NetMaster
JF-Expert Member
- Sep 12, 2022
- 1,454
- 4,925
Zingatio 1: Simo katika kabila lolote kwenye hii orodha, sina mgongano wa kimaslahi wa kunifanya kupendelea ama kuchukia makabila niliyotaja.
zingatio 2: kuwa ndani ya haya makabila haimaanishi watu wote wa kabila hilo wafanikiwa, hata idadi ya wenye mafanikio makubwa ndani ya haya makabila bado ni ndogo, usibweteke kujidanganya umefanikiwa kisa umo ndani ya haya makabila, Tafuta chako!!
Muhimu 3: kama kabila halipo haimaanishi halina watu waliofanikiwa, kuna watu wa makabila ambayo hayamo humu wana mafanikio makubwa kuzidi watu kibao wa makabila yaliyowekwa hapa.
Muhimu 4: hakuna muhuri wa kudumu wa umasikini ama maendeleo kwenye haya makabila, kuna kupanda na kushuka, kuna makabila yalikuwa chini zamani ila kwa sasa yanakuja kwa spidi ya radi, mengine yameshuka.
1. Wachaga -
🎯Biashara
🎯Elimu
🎯Siasa
🎯Kubebana
🎯Kuendeleza kwao
Kibiashara kabila hili wapo katika nafasi nzuri, wamekuwa pioneers wakubwa katika kuanzisha na kuziendeleza biashara kibao, mifano ya biashara maarufu kuna kampuni ya ndege za Precision Airways, Hamidu city sehemu ya makazi yenye nyumba elf 2 za kisasa, hotel kali za Arusha / Dar, n.k. Icon kubwa katika kabila hili ni Marehemu Mzee Reginald Mengi, aliweza kuingia ndani ya orodha ya top 10 ya matajiri wa hapa nchini akiwa ni mtanzania pekee mwenye asili ya makabila ya hapa kwetu, kwenye elimu nako hakuwa nyuma, alikuwa muhasibu wa kwanza nchini kuthibitishwa na bodi ya wahasibu na wakaguzi wa hesabu za fedha (CPA), aliweza kutumikia sehemu mbali mbali zilizompa mishahara minono lakini aliamua kugeukia ujasiriamali uliompa utajiri mkubwa.
Kielimu wamejitosheleza, mkoa wanaotokea unaongoza kwa kuwa na shule nyingi tangu zamani hadi sasa, kupata elimu ni kitu rahisi, maofisini katika kila watumishi 10 imeshazoeleka kumkuta mchaga walau mmoja na hii idadi imepunguzwa sana, miaka ya nyuma maofisin kulijaa wachaga na makabila machache yasiyozidi matatu yaliyokuwa na wasomi hususan wahaya. sikuhizi hali ni tofauti, elimu imesambaa kwenye makabila mengi na mbaya zaidi wasomi ni wengi kuzidi ajira kiasi kwamba nafasi 1 inagombaniwa na watu 500, pia wizara ndio inasimamia zoezi la ajira sio kama zamani kila shirika / taasisi ilijisiamia kwenye kuajiri, bosi akiwa mchaga anarundika ndugu zake. Uzuri ni kwamba wachaga hawategemei ajira pekee, huwa kuna mlango mwengine wa kufanya biashara, inakuwa rahisi kwao kuanza biashara maana wana utamaduni wa kubebana kwa kuchangiana mitaji na kwavile kunakuwa na ndugu wanaofanya biashara huwa inakuwa rahisi kushikwa mkono kupewa ramani, ushauri na connections za biashara.
Kisiasa wapo active na sijaona wa kuwakaraibia, vyama vikuu vya upinzani vilivhowahi kuleta upinzani mkali kuanzia Tlp, Nccr na Chadema vimeanzia huko kwao, wamo pia kwenye chama kikuu cha ccm na influence yao ya political power si haba.
Kubebana na kusaidiana ni silaha kubwa sana katika maendeleo yao, mmoja akitoboa anasaidia wengine.
