2022 Haya ndio makabila yanaongoza kwa maendeleo

2022 Haya ndio makabila yanaongoza kwa maendeleo

Hii mada haina kichwa wala miguu. Mleta mada hujui hata kutofautisha kati ya mfanya biashara na tajiri. Kuna watu wanaweza kuwa al-maarufu kwa biashara lakini wakawa si matajiri kwa kipimo cha utajiri.
 
Hii mada haina kichwa wala miguu. Mleta mada hujui hata kutofautisha kati ya mfanya biashara na tajiri. Kuna watu wanaweza kuwa al-maarufu kwa biashara lakini wakawa si matajiri kwa kipimo cha utajiri.
sawa tumekusikia mmakonde
 
Ngoja wapare na wasambaa wanakuja kukupinga.
Wapare hajawatendea haki kwenye post hii; na possibly kwenye swala la shule kwa sasa wanaweza kuwa ndiyo wanaoongoza; wanaweza kuwa wameshawapiku wahaya na wachagga.

Remaining number one is very difficult; becoming number one is easier than remaining number one!
 
Karne ya 21 kuzungumzia ukabila na kuushabikia ni kurudi nyuma. Makabila hayana maana yoyote kwa sasa katika ulimwengu huu.

Turudi kwenye mada. Dosari kubwa za mleta mada ni kuzungumzia maendeleo kabla ya kutoa tafsiri ya maendeleo. Kuna maendeleo ya kijamii (hii itaipimwa kwa ubora wa maisha kwenye eneo ambalo jamii husika inaishi) na kuna maendeleo ya mtu binafsi (hii utaipima kwa mtu mmoja mmoja).

Maendeleo ya jamii husika unaweza kuyapima kwa kuangalia hivi vitu.
1. Familia.
2. Ustaarabu.
3. Maisha.

Kwa mfano, kifamilia Katika hilo jamii za kabila la Kichaga ndio kinara. Mpaka leo hii mnyororo wa kimaendeleo kuanzia babu, watoto na wajukuu upo pale pale. Yaani unakuta babu alitoboa kimaisha, mtoto akatoboa na mjukuu akatoboa. Ama mjukuu aliyetoboa kimaisha atarejea kuendeleza jamii yake. Yaani haachwi mtu nyuma. Ni ngumu kukutana na mchaga asiyekuwa na connection ya moja kwa moja na ndugu zake. Kwa makabila mengi hilo jambo huwezi kulikuta kabisa.

Kama maendeleo ya jamii yatapimwa kwa kustaarabika, sote turejee vijijini kwetu tutazame bibi na babu zetu wanaishi vipi. Kuna makabila ukiwaambia kuwa na vyoo tu hiyo wanaiona ni anasa ya kuikuta mjini, hawana hata huo muda wa kuwaza kujenga choo bora, safi na salama. Kuna jamii mpaka leo zinaishi kwenye wingu la ushirikina au kutambika, wanarithi wake, wanaozesha mabinti wadogo nk. Wachaga pamoja na kuwa wamestaarabika kwenye mambo mengi lakini mpaka leo hii jamii nyingi za kichaga zinaendeleza matambiko huko uchagani tena kisiri. Hapo wameharibu ustaarabu! Kuna watu wa makabila mbalimbali wanaogopa kurudi kwao kijijini kusalimia au kujenga kwa woga wa kurogwa. Ni vipi utasema hilo kabila limeendelea.

Mwisho kijamii, maendeleo yatapimwa kimaisha (kula, kuvaa, kulala nk). Turudi vijijini kwetu, tuangalie watu wetu wanaishi vipi. Wanaishi kwenye nyumba zipi, wanakula nini, wanavaa nini?
 
Hao wakinga mbona walotoboa wachache sana na biashara zao ni mbao na mitumba tu wengi hawapo katika level za kumiliki makampuni kama walivyo wahaya wachaga na wahindi biashara za magenge ndo mnasema watu wametoboa
 
Unasumbuliwa na ego ya kabila badala ya kucheki facts.

