A BITTER TRUTH: Kwanini watu weusi walishindwa kwenda Ulaya/Amerika (Ughaibuni) kuwachukua wazungu (Whites) kisha kuwaleta Afrika kuwafanya watumwa?

A BITTER TRUTH: Kwanini watu weusi walishindwa kwenda Ulaya/Amerika (Ughaibuni) kuwachukua wazungu (Whites) kisha kuwaleta Afrika kuwafanya watumwa?

Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa jamiiforums. Mimi mdogo wenu (Last Born) Infantry Soldier nipo mzima kabisa wa afya. Thanks to God the Almighty. Eti ndugu zangu watanzania;

Kwanini watu weusi walishindwa kuwa wa kwanza kwenda Ulaya/Amerika (Ughaibuni) kuwachukua wazungu kisha kuwaleta Afrika kuwafanya watumwa?

Kwanini wazungu/waarabu waliweza kuwa wa kwanza kuwaza kuja kuwazoa babu zetu na kuwafanya bidhaa?

Waafrika tulikosa nyenzo gani za kutufanya kuwa wa kwanza kwenda Ughaibuni kisha kuwazoa wazungu kuja kufanya kazi za kitumwa katika mashamba yatu?

Je, hii inadhihirisha ya kuwa wazungu/waarabu wana kitu cha ziada kwenye akili/bongo zao (highly intelligent) tangia zama za kale mpaka wakawaza kuja Afrika kwa mara ya kwanza?

HILI SWALI WADAU WENGI WANALIKWEPA
Je, kuna umuhimu wowote wa watu wa bara la Afrika kuendelea kulialia na kulalamikia biashara ya utumwa kama ni janga lililowarudisha nyuma kimaendeleo mpaka sasa?

NINAOMBA KUWASILISHA MADA HII FIKIRISHI. KARIBUNI SANA KWA MICHANGO YENU NDUGU ZANGU

Ninauza Vitabu Vya Kujifunzia Lugha Ya Kijerumani. Ich komme aus der Stadt Dar Es Salaam und verkaufe diese Deutsch-Lernbücher - JamiiForums

KUMBUKA: KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TAFADHALI TIMIZA WAJIBU WAKOIPASAVYO.
Kujiongeza kuliwabeba sana(akili ya ziada) waliyokuwa nayo ndo iliwapa fursa ya kututawala
Mzungu wa kwanza kufika afrika hata alikuwa hajui anaenda wap akatokea na kujikuta yupo kwenye ardhi yenye rutuba,maliasili za kutisha na kila zuri lipo ndipo akarud kuwambia wenzake kuwa kuna sehemu iko hivi
Wakaja kutupima wakaona wanaweza kututawala na kutupora Mali zote
Ukweli ni kwamba tulizubaa kuanzia wanaleta Dini zao tukapokea,wakaleta ustaarabu wao tukaupokea na ndipo hapo tulipofeli mpaka kesho
 
First I'd like to refute the notion that seems to be communicated, that enslaving and demeaning a person makes one to be smart. "Economics without conscience is destruction". I'd like to prove this by setting forth am example of the Moors(africans) who conquered Europe and civilized it from 711AD to 1490's years before the whites came to Africa. Whites came to africa after mid 15thC

When Black Men Ruled the World: 8 Things the Moors Brought to Europe

We flourished with our civilizations and great riches and technology.
Why do you think they hoard African artefacts in their museums?

And we have to admit the fact that the demeaning acts of slavery, colonialism, neo colonialism, rewriting of African history by the whites has so much ingrained in an African inferiority complexes. WE HAVE TO BELIEVE IN OURSELVES. History has great examples speaking to us.
Today an average african worships the whiteman.
I think the most suitable question to ask ourselves is how can we deliver ourselves and shake off the stigma within us that we may thrive as we should.
The stigma out there isn't a factor if you've delivered yourself on the inside
 
Infact uwezekano wa mtu mweusi ulikuwepo but ni kuzidiana tu kwenye UTHUBUTU na KUAMUA (haya yaliwasaidia kwenye nyanja zote ikiwa kwenye technology, Trade, Education etc...) actually mtu akikuzidi akili na awe mwenye kwa vipengele hivyo lazima uwe mtumwa .......that's why we still in up to now .......
 
