80% ya Wanawake Tanzania ni 'omba omba'

Hii dhana ya kumuhudumia mtu mzima mwenye akili na nguvu zake katika set up yoyote ile, iwe ndoa au mahusiano ndiyo aiingii akilini. Kwanini ahudumiwe, awe mke au mchepuko. Ndiyo mentality ya kuwa omba omba, mtegemezi na kupe. Mabepari hatutaki.
Haya ni maisha ya wanawake wengi wa mjini aisee. Sisi tuliokulia kijijini hakuna kukaa home tu eti usubirie mume alete. Baba yangu alikuwa mwalimu na mama mfanyabiashara ya samaki. Weekend ilikuwa siku ya kwenda shamba.

Baba anatangulia na watoto wa kiume, mama anakuja baadae na chakula cha kula watu shambani. Mnalima jioni home. Siku za kazi baba shule mama kwenye biashara , mshahara wa baba ni wa kununua nguo na matumizi makubwa ya nyumbani, mala akirudi sokoni anarudi na mboga ,matunda kwa hela yake ya biashara. Sijawahi kuona wanawake wamekaaa tu .

Mpaka leo kila mmoja anacharika na ndoa zilidumu mpaka kifo. Tuwafunze watoto watu kuwajibika toka wakiwa wadogo, na waepuke kutumia sehemu zao zz siri kwa ajili ya kupewa kitu in return .
 
Hakika, haya ndio yalikuw maisha ya wazee wetu, mama zetu pamoja na kuwa walikuwa "mama wa nyumbani" lakini mchango wao katika familia ukikuwa mkubwa mno mno.
 
Mama yako ni mwanamke, dada zako ni wanawake... Wapo kwenye hii 80%.. ... Nadhani utafiti ulianzia hapo nyumbani !!!!
 
umenena yaliyo mema
 
Acha ku-justify udangaji
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…