Hivi kuna msukuma hata moja tu alieweza kuingia top 10 ya matajiri ya hapa Tz kama Mengi ?
Unaangalia mambo ya kale bila facts, angalia present ndugu, huyo mengi kuingia kwenye top 10 inamaanisha kila mchaga ni tajiri, endeleeni na ujinga wenu, na leta list ta top 10 ya sasa, nakushauri acha kukariri maisha, kama kusoma kwa sasa kila kabila watu wake wamepata elimu ya kutosha tu.
 
Wewe kabila lako lina maendeleo gani, au kuuza duka la rejareja naww unakuwa mfanyabiashara mkubwa, acha kushindana na msukuma kenge wewe, wakitoka wahindi na waarabu wanaofuata kwa ukwasi hapa Tanzania ila hawana kelele za kipimbi hakuna kabila lingine bali ni wasukuma.
Uko sawa wewe? Yaani wasukuma hawa hawa???? Aisee kwa maendeleo bora hata wanyaturu kuliko wasukuma
 
Ni kipi nimedanganya hapa ?

1. Mkoa wanaotoka wachaga hauongozi kwa shule nyingi ?
2. Mengi hakuwa tajiri pekee list ya top 10 mwenye asili ya Tz?
3. Mengi hakuwa muhasibu wa kwanza (CPA) hapa nchini ?
4. Wachaga sio kabila pekee wanalorudi pamoja kila mwisho wa mwaka?
5. Wachaga sio kabila linaloongoza kwa kuendeleza makwao ?
We una umri gani kwanza. Mambo unayozungumzia yameshapitwa na wakati. Kwanza yanakusaidia nini kama siyo umejaa ukabila? Umesahau uchagani ndio kuna ongoza kwa kwashiakor? Kunaongoza kwa aina nyingi za pombe ya kienyeji kiasi wanawake ndiyo wanaochimba mifereji? Je siyo uchagani wanaume wameshindwa kuhudumia wanawake zao kingono mpaka wanasaidiwa na wakenya kwa sababu ya ulevi?

Shule unazozungumzia ni zile zilizojengwa na taasisi za kizungu hasa za kidini na zikaja kutaifishwa na serikali na hatimaye walisoma watanzania wote siyo wachaga tu. Kwa leo Mikoa yote ina shule nyingi za sekondari na za msingi. Sasa hivi unakuta kata moja ina shule za sekondari mpaka 4. Kama kusoma sasa hivi makabila yote yamesoma acheni kudanganya watu wasiowafahamu.

Uchagani kuna umaskini hakuna mfano ndiyo maana kijana wa kichaga akimaliza tu shule iwe ya msingi au ya sekondari na ameshindwa kuendelea ni kukimbia kuelekea mikoa mingine kwa sababu uchagani hakukaliki. Mnaishi kama wakimbizi bado unajisifu eti mwisho wa mwaka mnarudi nyumbani mlikuwa wapi mwaka mzima? Kama kwenu ni kuzuri kumeendelea kitu gani kinawafanya msitulie kwenu? Msidanganye watu uchagani kugumu mi nakufahamu tena sana.

Unazungumzia kuendeleza kwenu, nikuulize ni wilaya gani ndani ya mkoa wa Kilimanjaro makao makuu yake yana hadhi hata ya halmashauri ya mji? Mkoa kama Tanga Korogwe ina Halamashauri 2 moja ya mji, una Halamashauri 2, wilaya ya Handeni ina Halmashauri 2 moja ya mji. Kilimanjaro Rombo ni ili ile, Hai ndiyo ina mji mdogo wa Bomang'ombe, Siha haina lolote, Same ndiyo hivyo tena imeshadoda, Mwanga huwezi kujua hata kama ni makao makuu ya Wilaya utafikiri kijiji. Sasa niambie huko mlikoendeleza miji yake inaitwaje?

Tatizo wachaga wengi mna matatizo ya afya ya akili kwasababu ya ugumu wa maisha. Mnapenda makuu kwa vitu vidogo sana, mnapenda sifa za kijinga tena za uwongo, mna ukabila, mnapenda sana ligi tena mnataka kushindana na makabila zaidi ya 120 ya Tanzania. Kwenu kuna umaskini hakuna rasilimali yoyote, hakuna ardhi kusema mlime, kwanza ni wavivu wa kulima mnapenda short cut muuze vifaa vya kichina, mfanye umachinga, mchome nyama, mpike supu, mkaange chipsi ndiyo kazi yenu.

