Ngurukia
JF-Expert Member
- Feb 25, 2023
- 4,407
- 16,942
Paraghraph zako 2 za kwanza zilinifanya nifikiri ni chawa kazini ila mpaka mwisho wa comment yako nimekuelewa mno.Mamlaka ya kiti cha uraisi yanapaswa yawe na Uungu ndani yake, katika Uungu hakuna kingine kilichojaa zaidi ya UPENDO (Agape).
Jinsi UPENDO wa Rais Samia unavyopoa ndivyo jinsi mamlaka aliyopewa na aliyonayo yanapoa pia.
Wamasai hawajazaliwa Ngorongoro kwa bahati mbaya na waarabu wa Dubai, Oman hawajazaliwa uarabuni kwa bahati mbaya.
Rais Samia anapaswa kutafakari yeye binafsi na kujifanyia tathmini akiona vipi asisubiri kama mbwai iwe mbwai bora astaafu zake kwa heshima 2025 arudi zake Kizimkazi tutaendelea kumpenda na kumuheshimu.
Tutaendelea 'kumpenda' akiwa mstaafu ila kwa sasa kama raisi inatosha kwa kweli. Samia akapumzike tu.