Sidhani kama waafrika tuna akili tofauti na watu weupe au wazungu. Nachoona ni wenzetu waliwahi kustaarabika na kuendelea kabla yetu na waliweza kugundua vingi kabla yetu hivi hapo ndipo walipotuzidi.

Ila kama ubaguzi usipokuwepo kabisa duniani na mtoto wa kiafrika na kizungu akakuzwa katika mazingira sawa utakuta akili zao zinafanya kazi sawa. Mfano ni mashirika kama FBI ambapo kuna watu weupe na weusi na wote wanapiga mzigo sawa sema kutokana na ubaguzi mweupe atafanywa awe kiongozi wa mweusi
Huko kutangulia kwa wazungu kujuwa mambo ndio kuliko tufanya tuwe nyuma kwa kuchelewa kwetu.

Huu ni mpango wa Mungu, kaamua kutupunguzia majukumu.

Ndo maana hatuna uvumbuzi wa kitu chochote duniani ,Hata hizi ngoma zikienda ulaya wanaziboresha na zinakuwa nzuri na zenye mvuto mzuri sana..

Mwafrika ni imara kwa kazi ngumu zisizohitajimaarifamakubwa,hata akiwa amesoma,.

Karibuni miaka 60 tangia tuwe huru na zaidi ya miaka 100 tangia muafrika wa kwanza awe na elimu ya PHD au degree sawa na zile za wazungu. Lakini hakuna hata kitu kimoja tulichoweza kuvumbua kikawa UNIQUE kwa Afrika invention.

Ukweli ni kwamba hatuna uwezo wa ki uvumbuzi wala wa kutunza taarifa za research za vitu ambavyo vipo Afrika tuu haviko sehemu nyingine duniani.

Huundio udhaifu na kikomo cha uwezo wetu
 
Kwanini mzungu awe mbali kidogo? Huu ndio msingi wa swali langu. Ina maana wazungu wapo very intelligent tangia zamani sana na ndio maana wanatawala dunia mpaka sasa?
HUU ndio ukweli,
Ukiwa na akili kuliko wengine utaendelea kuwatawala wajinga,
Ukiwa na akili kuliko wengine,utaendelea kumiliki nguvu za kijeshi na utawala.
Ukiwa na akili kuliko wengine utaendelea kuutawala Uchumi wa dunia na technolojia.
Ukiwa na akili kuliko wengine utaendelea kuwa na nguvu za kijeshi, kisayansi, vifaa tiba,viwanda,uundaji wa mashine,mbali mbali na kuwa na ushawishi wa kisiasa duniani.
 
This truth is bitter indeed
 
Kwanza kabisa wazungu hawajatuletea dini. Tulikuwa na dini kabla hawajafika kwetu.

Pili, Waafrika hawakuwa na haja ya kwenda Ulaya kwa sababu waliridhika na neema nyingi za bara lao. Wakina Vasco da Gama wameondoka kwao kutafuta vitu ambavyo kwao havioti, wa Afrika hawakuwa na sababu ya kwenda Ulaya. Waliridhika na maisha yao.

Tatu, hizo habari za kumfanya mtu mwingine mtumwa zinaweza kuwa na manufaa kwa mtu mwenye akili fupi. Kwa kipindi kifupi. Maendeleo yanayotegemea utumwa ni maendeleo yasiyo sustainable. In the long run, jamii zilizoendekeza itumwa ama zilianguka (Rome) au ziliacha utumwa (Marekani).

Ndiyo maana watu wenye elimu wamepiga marufuku utumwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu nimeielewa sawasawa hii post Ila nina maswali mawili kwenye aya ya pili.
1.Hao kina Vasco ga Gama walivijulia wapi vitu visivyoota kwao?