Hawasahau kuendeleza walikotoka, wanajenga na kuboresha makwao huko kwenye asili yao, hata ikitokea misiba au wakirudi kusalimia huwa hapati shida kwenye makazi. Kuna nyumba ya Marehemu mzee Mengi aliijenga kwao ni mfano wa mansion za kisasa.
kila mwisho wa mwaka kabila zima huwa wanarudi makwao kwa pamoja, ni utamaduni wa kipekee, kukutana huku husaidia ndugu waliotawanyika kukutana, ndugu kuchangiana mitaji, ndugu na majirani kujuliana hali, kupanga mikakati, kutambulisha watoto kwa ndugu, n.k. kurudi inakuwa rahisi maana makazi ya vijijini wanayaboresha.
mkoa wao ni wa pili kwa kiwango kidogo cha umasikini...
Niishie hapa maana ntaanza kuonekana nawapendelea lakini kila nilichoorodhesha hapa ni facts.
Wakinga -
🎯Biashara
🎯Kubebana
Kama ilivyo kwa wachaga, nao hawa kubebana na kusaidiana ni silaha kubwa sana katika maendeleo yao, idadi yao ni ndogo hawavuki milioni lakini wanabebana sana pengine kuzidi hata wachaga.
Hawa shabaha yao kuu ya mafanukio wameilenga sehemu moja kwenye biashara, kwenye elimu bado wanajikongoja lakini main focus wameweka kwenye biashara na kiukweli biashara zimebadili maisha yao.
Nchini China katika jiji la Ghuangzhou wakinga ndio watanzania waliojazana zaidi mpaka wana mitaa yao, ni jiji kubwa la kibiashara lenye viwanda vingi na kuna bandari kubwa ya kusafirisha mizigo, wakinga wa huko huwa wanashughulika na kutafuta bidhaa nzuri viwandani kisha wanasafirisha kwa meli ziwafikie ndugu zao wa huku, hata ikitokea kuna bidhaa kama kiatu kinauzwa sana hapa nchini basi kitasafirishwa kwa ndege kiwafikie ndugu zao wa huko wakipeleka kwa wachina watengeneze vingi na kuvisafirisha haraka vifike hapa kwetu wapige pesa, wana kampuni maarufu ya kusafirisha bidhaa kutoka China hadi hapa kwetu inaitwa Mapembelo Cargo, hilo neno Mapembelo ni salamu yao ya kilugha.
Silaha yao kubwa ni kuuza kwa bei ndogo, ndugu zao wa huko China wanahusika sana hapa kwa kupeana connection za machimbo ya huko China yenye bei za chini, kampuni ya kusfirisha bidhaa zao nayo inapunguza gharama, pia na wao hawanaga tamaa za faida kubwa nayo hii inasaidia sana gharama kuwa ndogo. hii mbinu ya kuuza kwa bei ndogo ndio iliwafanya hata wapemba na wachaga kupungua pale Kariakoo, ni ngumu kushindana na mtu anaeuza bidhaa hio hio au yenye ubora zaidi kwa bei chee, ni ngumu sana!
Mwamko wa biashara kwa wakinga wengi ulianza miaka ya 2000 lakini ndani ya muda mfupi maendeleo yao ni mithiri ya spidi ya radi.
Masoko waliyoteka ni soko la kuu la Kariakoo pamoja na mikoa ya nyanda za juu kusini. Kwa Dar wamejaa kwenye soko la Kariakoo ambalo ni soko mama na kubwa kuzidi yote nchini, wafanyabiashara wengi wenye maduka Dar, mikoani na wale wa nchi za Malawi, Zambia, Congo, Rwanda na Burundi wanajumua mizigo yao katika soko hili. Kariakoo si ajabu kwenye maduka 10 kuyakuta 6 yana wakinga, soko hili hapo zamani walijaa wachaga na wapemba hapa lakini kwa sasa hali ni tofauti, wakinga wamejazana na ndio wanaongoza kwa uwakilishi. Pia wanamiliki maghorofa mengi hapo Kariakoo.