Hakuna bahari wala ziwa kwenu kusema mvue, hakuna ufugaji wowote mna uchumi gani?. Nyie mtaendelea kuishi kama wakimbizi ndani ya Tanzania. Mwezi wa 12 mnarudi kwenu kwenda kuwaonesha ndugu zenu mliowaacha mlichovuna mnavyopenda sifa. Kingine ni kwenda kuzikwa kwenu. Matajiri wa kichaga ni wachache sana kulinganisha ni population ya wachaga, wachache sana. Acheni show off na sifa za kijinga, sifa ya tajiri wa kweli ni siri hapendi kujionesha, ni maskini tu ndio hupenda kujionesha na kujisifu ndiyo sifa yenu.
 
Wachaga pamoja na kuwa wamestaarabika kwenye mambo mengi lakini mpaka leo hii jamii nyingi za kichaga zinaendeleza matambiko huko uchagani tena kisir
Kwani kutambika Kuna kosa lipo hapo ?

Kuna kabila lipo ambalo halitambiki ??


Mila na desturi ziheshimiwe.

Pia ujue kutofautisha uchawi na Mila, hata Magufuli alizikwa Kwa mila zao hatuwezi kusema huo ni uchawi
 
We umelewa siyo bure na yale mapori ya kwenu yanamsubiri nani
Huku kuna pori gani? Msukuma anaanzisha miji, na ameanzisha miji mingi hapa Tanzania, na kwa taarifa yako sehemu yoyote yenye rutuba hapa Tanzania msukuma huwa hakosi ata kidogo, hakuna watu wanaonusa fursa haraka na wana macho ya mwewe kama wasukuma, kaa na uzwazwa wako😝😝😝😝😝
 
Disclaimer: Mimi wala sio mtu wa kabila lolote katika haya wala sina undugu nao, facts be facts,

Wachaga - Ni kabila la pili kwa idadi ya watu wengi na hii idadi yao wanaitumia vizuri katika maendeleo kwa kusaidina / kubebana kwenye kuinuana kibiashara kwa kuchangiana mitaji...

Wewe ni mchagga sio? Ukaamua kujiweka no 1
 
Kwani kutambika Kuna kosa lipo hapo ?

Kuna kabila lipo ambalo halitambiki ??


Mila na desturi ziheshimiwe.

Pia ujue kutofautisha uchawi na Mila, hata Magufuli alizikwa Kwa mila zao hatuwezi kusema huo ni uchawi
Nadhani hujanisoma na kunielewa.

Kabla ya kuelezea maendeleo ni muhimu kuweka tafsiri. Tafsiri yangu niliyoweka hapa kuhusu maendeleo inajumuisha na suala la kustaarabika. Katika mazingira ya jamii (kabila) iliyofikiwa ipasavyo na elimu, sayansi, teknologia na imani za kidini (Ukristo na Uislamu) halafu bado jamii hiyo ikaendelea kutambika, maana yake (inachukuliwa kuwa) bado haijastaarabika, na iko nyuma kimaendeleo. Na kwa hapa Tanzania, kabila lolote linaendekeza imani za matambiko (ushirikina) linatafsiriwa kuwa halijaendelea! Na karibu kila mtu hapa anaona hivyo.

Tuje sasa kwa kabila la wachaga. Kwa jinsi kabila la wachaga walivyofikiwa ipasavyo na Elimu, Sayansi, Teknologia na Imani za kidini, usingetegemea kama na wao bado wanatambika (wanaloga!). Na karibu wachaga wote huku mijini ukiwauliza kama wanaamini mafanikio yao ni sehemu ya matokeo ya wao kutambika (kuloga) watasema hapana, wanakana wao kufanya hivyo vitu, lakini kisiri wakiwa huko uchagani wanatambika (wanaloga!)

Hitimisho langu ni kuwa, jamii inayoamini katika kutatua matatizo yake kwa njia za kisasa au kisayansi kuliko kuamini kwenye imani za kale (kutambika/kuloga) basi hiyo jamii itakuwa imepiga hatua kubwa kimaendeleo.
 
Back
Top Bottom