A BITTER TRUTH: Kwanini watu weusi walishindwa kwenda Ulaya/Amerika (Ughaibuni) kuwachukua wazungu (Whites) kisha kuwaleta Afrika kuwafanya watumwa?

A BITTER TRUTH: Kwanini watu weusi walishindwa kwenda Ulaya/Amerika (Ughaibuni) kuwachukua wazungu (Whites) kisha kuwaleta Afrika kuwafanya watumwa?

@Hapo kwenye neno dunia ulipaswa kusema neno wazungu kwa maana wao ndio waliovunja amani kwa kuwafanya waafrika kuwa watumwa kwa maendeleo yao
Hata Waafrika walivunja amani.

Machifu wa Kiafrika waliuza Waafrika wenzao kwa wazungu, waliwaonesha wazungu njia, mzungu ilikuwa vigumu sana kuingia Afrika na kufanya mambo yake bila msaada wa Muafrika.

Pia, kama mfumo huo umezifanya nchi fulani zikaendelea mpaka keo zikaanzisha internet, unayofaidika nayo wewe leo, na wewe umefaidika nao huo mfumo.

Ndiyo nauliza, is the pain worth the reward?

If yes, why. If no. Why not?

Hapa tunafanya cost benefit analysis.

Sent from my typewriter using Tapatalk
 
@Scenario hii inategemea na ujasiri wa mtu. Mimi ninakwenda ila kuna mwingine hawezi kwenda hata ukimpa silaha.

Na hii kitu (risk taking) ndio humtofautisha mjarisiamali na mtu wa kawaida. Inawezekana hata huko porini hakuna Simba ila watu wanataka kupima ujasiri wako.

Wazungu waliweza kutoka kwao na kuja kwetu Afrika kwa maana walikuwa ni risk takers. Walijua wanakuja watakutana na dhoruba kali baharini wakiwa na majaazi still wakaja.

Walijua wanakuja kukutana na watu wasiokuwa na taarifa za kutosha juu yao still wakaja na kutuma wapelelezi. The higher the risk one is willing to take, the higher the return.
Constraints za swali zinasema ukienda hurudi. Unakufa.

Wewe unakwenda.

Mpaka hapo nina mashaka. Inawezekana hujaelewa swali au uko suicidal.

Sent from my typewriter using Tapatalk
 
Bila kuathiri majibu ya watu wengine, sababu ya ziada ninayofikiri ni kwamba inawezekana Wazungu walikuwa na shida nyingi kuliko Waafrika. Kabla hawajagundua teknolojia watu wao wengi walikufa kutokana na mazingira magumu ya kuishi, ikiwa ni pamoja na baridi kali, njaa, magonjwa nakadhalika -- yaliyotokana na jiografia ya nchi zao. Ilibidi watumie akili za ziada kuishi. Wakajikuta wanatoka 'nje ya box' hadi kufika kwetu. Kwa upande wetu huku Africa, Mungu alitupendelea sana kwa raslimali nyingi, hali ya hewa nzuri n.k. ikawa huhitaji kutumia akili nyingi sana 'kusavaivu' Afrika. Tukabweteka. Bahati mbaya sana tunaendelea kubweteka hadi leo.
problems bring development
 
1.Technology-mzungu na muafrica walikutana kwa mara ya kwanza mnamo karne ya 15 wakati huo mzungu yupo mbali kidogo katika teknolojia mfano silaha hivyo tusingeweza kuwateka kama tungeenda

2.Umasikini -Mzungu aliweza kufika huku kututeka kutokana na kwamba alikuwa na capital sasa kwa mfano mkwawa angeweza ku finance jeshi lake kwenda Ulaya ?