Ukiachana na kariakoo, wameweza kuuteka kibiashara ukanda wa nyanda za juu kusini kwenye miji mikubwa ya mikoa ya Mbeya, Songwe, Iringa, Njombe, Ruvuma..
wenye chuki na wivu wa maendeleo hawakosekani, waliwahi kusambaza uchungu wao kwa wachaga kwa kuwaita ni majambazi na matapeli, hivi sasa wamehamia kwa wakinga kuwaita ni wachawi, yani kuna watu hawafurahii hata kidogo maendeleo ya wengine, naweza kusema hayo mambo hata kama yapo ni kwa wachache waliofanya maamuzi yao binafsi, na hata kama ingekuwa uchawi unategemewa basi kwanini waganga walioshika huu uchawi hali zao ni duni ? Kwanini makabila yanayosifika kwa uchawi hali zao ni duni, wanashindwaje kutumia matunguli yao waroge biashara ziwape maendeleo ?
Wapemba -
🎯Biashara
🎯Kubebana
Hawa nao kubebana na kusaidiana ni silaha kubwa sana katika maendeleo yao, kwa mara nyingine tunaona jinsi umoja ulivyo na nguvu
Kwenye swala la elimu huko Pemba wapo chini sana ni mkoa unashika namba ya mwisho miaka nenda rudi lakini kwenye biashara wapo mbali sana, mafanikio waliyonayo ni kuzidi hata ya wasomi wengi wanaopokea mishahara mirefu, connection walizonazo na ndugu zao waliojazana nchi za nje nyingi zinawabeba pia.
Wahaya -
🎯Elimu
katika swala la akili za darasani ni kama walizidishiwa 😂, mkoani kwao mazingira ya elimu yapo chini lakini bado wanafaulu, ilifikia kipindi serikali iliongeza alama za ufaulu kwa mkoa wa kagera maana watu walikuwa wanafaulu kama vile wanakunywa maji.
Elimu inawabeba na inawapa sifa za kuajiriwa sehemu nyingi,
Maofisini katika kila watumishi 10 si ajabu utamkuta mhaya angalau mmoja na hii idadi imepunguzwa sana, miaka ya nyuma ilishazoeleka maofisin kujaa wahaya na makabila machache yaliyokuwa na wasomi kama wachaga. Sikuhizi uwanja umebadilika kwasababu elimu imesambaa kuna shule nyingi za serikali + private, tuisheni, upatikanaji rahisi wa vitabu, ufaulu umekuwa mkubwa, n.k. hali hii imefanya kuwe na wasomi kibao karibu kila kabila, maofisini hata wamasai wapo. pia kwa sasa wizara ndio inasimamia zoezi la ajira sio kama zamani bosi wa shirika unamkuta ni mhaya au mchaga anarundika wenzake. ubaya ni kwamba wahaya wengi hawana mlango wa pili (plan b), wana uwezo mkubwa darasani wa kuwafanya wapate sifa za kujirika (zamani ilikuwa ni uhakika wa ajira) lakini sasa nje yah apo kujiongeza hata kwenye biashara ni wazito.
Kubebana bado wapo kiwango cha chini, naweza kusema kubebana kupo sana makabila ya kibiashara kwenye kuchangiana mitaji lakini huku kwengine sio kivile.
Wasukuma -
🎯Elimu
Wasukuma ndio kabila lenye watu wengi kwenye hii nchi, wapo takribani milioni 12, idadi yao ni kubwa sana na ilibidi iwabebe lakini tatizo lao kubwa ni kwamba wana ushirikiano mdogo, laiti wasukuma wangekuwa na muungano hakuna kabila lingewafikia hata nusu ya maenddeleo yao.
Any way kwa wasukuma bado idadi yao kubwa inawabeba, katika hii idadi kuna koo zimeelimika na kuliweka kabila kwenye ramani,
Pia hujishughulisha na shughuli za uchumbaji mdogo wa dhahabu na kilimo japo ni kiwango cha kawaida.
Kuzaliana kwa sana kumekuwa ni tatizo kubwa.