A BITTER TRUTH: Kwanini watu weusi walishindwa kwenda Ulaya/Amerika (Ughaibuni) kuwachukua wazungu (Whites) kisha kuwaleta Afrika kuwafanya watumwa?

@Hapo kwenye neno dunia ulipaswa kusema neno wazungu kwa maana wao ndio waliovunja amani kwa kuwafanya waafrika kuwa watumwa kwa maendeleo yao
Hata Waafrika walivunja amani.

Machifu wa Kiafrika waliuza Waafrika wenzao kwa wazungu, waliwaonesha wazungu njia, mzungu ilikuwa vigumu sana kuingia Afrika na kufanya mambo yake bila msaada wa Muafrika.

Pia, kama mfumo huo umezifanya nchi fulani zikaendelea mpaka keo zikaanzisha internet, unayofaidika nayo wewe leo, na wewe umefaidika nao huo mfumo.

Ndiyo nauliza, is the pain worth the reward?

If yes, why. If no. Why not?

Hapa tunafanya cost benefit analysis.

Sent from my typewriter using Tapatalk
 
Constraints za swali zinasema ukienda hurudi. Unakufa.

Wewe unakwenda.

Mpaka hapo nina mashaka. Inawezekana hujaelewa swali au uko suicidal.

Sent from my typewriter using Tapatalk
 
problems bring development
 
Hakuna muafrika aliyechukuliwa bila waafrika wenzie kuhusika na huu ukweli huwa hatutaki kuukubali.
Ukisoma tu issue nzima ya utumwa ni waafrika baadhi waliamua kuungana na wazungu ili kuuza wenzao so, ni kweli wazungu walitumia urafi wa supremacy ya waafrika baadhi kurahisisha kitu chote.

Waafrica kutokwenda mbele kutawala ni kutokana na system tuliyokuwa nayo. Wakati wenzetu wapo kwenye capitalism, sisi kwa kiasi kikubwa tulikuwa katika feudal societies ambazo zisingeweza kuwa na nguvu yoyote ya kufanya hilo
 

kweli kabisa mkuu,hilo hata mimi nimeliona,nimewahi kufuatilia barua za david livingstone anasema alipofika Tabora alikuta wenyeji wanawakamata watumwa walioachwa njiani na slave traders kwa sababu mbalimbali ikiwemo udhaifu na magonjwa na kwenda kuwauza kwa slave traders wengine[emoji16]


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Waafrica kutokwenda mbele kutawala ni kutokana na system tuliyokuwa nayo. Wakati wenzetu wapo kwenye capitalism, sisi kwa kiasi kikubwa tulikuwa katika feudal societies ambazo zisingeweza kuwa na nguvu yoyote ya kufanya hilo
@kwa hiyo huu ni uthibitisho tosha ya kuwa wazungu wapo inherently Intelligent tangia zama za kale? Au sio?
 
Sijasema wewe. Nimesema ninyi mkuu
Ukisema ninyi uneshanijumulisha mimi hapo.

Katika set theory, ukiniletea set ya ninyi, set ya mimi ni subset katika set ya ninyi.

Sent from my typewriter using Tapatalk
 
Na kuna makabila ambazo zilikuwa kama nchi kipindi hicho zilikuwa zinauza watu wa makabila ambayo yamewazidi nguvu. Kwa hiyo kuweka utumwa kama responsibility ya wageni na kuondoa kushiriki kwetu, kwa kiasi flani ni kupotosha watu
 
Na kuna makabila ambazo zilikuwa kama nchi kipindi hicho zilikuwa zinauza watu wa makabila ambayo yamewazidi nguvu. Kwa hiyo kuweka utumwa kama responsibility ya wageni na kuondoa kushiriki kwetu, kwa kiasi flani ni kupotosha watu

kweli kabisa Chief ,kwa kiasi kikubwa Waafrica wenyewe walichangia kutawaliwa,hivi wazungu wana makabila au ukoo ?


