7/7 ni 'miscalculation' ya wanaharakati, itafeli na kuishia kuwadhoofisha

We hata elimu ulikosa kuhusu walijitolea wakafa kwa ajili ya ujinga wako ukaishi na uhuru na kutumia vitu ambavyo unaweka emoji kumbe vyao tokea mpaka leo.
Mkuu jukwaa huru hili,, ulitaka kulazimisha kila mtu akaandamane??
Hakuna sehemu maandamano yaliletaha Suluhu zaidi kufanya hali kuwa mbaya zaidi. Shida umeishi bongo, na haujui kitu kuhusu Mifumo ya watu.
 
Wewe ni katika wale wapiga debe na waokota makopo au wamachinga?
Tutaona na kusikia mengi lakini waombolezaji siyo WAJINGA kama mnavyoaminishwa hapo lumumba
 
Inaleta tofauti ipi?
kwani lengo la kuandamana ni kuonekana na wazungu?
 
Kwani alliyekutuma uje kwa namna hii hakuona wengine ambao wangekuja kivingine?
 
Wewe ni katika wale wapiga debe na waokota makopo au wamachinga?
Tutaona na kusikia mengi lakini waombolezaji siyo WAJINGA kama mnavyoaminishwa hapo lumumba
Ni kweli watu wanavidonda moyoni, lakini hawatoandamana kama ambavyo hawakuandamana ile 9 December!

Lilikuwa kosa la kimkakati kuitisha yale maandamano ya December na ni kosa zaidi kuitisha hayo. Itadhoofisha sana harakati zao.
 
Wewe una akili ndogo sana, unadhani kwa akili zako watu wote ni wajinga kama wewe. Fungua akili uone mbele, wewe unaona tarehe 7/7 tu
Iko hivi, ukimtishia mtu basi hakikisha unao uwezo wa kutekeleza vitisho vyako kama asipokusikiliza.

Ukitoa vitisho alafu ukashindwa ku follow through inakudhoofisha!

Kosa hilo hata kaka yake Polepole amelifanya mara kadhaa.

Sasa kama unaitisha maandamano wakati unaona kabisa 'atmosphere hairuhusu' kisha yanafeli unadhani watesi wako wanapata picha gani??
 
Tunataka nch yetu tunataka nch yetu
 
Hiyo paragraph yako ya mwisho ndiyo inaonesha huelewi siasa na harakati za Tz. Nikuambie tu hayo maandamano yameivuruga serikali kuliko unavyo dhani. Kwahiyo unadhani wanao organize hayo maandamano hawajui kama yatafanikiwa au laah? Sasa hivi watu wanaenda kwa mahesabu.
Usidhani serikali inapuuzia hayo maandamano kama wewe unavyo puuzia, wewe unaona hayana impact ila nikuambie serikali ishaona hayo maandamano hata yasipokuwepo ni tatizo, tena wanataman yawepo ili wa react passive.
Mkuu huna hata D ya civics au uraia?
 
Dah, sijaeleweka vizuri.

Nilimaanisha hivi: ' katika hili tukio baya kabisa la mauaji na maandamano ya Oct 29, uliwaona watu wakijiandaa kuandamana kabla ya Trh 29' ?
Nimekuelewa! Hakukuwa na maandalizi rasmi, lakini watu wengi walikuwa na nia ya kuzuia uchaguzi. (No reforms no election).

Kwasasa ajenda kuu ni ipi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…