4% ya mapato kwenda Zanzibar kama Hoja ya Muungano

4% ya ulichosema ni kwa ajili ya mambo ya Muungano.
Muungano ni gharama wala sio bra bra sijui nani anachangia nini wapi na lini.
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni nchi moja, kama ambavyo fedha zinatolewa Kigoma /Mbeya zinakwenda Singida /Kilimanjaro & kinyume yake ndivyo ambavyo zinatakiwa zipelekwe Pemba /Unguja.
Maendeleo ni kwa ajili wote ndani ya JMT.
Zanzibar ni muhimu kuliko tunavyodhani, ukitaka kujua umuhimu huo ebu ishi Mikoa ya Pwani walau kwa miaka 10.
 
Unauliza juu ya marais waliopita kutolishughulikia hilo, napenda kukukumbusha tu kuwa kinachoitwa KERO ZA MUUNGANO zipo toka wakati wa Nyerere. Ni nyingi kimsingi ikiwa pamoja na hilo, marais wengine walilifumbia macho.

Ukiliona hilo ni gumu kwako au kwa Tanzania bara kuna suluhisho jingine. Nalo ni kuwaitoa wizara ya fedha kutokuwa ya muungano kama zilivyokuwa baadhi ya wizara. Hii itaiwezesha Zzibar kutafuta mapato yao wenyewe ikiwa pamoja na kukopa nje, misaada na hata kutafuta washirika wa kibiashara ndani na nje.

Mwisho hivi katika miradi mikubwa (SGR, BOMBA LA MAFUTA, Umeme, Fly over , mwendo kasi) aliyokuwa anaifanya Hayati Magu, ni mradi gani mkubwa aliufanya kule Zanzibar?
 
We fala kweli yani vipindi vyote huoni kama Rais wa muungano wa bara anatawala Zanzibar .. acha roho mbaya wewe dogo Rais wa zanzibar ni kama boya tu Rais wa Jamhuri wa Mungano wa Tanzania ni anajulikana duniani kichwa panzi wee.
 
Mkuu, mbona hii ni simple. Ni kama vile ambavo dhabu na gesi ya Tanganyika haiwahusu wazanzibari.

Haiwahusu wakati wanataka wagawiwe 4% ya chenchi ya matumizi ya Muungano? Dhahabu na gesi havina chenji kwenye matumizi ya Muungano?
 

Orodhesha hayo maeneo machache ni kama yapi tuyajue
 

Mkuu umefika Zanzibar? umeona wabara waliokuepo Zanzibar? 80% ya wafanykazi wa mahoteli ni wabara. sasa hiyo hoja ya kuwa wazanzibar bara wapo wengi haina mashiko, mana hata Zanzibar wabara wapo wengi
 
Wanafaidika kwa kipi? kwa makampuni kufanya kazi zao bila ya kulipa kodi?
 
Mi naona kuweka vitu simple Zanzibar iwe na ZRA, iwe inakusanya mapato yenyewe ila shida sasa kwenye kugaramia shughuli za muungano itabidi Zanzibar ichangie. Au shughuli za muungano zipunguzwe zaidi ibaki moja tu ya Ulinzi.

Mkuu mapato ya nchi hayatokani na kodi za TRA tu, kuna na source nyengine za mapato katika nchi
 
kuna kipindi nilisikia wanalalamika kuwa ukiagiza bidhaa toka zenji, inakuwa imelipiwa ushuru zenji lakini ikifika dsm inalipiwa tena. ina maana kule wana ushuru wa kikwao na wana makusanyo ya pesa ya kikwao.

Iko hivi mfano umennua Tv Zanzibar inch 38 kwa 300,000/= ile Tv unalipa usafiri kwenye boat 15,000/= unalipia bandari 5,000/= unasafiri na TV yako ZRB office pale Babdarin Zanzibar hawakugusi ukishuka pale Ferry dar kuna office ya TRA wanapima mizigo na kupekua mikoba pale sasa unalipia 30,000/= kama freezer 50,000 kama kubwa laki moja the same kwa bidhaa nyengne zozote electronics na nyengne mfano kama bidhaa za nyumbani zikizidi tano kwa items moja mfano umennua sufuria Zanzibar zikawa 5 kwa items hiyo hiyo ( sare) unalipa kodi haijalishi sio electronic na ukinnua kitu Tanganyika kikawa hivo pia unalipa kodi Zanzibar ukifka tu bandarin hakuna kitu utannua bila kulipa kodi
 
Wewe unaambiwa Zanzibar wamechangia zaidi ya 60% mchango wa kuanzishwa BOT halafu unasema 4% zanzibar kwa nini wakati Zanzibar ata 50% bado Tanganyika itakuwa wanaionea Zanzibar.,

Halafu Tanganyika wanajisahau sana kwenye hili wanaangalia idadi ya watu wakati Tanganyika walipoungana na zanzibar waliungana kama nchi na nchi.
 
Hizi zilipendwa mkuu!
 
Kila nchi iwe na mapato yake. Almasi ya Mwadui iende kuwanufaisha Shinyanga na Tanganyika full stop... Hao sijui ndugu zetu Wazanzibari wakae na miradi yao... Eti Sato na Sangara wa Mwanza waende kupeleka maendeleo Pemba [emoji15] Hakuna hicho kitu....
 
Kumbuka kuwa yeye mwenyewe ni Mzenji,kwa hiyo usishangae hiyo asilimia 4 ikapanda ikafika hata 40%.Mimi nomeshaona dalili za kuibeba Zanzibar kwa mbeleko ya chuma.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…