2025 ili ukubalike kwa haraka, italazimu Tundu Lissu kulitaja jina la JPM kuomba kura kwa Wananchi

2025 ili ukubalike kwa haraka, italazimu Tundu Lissu kulitaja jina la JPM kuomba kura kwa Wananchi

Pslmp

JF-Expert Member
Joined
Mar 18, 2021
Posts
1,622
Reaction score
2,458
Amini usiamini ndivyo itakavyokuwa,

Kama ambavyo imekuwa karibu Kila mara Jina la Hayati Mwl JKN kuwa ndio dira na mfano Bora Kwa kila kiongozi kuombea Kura hata kurejea hotuba zake Ili kujijenga kisiasa.

Kwa kadri siku zinavyosonga na vizazi vingi kwa sasa Kwa sababu ya kukosekana somo la historia kujua historia za viongozi wao, wapo ambao ukuwatajia Jina la Hayati Mwl Nyerere unaweza ukajikuta unaulizwa kuwa ni Nani huyo na Yuko wapi?

Kwa sababu hiyo, kizazi cha sasa huwezi kukitenganisha na viongozi ambao kimekuwa kikiona kazi zao, na kikawaida yetu kama binadamu, tunaamini Kwa kuona, Kwa kazi ambazo zinaonekana ambazo zimefanywa Kwa awamu hii, zinawafanya Watanzania kuamini kuwa, kumbe inawezekana kukiwepo viongozi wachapa kazi, viongozi wasio na uhusiano na mafisadi, na ndiyo Maana nampongeza Hayati Dkt JPM kukazia somo la historia lirejeshwe mashuleni.

Nachotaka kusema hapa ni kwamba, 2025 nina uhakika kwamba, mwanasiasa yeyote awe wa upinzani na hata CCM, kama atataka kujizolea umarufu na hata kukubalika mapema kwa jamii, itamlazimu kurejea utendaji kazi wa Hayati JPM, hatakii!!! wananchi hawatamwelewa, Kwa sababu hiyo, Mh Tundu lissu, itamlazimu aombe Kura huku akirejea utendaji wa JPM na Jina la JPM kuombea Kura.

Kwa muda mfupi, Hayati Dkt JPM, karibu Kila mtu amejikuta akikubali kazi zake, Uongozi wake, uchapakazi wake na wengine wanaenda mbali kusema! Hakujawahi Kutokea kiongozi Bora kama huyu hapa Tanzania.

Mwenye macho asikie na mwenye masikio aone.
 
Kwamba amtaje mtu aliyevuruga bei ya sukari
Bei ya mbaazi
Bei ya mafuta
Bei ya korosho

Sio mbaya hayo ni mawazo yako inabidi tuyaheshimu
Inawezekana kuwa ni kweli, lkn haya ni sehemu ndooogo Sana Kati ya makubwa mengi mazuri aliyofanya huyu Jembe
 
Hadi muda huu nyie msiojitambua mnaonekana mmeshinda!. Subirini tumzike halafu tunaojielewa tuanze kufunguka, muone uchafu wa huyo jamaa yenu, mtayajua na yaliyofichwa
Sidhani, na hata kama ikiwa, haitasaidia mkuu, ukiwa unayasema hayo madhaifu, jihoji pia wewe, umekamilika asilimia zote mkuu?
 
Magufuli alikua wa CCM ameondoka kimwili lakini kifikra anaishi ndani ya mioyo ya Watanzania, na CCM imara pamoja na serikali makini alivyojenga bado ipo chini ya uongozi makini aliouacha wa Rais Samia Suluhu Hassan 😍🇹🇿🔥



Hongera sana kwa CCM hakika wa kuwaondoa marakani atafute kitanda alale tuu maana atasubiri karne

Mungu ibariki Tanzania Mungu mbariki rais wetu Samia Suluhu Hassan 🇹🇿😍🔥

Apumzike kwa amani Dr John Pombe Joseph Magufuli 💔🙏
 
Siku zote uongo hutumia lift kwenda juu bali ukweli hutumia ngazi kwenda juu. Hatimae ukweli hutamalaki na kuushinda uongo.Ni jambo la muda tu,
 
Magufuli kwa sasa ndio SI Unit ya maendeleo na uongozi wenye kugusa maisha ya watu.

Chadema mnavyoendelea kujaribu kupambana nae ndio watu wanaendelea kuwapuuza.

Lowassa alishawai washauri achaneni na harakati fanyeni siasa za kistaarabu, mkamuona hamnazo. Haya endeleeni kupambana na Magufuli mtakiona cha moto.
 
Ni kweli JPM kafanya mengi Tanzania but remember magazeti mengi if not yote yalikua yanaandika habari za upande mmoja tu; zote/nyingi zilikua za KUSIFIA tu, hakukua na kukosoa au kwa maneno mengine hatukua tunapewa habari za upande wa pili kumuhusu mhe; kwasasa huenda hakuna litakalo zuia kuandikwa habari HASI, huenda waandishi wakaweka na ushahidi wa yale wanayo yaandika. ni mapema sana sasa hivi kuzungumzia uchaguzi wa 2025; tusubiri mkuu.
 
Huyu mtu atasahaulika haraka sana kwasababu anapewa sifa za kulazimisha kwa kutumia nguvu ya media.
Hahaha!!

Kama kuna watu bado wanakumbuka Lichimondi sidhani huyu mwanzilishi wa SGR nchini asahaulike, mjenzi wa Kota Magomeni na wananchi wakae bule, mjenzi wa vituo vya Afya asahaulike mapema

Wa kusahaulika ni wewe, usipoonekana hapa siku tano tu ndio basi tena
 
Back
Top Bottom