3.Kutokuwa na Wazo hilo- Mu Africa hakuwa na wazo la kumtawala mzungu kama mtumwa kwa sababu wazungu walimuitaji mtu mweusi kumfanya mtumwa kwenye mashamba ya Miwa nk lakini sisi tuliitajiana kufanyana misukule

4.SABABU ZA KIUTAWALA-Wazungu walikuwa na mfumo mzuri wa kiutawala kwa mfano Uingereza ilikuwa chini ya utawala wa kifalme pamoja na nchi zingine za Ulaya lakini huku kwetu tuliongoz kitemi kila kabila na mtemi wake hivo isingewezekana wote wakubaliane katika kwenda Ulaya na kuteka wazungu
Hakuna muafrika aliyechukuliwa bila waafrika wenzie kuhusika na huu ukweli huwa hatutaki kuukubali.
Ukisoma tu issue nzima ya utumwa ni waafrika baadhi waliamua kuungana na wazungu ili kuuza wenzao so, ni kweli wazungu walitumia urafi wa supremacy ya waafrika baadhi kurahisisha kitu chote.

Waafrica kutokwenda mbele kutawala ni kutokana na system tuliyokuwa nayo. Wakati wenzetu wapo kwenye capitalism, sisi kwa kiasi kikubwa tulikuwa katika feudal societies ambazo zisingeweza kuwa na nguvu yoyote ya kufanya hilo
 
kweli kabisa mkuu,hilo hata mimi nimeliona,nimewahi kufuatilia barua za david livingstone anasema alipofika Tabora alikuta wenyeji wanawakamata watumwa walioachwa njiani na slave traders kwa sababu mbalimbali ikiwemo udhaifu na magonjwa na kwenda kuwauza kwa slave traders wengine[emoji16]

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
@kwa hiyo huu ni uthibitisho tosha ya kuwa wazungu wapo inherently Intelligent tangia zama za kale? Au sio?
 
Na kuna makabila ambazo zilikuwa kama nchi kipindi hicho zilikuwa zinauza watu wa makabila ambayo yamewazidi nguvu. Kwa hiyo kuweka utumwa kama responsibility ya wageni na kuondoa kushiriki kwetu, kwa kiasi flani ni kupotosha watu
 
kweli kabisa Chief ,kwa kiasi kikubwa Waafrica wenyewe walichangia kutawaliwa,hivi wazungu wana makabila au ukoo ?

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
@kwa hiyo huu ni uthibitisho tosha ya kuwa wazungu wapo inherently Intelligent tangia zama za kale? Au sio?
Ukisoma historia ya civilisation ulimwengu huu utaona hata wazungu kuna kipindi walionekana ni barbaric. Nchi za Asia kama China na India zilianza civilisation kabla hata ya wazungu wenyewe.
ukisoma deeply kwa History unakuja kujua hata mazingira yalichangia wao kuendelea mfano mazingira ya baridi kali ni lazma yangewalazimu kutafuta alternative ya chakula na malazi katika msimu huo. Tofauti na huku kwetu ambapo kwa kiasi kikubwa tulipata vingi kutoka katika nature na hata climate ni nzuri kiasi hivyo, maendeleo yalikuwepo kutokana na level yetu ya changamoto tu
 
kweli kabisa Chief ,kwa kiasi kikubwa Waafrica wenyewe walichangia kutawaliwa,hivi wazungu wana makabila au ukoo ?

Sent from my iPhone using JamiiForums

Sijawahi kufuatilia kiundani lakini kwa context ya nini maana ya koo ni lazma ziwepo ila kwa makabila sijui na sijawahi kusikia zaidi ya kujua kuwa watu wengi waliishi kwa classes.