2.Kwanini wafrika hawakwenda nje kutafuta visivyoota kwao? Si kuna mazao mengi tu yaliyoletwa na wazungu Africa kwa mara ya Kwanza?
 
Hili ndilo jibu sasa....mengne yote mnaruka ruka tuu...

Nami naongezea ....mtoa mada anatafuta source ya weupe kuwa chap kuliko sis wa huku weus..ishu ni mazingira tuu.ugumu wa mazingira.sis hal za hewa zetu znatufanya tu practice mambo kirahis tuu.mwkaa mzima unaweza lima.matunda mboga mboga yanajiotea.mvua za kutosha..hata nguo za kuvaa kwetu zilikua za ziada tuu..kule huwez ishi bila kujifunika sbab ya barid nakadhalika kadhalika so walitumia akili za ziada ku survive...

Sent using Jamii Forums mobile app
Nakubaliana na majibu yenye mtazamo ulionao, ni kweli shida nyingi huongeza maarifa.Lakini pia huku Afrika kulikuwepo na shida nyingi ambazo majibu yake yalitoka nje la sivyo tusinge adopt chochote kutoka nje.Hata leo Africa kuna changamoto nyingi ambazo utatuzi wake unasubiriwa kutoka taasisi za nje.Je hizi shida zilizotamalaki Africa hadi sasa bado hazitoshi kutufanya tufikiri zaidi.
 
Waafrika didn't have a reason kwenda Uarabuni au Ulaya kuchukua watumwa because sie ni wachapakazi wa ukweli, hatukuhitaji watumwa waje kutulimia mashamba yetu tulijitosheleza sie wenyewe. Kingine, mila na desturi zetu zinakataza unyama kama huu.
Mila zetu ndo zikawatupa mababu zetu na vizazi vyao kwenye utumwa? Bila shaka zilikuwa mila potofu.
 
Wazungu ni dhaifu sana kwenye kazi zinazohitaji misuli na nguvu nyingi,pili tulikosa nyenzo za kusafiri
 
Mkuu nimeielewa sawasawa hii post Ila nina maswali mawili kwenye aya ya pili.
1.Hao kina Vasco ga Gama walivijulia wapi vitu visivyoota kwao?

2.Kwanini wafrika hawakwenda nje kutafuta visivyoota kwao? Si kuna mazao mengi tu yaliyoletwa na wazungu Africa kwa mara ya Kwanza?
1. Walivijua kwa biashara, watu walibadilishana vitu kijiji kwa kijiji mpaka vitu vikafika mbali. Pia kuna watu wachache kama kina Marco Polo walitembea kufika nchi za mbali.Ukisoma historia ya Ulaya, hususana wakati wa Crusades, utaona Crusades zilivyowafungua macho Europe.

2.Waafrika wana neema, vitu kedekede vinaota kwao.Waingereza wanasema "necessity is the mother of invention". Waafrika hawakuwa na necessity ya kwenda Ulaya kutafuta kisichoota kwao, Waafrika walisambaa sana Afrika kila walipotaka kujitanua, bara la Afrika lina hinterland kubwa, liliwezesha expansion ndani ya Afrika.Bara la Ulaya lina coastline kubwa na hinterland ndogo.Nchi moja tu ya Congo ni sawa na 66% ya Western Europe nzima.

Kwa hiyo, Waafrika walitembea sana, ndani ya Africa.Nchi ilikuwa kubwa ipo. Wazungu nchi ilijaa, ikawabidi waende kutafuta makoloni nje ya Ulaya. Ndiyo maana wakaenda Marekani, Australia na Afrika.
 