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
@kwa hiyo huu ni uthibitisho tosha ya kuwa wazungu wapo inherently Intelligent tangia zama za kale? Au sio?
Ukisoma historia ya civilisation ulimwengu huu utaona hata wazungu kuna kipindi walionekana ni barbaric. Nchi za Asia kama China na India zilianza civilisation kabla hata ya wazungu wenyewe.
ukisoma deeply kwa History unakuja kujua hata mazingira yalichangia wao kuendelea mfano mazingira ya baridi kali ni lazma yangewalazimu kutafuta alternative ya chakula na malazi katika msimu huo. Tofauti na huku kwetu ambapo kwa kiasi kikubwa tulipata vingi kutoka katika nature na hata climate ni nzuri kiasi hivyo, maendeleo yalikuwepo kutokana na level yetu ya changamoto tu
 
kweli kabisa Chief ,kwa kiasi kikubwa Waafrica wenyewe walichangia kutawaliwa,hivi wazungu wana makabila au ukoo ?


Sent from my iPhone using JamiiForums

Sijawahi kufuatilia kiundani lakini kwa context ya nini maana ya koo ni lazma ziwepo ila kwa makabila sijui na sijawahi kusikia zaidi ya kujua kuwa watu wengi waliishi kwa classes.

Mfano sehemu nyingi waliishi kwa status mfano royal families na viongozi wengine, wafanyabiashara na maskini wengi ambao walikuwa peasants. Sina uhakika sana maana sijayapitia siku nyingi
 
mazingira yalichangia wao kuendelea mfano mazingira ya baridi kali ni lazma yangewalazimu kutafuta alternative ya chakula na malazi katika msimu huo.
Mkuu, kumbuka wazungu walikuwa na silaha kali zaidi ya babu zetu ndio maana walitushinda vita. Tulishindwa kuonesha upinzani ulio thabiti dhidi yao na kuwafurusha kurudi kwao. Huoni hii pia ni ishara ya kuwa na akili kubwa dhidi yetu?
 
mazingira yalichangia wao kuendelea mfano mazingira ya baridi kali ni lazma yangewalazimu kutafuta alternative ya chakula na malazi katika msimu huo. Tofauti na huku kwetu ambapo kwa kiasi kikubwa tulipata vingi kutoka katika nature
Vp kuhusu industrial revolution? Wakati sisi tunawinda na kula matunda porini, wao walikuwa na viwanda vikubwa vikubwa
 
Sijamlaumu Mansa Musa kufafiri nimeangalia faida na hasara ya kusafiri kwake kama zao la utashi wake.
 
Mkuu, kumbuka wazungu walikuwa na silaha kali zaidi ya babu zetu ndio maana walitushinda vita. Tulishindwa kuonesha upinzani ulio thabiti dhidi yao na kuwafurusha kurudi kwao. Huoni hii pia ni ishara ya kuwa na akili kubwa dhidi yetu?

Okey unajua ukifuatilia maendeleo huwezi kuangalia angle moja tu mfano hao wazungu walianza kuwa powerful baada ya kugundua hizo silaha kali pamoja na teknolojia ya majini ambayo ilisababisha wao kuweza kutembelea sehemu nyinginezo duniani. Ila tukiangalia msingi wa teknolojia na civillisation utaona umetoka sehemu nyingine tofauti ambazo hata weusi tulihusika japo historia nyingi ziliandikwa na wakoloni hivyo, angle ya kumtambua mtu mweusi kama aluyeendelea kabla ya wao ikafutika. Kwa nini unadhani ??..

Waliua kila kitu cha mtu mweusi hadi historia ili tuwe wategemezi hadi kifikra. Ukishakuwa hivi huwezi kuendelea maana utakuwa soko na sio mzalishaji always

Kafuatilie jinsi nchi za Asia ziliaga umaskini ingawa ukifuatilia katika kipindi cha uhuru tulikuwa almost sawa kiuchumi. Labda hili litakupa picha kamili mfano ni tiger economies za Asia. Google them mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…