Mfano sehemu nyingi waliishi kwa status mfano royal families na viongozi wengine, wafanyabiashara na maskini wengi ambao walikuwa peasants. Sina uhakika sana maana sijayapitia siku nyingi
 
mazingira yalichangia wao kuendelea mfano mazingira ya baridi kali ni lazma yangewalazimu kutafuta alternative ya chakula na malazi katika msimu huo.
Mkuu, kumbuka wazungu walikuwa na silaha kali zaidi ya babu zetu ndio maana walitushinda vita. Tulishindwa kuonesha upinzani ulio thabiti dhidi yao na kuwafurusha kurudi kwao. Huoni hii pia ni ishara ya kuwa na akili kubwa dhidi yetu?
 
mazingira yalichangia wao kuendelea mfano mazingira ya baridi kali ni lazma yangewalazimu kutafuta alternative ya chakula na malazi katika msimu huo. Tofauti na huku kwetu ambapo kwa kiasi kikubwa tulipata vingi kutoka katika nature
Vp kuhusu industrial revolution? Wakati sisi tunawinda na kula matunda porini, wao walikuwa na viwanda vikubwa vikubwa
 
Mansa Musa kasafiri unamlaumu, asingesafiri ungemlaumu kwa nini Waafrika hawajasafiri!

Utashi unaenda na vipaumbele vya jamii.

Waafrika kipaumbele chao tangu awali ni kuishi kwa amani na utulivu, Ndiyo maana Waafrika original walikuwa watu peaceful sana. Sasa, ukiwa mtu peaceful habari za maendeleo ya kumfanya mwenzako awe mtumwa huwezi, mambo ya kwenda nchi za watu utaona mwiko, utaona unawaingilia sehemu zao.

Hizi sheria hata wanyama wanazo, wana kojolea sehemu zao kuzi mark, akija mnyama mwingine ajue hapa ni eneo la mnyama tofauti na mimi.

Wazungu waliondoa habari za kutaka kuishi kwa amani, wao kipaumbele chao kikawa kupata utajiri.Na ukiwa na mawazo hayo ndiyo unapata habari za kuafanya wenzako watumwa na makoloni.

Swali la muhimu hapa ni, je, ingewezekana dunia kupata maendeleo ya kiuchumi bila amani kuvunjwa? Bila watu kufanywa watumwa na vita kubwa kufanyika?

Na kama iliwezekana, hao mnaosema wazungu, walikosea kutafuta maendeleo kwa vita na utumwa na ukoloni? Hiyo ni akili nzuri au mbaya?

Na kama haikuwezekana, tukipata maendeleo sana, halafu dunia ifike mwisho wa uwezo wake wa ku support maisha, kwa sababu ya ma global warming, ma nuclear weapons etc, hayo maendeleo yakakayomaliza maisha duniani yatakuwa na maana gani?
Sijamlaumu Mansa Musa kufafiri nimeangalia faida na hasara ya kusafiri kwake kama zao la utashi wake.
 
Mkuu, kumbuka wazungu walikuwa na silaha kali zaidi ya babu zetu ndio maana walitushinda vita. Tulishindwa kuonesha upinzani ulio thabiti dhidi yao na kuwafurusha kurudi kwao. Huoni hii pia ni ishara ya kuwa na akili kubwa dhidi yetu?

Okey unajua ukifuatilia maendeleo huwezi kuangalia angle moja tu mfano hao wazungu walianza kuwa powerful baada ya kugundua hizo silaha kali pamoja na teknolojia ya majini ambayo ilisababisha wao kuweza kutembelea sehemu nyinginezo duniani. Ila tukiangalia msingi wa teknolojia na civillisation utaona umetoka sehemu nyingine tofauti ambazo hata weusi tulihusika japo historia nyingi ziliandikwa na wakoloni hivyo, angle ya kumtambua mtu mweusi kama aluyeendelea kabla ya wao ikafutika. Kwa nini unadhani ??..

Waliua kila kitu cha mtu mweusi hadi historia ili tuwe wategemezi hadi kifikra. Ukishakuwa hivi huwezi kuendelea maana utakuwa soko na sio mzalishaji always

Kafuatilie jinsi nchi za Asia ziliaga umaskini ingawa ukifuatilia katika kipindi cha uhuru tulikuwa almost sawa kiuchumi. Labda hili litakupa picha kamili mfano ni tiger economies za Asia. Google them mkuu
 
Back
Top Bottom