Infantry Soldier mdogo wangu hii Africa yetu ni nzuri sana Ila tatizo kuna baadhi ya watu ndio wanatuangusha
 
Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa jamiiforums. Mimi mdogo wenu (Last Born) Infantry Soldier nipo mzima kabisa wa afya. Thanks to God the Almighty. Eti ndugu zangu watanzania;

Kwanini watu weusi walishindwa kuwa wa kwanza kwenda Ulaya/Amerika (Ughaibuni) kuwachukua wazungu kisha kuwaleta Afrika kuwafanya watumwa?

Kwanini wazungu/waarabu waliweza kuwa wa kwanza kuwaza kuja kuwazoa babu zetu na kuwafanya bidhaa?

Waafrika tulikosa nyenzo gani za kutufanya kuwa wa kwanza kwenda Ughaibuni kisha kuwazoa wazungu kuja kufanya kazi za kitumwa katika mashamba yatu?

Je, hii inadhihirisha ya kuwa wazungu/waarabu wana kitu cha ziada kwenye akili/bongo zao (highly intelligent) tangia zama za kale mpaka wakawaza kuja Afrika kwa mara ya kwanza?

HILI SWALI WADAU WENGI WANALIKWEPA
Je, kuna umuhimu wowote wa watu wa bara la Afrika kuendelea kulialia na kulalamikia biashara ya utumwa kama ni janga lililowarudisha nyuma kimaendeleo mpaka sasa?

NINAOMBA KUWASILISHA MADA HII FIKIRISHI. KARIBUNI SANA KWA MICHANGO YENU NDUGU ZANGU

Ninauza Vitabu Vya Kujifunzia Lugha Ya Kijerumani. Ich komme aus der Stadt Dar Es Salaam und verkaufe diese Deutsch-Lernbücher - JamiiForums

KUMBUKA: KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TAFADHALI TIMIZA WAJIBU WAKOIPASAVYO.

Swali Fikirishi hili, Ila kwa uelewa wangu Mimi ni kuwa Waafrika walistaarabika kabla ya Wazungu, Wayunani (Wagiriki) walisoma Kemet (Misri ya leo).
Unajua kitu kimoja ambacho kimezikumba jamii zetu nyingi ni kutokuhifadhi kumbukumbu kwa maandishi (jamii chache za Kiafrikazilifanya hayo).
Tuchukulie mfano wa Mansa Abubakri (Kaká yake Mansa Musa) wa Dola ya Mali (Mali Empire), huyu alifanya juhudi za makusudi za kutaka kujua mwisho wa bahari ya Atlantiki, na alikutana na Wahindi wekundu wa kule Amerika (miaka kama 300 hivi kabla ya Christopher Columbus kufika kule), na yeye pia alikiri hilo, zana walizokuwa wakitumia wale Wahindi wekundu zilikuwa sawa na za Mali enzi zile, Kuna kitu kinaitwa OLMEC COLOSSAL HEAD, jaribu pia kufuatilia na hichi kitu.
Pia kasome historia ya Mbanza Kongo (São Salvador wa Angola).

Amma kujibu swala lako, sijui kwa nini hatukuwafanya watumwa n.k ila Waafrika walifika mbali.
 
Kwanini mzungu awe mbali kidogo? Huu ndio msingi wa swali langu. Ina maana wazungu wapo very intelligent tangia zamani sana na ndio maana wanatawala dunia mpaka sasa?

Mamalaka yanakuja na kuondoka, Warumi, Warabu, Wachina, Wakemet (Wamisri + Wakush) n.k , wenzetu wameviandika na kutuambia chetu nnya na chao dhahabu nasi bado tunaamini hayo. Kwa Sasa wametupiga bao sana..
 
Sawa kaka mkubwa. Asante sana
 
Sidhani kama waafrika tuna akili tofauti na watu weupe au wazungu. Nachoona ni wenzetu waliwahi kustaarabika na kuendelea kabla yetu na waliweza kugundua vingi kabla yetu hivi hapo ndipo walipotuzidi.

so wao wastaarabu kuliko sisi? so huo ustaarabu walikua nao kabla ya kutufanya watumwa au baada?
 
Back
Top Bottom