20M inatosha kuhamia Dar kuanza Maisha na Biashara?

We jamaa unaonekana unaskiliza sana stori za vijiweni
Na zimekuharibu
 
Fala kweli huyu aisee!
 
Changamoto ni kwamba kama unaenda kuanza biashara au mishe mpya ambayo hujawahi fanya hapo hutatoboa. All in all kafanye kitu ulicho na utaalam nacho au uzoefu, usijerogwa ukaambiwa kitu fulani kinalipa ukajichanganya. Note: Usitupie mapene yote..anza hata na robo yake
 
We jamaa bonge la kiazi
 
Ngoja kwanza una familia...!? Yaani mke watoto n.k au upo single?

Kwanza, Kama una familia njoo Dar chukua chumba na sebule. Kama upo single chukua chumba kimoja hakikisha ni kina choo bafu ndani (master)

Pili, nenda sokoni Mabibo, kariakoo, jifunze biashara zifuatazo Viazi vya chipsi, Ndizi, vitunguu, miwa,machungwa n.k jifunze watu wanavyo fanya hizo biashara A-Z hakikisha unafahamu vyema kuhusu hizo biashara. Tumia muda wa kutosha kujifunza hata wiki 2 sawa tu.

Tatu, funga safari mpaka mkoa unao zalisha sana bidhaa moja wapo kati ya hizo ulizo jifunza nunua chukua fuso lako peleka sokoni anza kuuza bidhaa yako. Ukimaliza una rudi tena shamba hata kama kuna muda utapata hasara ila jua kwamba kila mwisho wa mwezi hauwezi kukosa faida ya 2/3 M's itategemea na soko mwezi husika limeendaje.

Angalizo usiweke mtaji wote kwenye biashara hii una weza kuanza hii biashara kwa 13M's huku bank account yako ikiwa na reserve ya 7M's. Mwombe Mungu sana azidi kukufungulia milango ya baraka, focus kwenye kazi yako mambo yasiyo ya muhimu kwako na kwa familia yako ya puuze. Baada ya mwaka usipo kuwa na faida ya 50/70 M's mmh sijuiiiiii.
 
Kutosha au kutokutosha inategemea na vingi.
Mfano maisha unayotaka kuja kuishi huku dar, je pia plans zako zinafanyika kivitendo maana kuna wengine wana plans kwenye vitendo ni ngumu.

Hiyo pesa inawezekana kabisa kuanzia life na mengine yakaenda, ila kwanini dar, hakuna sehemu ukafanya jambo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…