A BITTER TRUTH: Kwanini watu weusi walishindwa kwenda Ulaya/Amerika (Ughaibuni) kuwachukua wazungu (Whites) kisha kuwaleta Afrika kuwafanya watumwa?

A BITTER TRUTH: Kwanini watu weusi walishindwa kwenda Ulaya/Amerika (Ughaibuni) kuwachukua wazungu (Whites) kisha kuwaleta Afrika kuwafanya watumwa?

Slavery bana ilukua ni mode of business kwa kipindi kile, nothing personal ubaguzi wa rangi uliotokea baada ya slavery ni matokeo ya mwafrika kuonekana inferior kwakua alikua mtumwa. Mzungu alijua mwafrika ni binadamu wa kawaida toka mwanzo tu, sio kwamba alidhani sisi ni nyani au kenge sema wakawafundisha watu na waafrika wenyewe kwamba negros are created by God to serve hii mentality ilikuepo marekani kwa kiasi kikubwa hadi in 1970's. Na tukumbuke kwamba mwafrika sio mtumwa wa kwanza enzi izo kwenye tawala zilistaarabika Kama Uingereza kulikua na ubaguzi mkubwa wa kiuchumi, kiutawala na kijamii hapo kulikua na madaraja ya wazungu watumwa na wale watawala na matajiri wafanya biashara. Hata kipindi wazungu wengi wanahamia "New world" marekani, wazungu wenyewe na native Americans ndo walichapa kazi kwenye plantations za wadosi kabla ya kupatikana altanative, cheap kama sio free labour kutoka West Africa. Kwaio mtazamo wangu ni biashara tu jamaa walituwahi mbona sisi tualiwawahi waisraeli kule misri na walichapa kazii kweli 😂😅. Ni kama sisi tunavowakandamiza mbwa, nyani, artificial intelligence, computers na robots kwa wale wanaomini katika evolution theory vipi na hawa viumbe siku wakapata ufahamu na kuanza kutulaumu kwa kuwakandamiza.
Good reasoning brother
 
Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa jamiiforums. Mimi mdogo wenu (Last Born) Infantry Soldier nipo mzima kabisa wa afya. Thanks to God the Almighty. Eti ndugu zangu watanzania;

Kwanini watu weusi walishindwa kuwa wa kwanza kwenda Ulaya/Amerika (Ughaibuni) kuwachukua wazungu kisha kuwaleta Afrika kuwafanya watumwa?

Kwanini wazungu/waarabu waliweza kuwa wa kwanza kuwaza kuja kuwazoa babu zetu na kuwafanya bidhaa?

Waafrika tulikosa nyenzo gani za kutufanya kuwa wa kwanza kwenda Ughaibuni kisha kuwazoa wazungu kuja kufanya kazi za kitumwa katika mashamba yatu?

Je, hii inadhihirisha ya kuwa wazungu/waarabu wana kitu cha ziada kwenye akili/bongo zao (highly intelligent) tangia zama za kale mpaka wakawaza kuja Afrika kwa mara ya kwanza?

HILI SWALI WADAU WENGI WANALIKWEPA
Je, kuna umuhimu wowote wa watu wa bara la Afrika kuendelea kulialia na kulalamikia biashara ya utumwa kama ni janga lililowarudisha nyuma kimaendeleo mpaka sasa?


NINAOMBA KUWASILISHA MADA HII FIKIRISHI. KARIBUNI SANA KWA MICHANGO YENU NDUGU ZANGU

Ninauza Vitabu Vya Kujifunzia Lugha Ya Kijerumani. Ich komme aus der Stadt Dar Es Salaam und verkaufe diese Deutsch-Lernbücher - JamiiForums

KUMBUKA: KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TAFADHALI TIMIZA WAJIBU WAKOIPASAVYO.


Waafrika didn't have a reason kwenda Uarabuni au Ulaya kuchukua watumwa because sie ni wachapakazi wa ukweli, hatukuhitaji watumwa waje kutulimia mashamba yetu tulijitosheleza sie wenyewe. Kingine, mila na desturi zetu zinakataza unyama kama huu.
 
Waafrika didn't have a reason kwenda Uarabuni au Ulaya kuchukua watumwa because sie ni wachapakazi wa ukweli, hatukuhitaji watumwa waje kutulimia mashamba yetu tulijitosheleza sie wenyewe. Kingine, mila na desturi zetu zinakataza unyama kama huu.
Sawa mzee baba nimekuelewa sana. Je, kuna umuhimu wowote wa watu wa bara la Afrika kuendelea kulialia na kulalamikia biashara ya utumwa kama ni janga lililowarudisha nyuma kimaendeleo mpaka sasa?
 
