Haya yote ni matokeo ya familia zisizokuwa stable kwa kipato. Unakuta baba hana hela na hasapoti familia mama hana uwezo na anachangamoto za kimaisha matokeo yake sasa wanaoathirika ni watoto sababu ya kukosa matunzo.
Sasa baba anaona kabisa ana mabinti katika uzao wake. Anatakiwa mapema aanza kuchapa kazi na kutafuta pesa kwa nguvu sababu hawa mabinti wakishavunja ungo then mahitaji yao ya kimwili huanza kuongezeka
Mtoto anataka pedi, anataka mafuta mazuri, anataka kutengeneza nywele, anatakuwa kula vizuri ili aendelee kunawili. Baba upo upo tu umejua kuwaleta ila sio kuwatunza.
Na hata kama baba hayupo, ni jukumu la wajomba, mashangazi, baba wakubwa na baba wadogo kutoa mahitaji ya hawa mabinti ili wasiende huko nje kudanga wakitafuta mahitaji.
Hii kitu mimi nimeiona sasa. Unakuta unatoka na kabinti, kanakuwa na shida mfululizo hadi unajiuliza haka katoto hakana akili sawa sawa au ni kachawi. Yaani shida za ajabu ajabu kumbe yote hii ni kukosa sapoti.
Sasa shida sio sasa, bali shida ni huko mbeleni uzuri ukishafifia hawa mabinti huwa wanakuwa katika hali ngumu sana kiuchumi na kifamilia. Maana wanakuwa pia wanawatoto na hawana means ya kipato isipokuwa kudanga. Sasa miili ikichoka nini kinafuata.
So ushauri wangu kama mwanajamii, hili swala tuanze kurejea misingi ya familia maana watoto wa kike nje ya familia hawana kinga yoyote hata wakiwa na kipato bado wanakuwa nachangamoto mbali mbali.
Kuwalinda jamii ianze kusimamia upya misingi ya kuwa na familia imara na bora zilizosimama na kuweza kuwalinda watoto wetu wa kike.
Ila tukiendelea hivi hali itakuwa mbaya sana miaka si mingi. Maana watoto wa kike wanazaa hovyo, wanatoa ujauzito hovyo, wana tangatanga na Kila mwanaume anaewapatia chochote kitu, magonjwa ya zinaa yaani fujo tupu.