CCC). Amerudi Simba baada ya kiwango chake kuonekana duni, ilitakiwa asirudi Simba kwa sababu wachezaji wetu wazawa hakuna la kujifunza kwa huyo jamaa, lakini ndio hivyo tena.
Wasajiliwe wachezaji na makocha wenye viwango ili kuinua timu zetu kuweza kushindana na timu za nje.
Kwa mtindo huu, hata mabilioni ya fedha yawekezwe, kutoboa itakuwa ni ndoto za alinacha.
Ngoja nipooze koo kwa ulanzi kabla sijaendelea kusema.