Leo Tarehe 9 September, CEO mpya wa Apple
John Ternus (
amemreplace Tim Cook alieachia madaraka mwanzoni mwa huu mwezi), amezindua products mbalimbali za Apple kwenye event yao waliyoiita "Surprise and Shine"!
Event hiyo iliofanyika kwenye Steve Job's Theater, Apple Park California, USA, usikute wa leo saa 2 kwa masaa ya Africa Mashariki, imekuja na products za aina mbalimbali, kuanzia hardware na software, kama ifuatavyo:
1. iPhone Duo
Hii ndio talk of the street. Kwa mara ya kwanza Apple wameleta foldable phone (kama kitabu). Tofauti na wengi tulivyotegemea wataiita iPhone Ultra au Fold, wao wameona waiite iPhone Duo!
Better late than Never.
Hii Ina screen mbili za OLED, ya nje cover Ina ukubwa wa 5.5 inch, wakati ndani ukifungua ni 7.8 inch.
Ukiifunga Ina unene wa 9 mm, na ukifungua Ina unene wa 4.5 mm, ukiwa na frame ya titanium na aluminum.
Kwenye biometric, kama iPad Air, itakua na Touch ID ambayo ipo kwenye power button pembeni (Haina Face ID). Inakuja nyuma na camera mbili, Main ya 48 MP na Ultra Wide ya 48 MP, hamna camera ya tatu (macho matatu) ya telephoto. Na mbele, kwenye screen ya nje Kuna punch hole kwaajili ya selfie camera.
Imekuja na new cheap ya A20 Pro, 2nm, na unified memory ya 12 GB, na battery la 5,00 mAh.
Size zitakuja za 256 GB, 512 GB, 1TB na 2TB na Bei kuanzia $2,000 hadi $3,100 kutegemea na size. (Bei izo bila kodi, Wala usafiri Wala faida)!
2. iPhone 18 Pro na iPhone 18 Pro Max
Mwaka huu hamna iPhone 18 (plain). Iyo subirieni mwakani wakati wanazindua pamoja na iPhone Air 2 na iPhone 18e (peasants' iPhones)!
Kwa muonekano, iPhone 18 Pro na Pro Max ni kama iPhone 17 Pro na Pro Max, ila zina maboresho.
Zinakuja na screen ya 6.3 inch kwa Pro na 6.9 inch kwa Pro Max, zote OLED. Zote ziko powered na chip mpya ya A20 Pro. Pia camera Ile main sensor ya 48 MP Ina physical variable aperture (inamaana itakua inapunguza aperture kwa size kati ya f/1.4 na f/4.0, sio kutegemea software kama zamani).
Kwenye camera, iPhone 18 Pro Max pia amepewa Pro Max Zoom feature, kumruhusu kuzoom 10x (optical zoom), ukifananisha na 8x kwenye Pro.
Kwa mbele, Dynamic Island imepunguazwa ukubwa, na camera ya 24 MP imeboreshwa zaidi.
iPhone 18 Pro Ina battery za aina mbili, moja ya 4,300 mAh (eSIM only) na nyingine 4,000 mAh (yenye laini) wakati Pro Max nayo ivo ivo, 5,600 mAh kwa eSIM na 5,300 mAh yenye SIM card.
iPhone 18 Pro itakua na 12 GB RAM, na itauzwa kuanzia $1,200 hadi $1,900 wakati Pro Max atakua na 16 GB na Bei zitaanzia $1,300 hadi $2,000. Size zitakuja za 256 GB, 512 GB, 1 TB na 2 TB.
3. Apple Watch
John Ternus pia amezindua Apple Watch Series 12 na Apple Watch Ultra 4.
Zote ni maboresho kutoka kwenye model zilizotangulia, zikiwa na S11 chip ila kimuonekano zinafanana.
Apple Watch Series 12 sahivi inauwezo pia wa kurecord na kusummarize conversation yote, feature inaitwa Siri Recap.
Apple Watch pia zina feature mpya ya Health Age, ambayo inazijumlisha tests za VO₂ max, resting heart rate, HRV na ulalaji wako na kusema umri wako na matendo/mwenendo wako ni sahihi au.
Apple Watch Series 12 itaanzia $400 wakati Ultra 4 ukiwa $800.
4. AirPods 5
Kwa wapenzi wa music, AirPods 5 zimezinduliwa pia. Ziko powered na H3 chip, na amesema wameimprove mic, ANC (Active Noise Cancellation) na kukaa na chaji.
Pia, zimekua integrated na Health Sensors, kwahiyo itapa heart rate na workout wakati unasikiliza music.
5. Apple Home na Entertainment
HomePad na Apple TV 4K (Generation ya Nne) vimezinduliwa pia.
6. Software
Leo pia software zilizozinduliwa mapema iOS 27, watchOS 13, na homeOS zimeachiwa na kua available kwa Beta Tester na Developers.
Pre orders za products zote zitaanzia Tarehe 12 September, ila kwenye maduka zitakuwepo kuanzia Tarehe 18 September, kasoro iPhone Duo utaanza kuuzwa October.