1.Technology-mzungu na muafrica walikutana kwa mara ya kwanza mnamo karne ya 15 wakati huo mzungu yupo mbali kidogo katika teknolojia mfano silaha hivyo tusingeweza kuwateka kama tungeenda

2.Umasikini -Mzungu aliweza kufika huku kututeka kutokana na kwamba alikuwa na capital sasa kwa mfano mkwawa angeweza ku finance jeshi lake kwenda Ulaya ?

3.Kutokuwa na Wazo hilo- Mu Africa hakuwa na wazo la kumtawala mzungu kama mtumwa kwa sababu wazungu walimuitaji mtu mweusi kumfanya mtumwa kwenye mashamba ya Miwa nk lakini sisi tuliitajiana kufanyana misukule

4.SABABU ZA KIUTAWALA-Wazungu walikuwa na mfumo mzuri wa kiutawala kwa mfano Uingereza ilikuwa chini ya utawala wa kifalme pamoja na nchi zingine za Ulaya lakini huku kwetu tuliongoz kitemi kila kabila na mtemi wake hivo isingewezekana wote wakubaliane katika kwenda Ulaya na kuteka wazungu
Weak points mkuu ,no offence!

《Caprichar o teu sorriso》
 
Kwanini mzungu awe mbali kidogo? Huu ndio msingi wa swali langu. Ina maana wazungu wapo very intelligent tangia zamani sana na ndio maana wanatawala dunia mpaka sasa?
Ukijiongeza ukafuatilia historia nje ya hii uliyoaminishwa utagundua waafrika tulishawahi kutengeneza empire hadi hukoo roma ya kale na kiongozi wa mwisho aliitwa "Septimus severus karakala" huyu ndiye kiongozi wa mwisho mweusi wa roma ya kale .
Pia waafrika zamani tulikuwa tunaaminika na dunia kwa ujumla kuwa ni best warriors na ndiyo maana matajiri wa zamani wa ulaya , asia and the rest waliwakodisha waafrika kama walinzi wao fuatilia historia ya wale waafrika wanaoishi india zaidi ya miaka 800 wanajulikana kama "siddi".
Kingine ukifuatilia british royal family utagundua walikuwa na long line ya wafalme weusi waliotangulia mfano (1).prince james III of england (2).king james I of england e.t.c

Japo sijajibu swalu lako directly ila utapata mwanga zaidi ukifuatilia hizo angle chache nilizogusia na ukizidi jiongeza mwenyewe.

《Caprichar o teu sorriso》
 
Bila kuathiri majibu ya watu wengine, sababu ya ziada ninayofikiri ni kwamba inawezekana Wazungu walikuwa na shida nyingi kuliko Waafrika. Kabla hawajagundua teknolojia watu wao wengi walikufa kutokana na mazingira magumu ya kuishi, ikiwa ni pamoja na baridi kali, njaa, magonjwa nakadhalika -- yaliyotokana na jiografia ya nchi zao. Ilibidi watumie akili za ziada kuishi. Wakajikuta wanatoka 'nje ya box' hadi kufika kwetu. Kwa upande wetu huku Africa, Mungu alitupendelea sana kwa raslimali nyingi, hali ya hewa nzuri n.k. ikawa huhitaji kutumia akili nyingi sana 'kusavaivu' Afrika. Tukabweteka. Bahati mbaya sana tunaendelea kubweteka hadi leo.
Upo sahihi kabisa.

Mtu akipitia changamoto nyingi akili yake hupanuka haraka Sana
 
Mwafrika hakuwa na sabab kwenda ulaya! Mazingira yake yalijitosheleza kwa kila mamna! Angeenda ulaya kutafuta nini kinachokosekana afrika?kule ni kugumu!wao ndo walikuwa na kila sababu za kuja huku,kuhusu utofauti na mzungu! Sisi sio tofauti na wale jamaa ila ni mazingira tu!!wale changamoto nyingi ndo zilizowafanya wawe vile! Sisi hatuhitaji kufikiria saana ili tuishi kama wao!! Kosa tunalolifanya sasa ni ku behave kama wao wakati tupo kwetu na maisha yanaanza kuwa magumu bila sababu!! Tumeiga sana tamaduni zao na mwenendo wao wa maisha wakati mazingira yetu hayahitaji hivyo na tunazidi kuwa mambumbumbu kwenye mazingira yetu na wanatucheka tu!!!
 
Rejea historian..mwafrika amekuwa ulaya,Asia,Latin America etc miaka mingi kabla ya kristo. Uingereza, Spain,ufaransa,Russia etc wamethibitisha Hilo..hebu pitia vizuri vyanzo vyako mkuu..
 
Back
Top Bottom