Ukitaka kuagiza, agiza popote, kodi ya TRA haiangalii nchi inayotoka, kodi ni ile ile isipokua tu kama unaagiza South Africa na unataka unafuu wa kodi basi gari lazima iwe brand new, hapo kodi itakua kidogo sana. Kwa maana nyingine hutalipa import duty kwa sababu ya mikataba ya SADC. Gari iwe mpya zero kilomita.
Nizungumzie Toyota Fortuner isiyozidi miaka 3, hapa CIF haipungui dollar 💰 40,000 sawa na tzs 100m hivi, jumla na kodi yake na makorokoro mengine andaa +- 120m hivi.
Matengenezo, gari za Toyota zinajulikana na kuaminika ulimwengu kote kwa kuwa na roho ya paka, kudumu muda mrefu na gharama kidogo za matengenezo.
Binafsi, I would Prefer Toyota Fortuner.
Tathmini na utafiti wa consumers report Duniani kote, Magari ya Land Rover kwenye category ya Reliability hua yanashika mkia.