A BITTER TRUTH: Kwanini watu weusi walishindwa kwenda Ulaya/Amerika (Ughaibuni) kuwachukua wazungu (Whites) kisha kuwaleta Afrika kuwafanya watumwa?

Nn kilisababisha historia ikageuka?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yaani tumfanye mzungu mtumwa wakati hata mpaka leo hatujafikia pale walipokuwa wamefikia wao walipokuja kwetu.
 
Wewe ndio umeharibu zaidi kwa sababu hapa unamaanisha kuwa waafrika tuko katika hatua za evolution kuelekea kuwa wazungu, kwamba itafika wakati tutatoweka (extinct) kama yalivyopotea yale ma dinosaurs! Hilo sidhani kama ni kweli. Kama ni evolution inaendelea basi ni kwa wote, kwamba hata wazungu, waarabu, wahindi, wachina na waafrika tukijichanganya katika msaragambo wa kuzaana inter-racially itafikia kipindi kuwe na wanadamu wapya wanaotofautiana na races zilizoko leo, kwamba kila race itaathirika na mabadiliko.
Makaburu wa Afrika kusini walipopitisha ile sheria ya apartheid mwaka 1948, mojawapo ya malengo yao yalikuwa kufanya preservation of the white race. Hata Marekani until last century tu walikuwa wamepiga marufuku inter-racial marriages kwa lengo hilohilo.
 
hahahahhahahahaa umepiga bom...shukran
ujumbe... waache kujenga hoja kwa history ya shuleni. Si rahis kuumaliza ulimwengu
yamefanyika mengi sana hapa duniani
we were kings and queens never porchy of monkeys

Sent from my SM-J5007 using JamiiForums mobile app
 
Egypt iliyowapokea na kuwatumikisha wayahudi haikuwa ya weusi.
Inventions nyingi zilizofanywa Afrika hazikufanywa na weusi, hata hizi unazosikia geometry na algebra kugunduliwa north Africa, hawakuwa weusi wale! Ni waarabu hawahawa tunaowaona leo wa Egypt, Morocco, Tunisia, Algeria, na hawa wa Egypt walisonga wakasogea hapo Sudan ambako hawaivi na weusi, unaona hata sasa nchi imegawanywa weusi wakabakia kusini. Ethiopians hawajikubali kama waafrika, actually wako Afrika kijiografia tu lakini hawapendi unasaba na weusi, na hiki ndicho chanzo cha mapinduzi ya Ethiopia yaliyomwondoa Mfalme Haile Selassie, ambapo Col Mengistu Haile Mariam alitoka jamii ya watu weusi waliokuwa wananyanyaswa Ethiopia na ndio waliokuwa wanapewa kazi za ulinzi, akatumia fursa hiyo kumpindua mfalme. Chanzo cha Eritrea kujitenga na Ethiopia ni hichohicho, kila anayejiona mweupe zaidi anajihesabia haki zaidi dhidi ya anayeonekana mweusi zaidi. Wasomali wanapenda kujitambulisha kama wasomali, hawapendi uafrika! Kwahiyo waafrika weusi ndio wanaotengwa, na sifa yoyote nzuri inayozungumzwa kwa jambo lililofanikiwa Afrika siyo ya hawa weusi!
 
Hannibal hakuwa mweusi.
Rejea historia hapa: Hannibal - Wikipedia
 
unajua mwarabu ameingia egypt mwaka gan??.. [emoji4]
unazungumzia historia ya mtu kama haile wa karne ya 20
me nakupa data za misri iliyoongozwa na Black khemets (kushite)... miaka elfu 3 kabla ya kuzaliwa yesu... means huu ni mwaka 2020 toka azaliwe yesu
urudi miaka elfu tatu kabla
ambapo hata nabii mussa alikua hajazaliwa.
Misri ambayo iliishi kwa kuamini miungu kama Amun-ra... osirs.. horus ... Anubis ... sobek

Bro.... [emoji38]

Sent from my SM-J5007 using JamiiForums mobile app
 
nyongeza

kwa nnachozungumza mimi ukimtaja Haile Selasie means urudi nyuma hadi kwenye uzao wake ambao QUEEN OF SHEBA , Alipata mtoto baada ya kutembelea Asia kwa nabii suleiman (king solomon) suleiman ambaye alikua mtoto wa mfalme Daud
hii ndio story ya Afrika nnayoizungumzia hapa... sio story ya Adolf Hitler wa 1940... myth but intelectual

Sent from my SM-J5007 using JamiiForums mobile app
 
siku moja ntakupa chanzo cha Haile Selasie kupinduliwa na jeshi lake ambalo liligawanyika sehem mbili kwasababu ya balaa la njaa...
kwasababu ya kubeba watu weusi jamaica na kuwapa hifadhi ethiopia akiwa kama baba wa imani wa rastafaries..
selasie i

Sent from my SM-J5007 using JamiiForums mobile app
 
Hannibal hakuwa mweusi.
Rejea historia hapa: Hannibal - Wikipedia
Source wikipedia? Leta credible evidence mkuu
Haya nmetaja hapo Thutmose 3 naye mweupe? 25th dynasty ilikuwa weupe? Haya Kush Empire iliotawala Ethiopia mpaka Middle East nayo weupe?

Kingine nmekuonyesha hao wazungu walishatawaliwa na race zingine mfano nmetoa Mongolia, Ottoman, Caliphate ya Baghdad n.k

Tukitaka kubalance mjadala mtueleze kwanini mnaanzia historia ya 15th century kuonyesha utumwa ni watu weusi tu
 
Kwanini Mpaka leo CCM haijaondoka madarakani?

Majibu yake ndio hayo hayo
 
Katika "factors" zote ulizozielezea inaonekana "Muzungu" alikuwa hatua moja mbele kuliko mtu mweusi. Swali bado liko palepale.
Why !??
 
Kwanini watu weusi walishindwa kuwa wa kwanza kwenda Ulaya/Amerika (Ughaibuni) kuwachukua wazungu kisha kuwaleta Afrika kuwafanya watumwa?

Kwanini wazungu/waarabu waliweza kuwa wa kwanza kuwaza kuja kuwazoa babu zetu na kuwafanya bidhaa?
Hawakushindwa. Hawakuona faida. Kinyume Afrika ilikuwa na watawala wengi waliokuwa tayari kuuza watu.

Utumwa ulikwa kwanza uhusiano wa kiuchumi. Chukua mfano miaka 1000 iliyopita. Katika sehemu za Afrika watumwa walikuwa wengi (ni wale waliokamatwa katika vita baina ya Waafrika). Hapakuwa na haja kubwa kuongeza wafanyakazi watumwa.
Kinyume Uchumi katika sehemu za Asia na baadaye pia Ulaya ulikuwa mbele zaidi, walihitaji wafanyakazi na pia askari watumwa (jisomee kuhusu askari watumwa katika nchi za Waislamu). Hivyo mfanyabiashara aliweza kupata faida kupeleka watumwa kutoka Afrika kwenda kaskazini kuliko kinyume.
Miaka 1000 iliyopita watumwa walikuwepo pia Ulaya na Asia. Pia "weupe". Kundi lote la "Slavonic peoples" (mababu wa Warusi, Wapoland, Wabulgaria...) lilipata jina la "slavonic=slaves" kwa sababu Ulaya Mashariki ilikuwa chanzo kikubwa cha watumwa kwa ajili ya nchi za Waislamu.
Ila kati ya watumwa hao wazungu ni wachache tu waliouzwa hadi Afrika; hasa mabinti waliouzwa. Mfano Mama wa Sayyida Salme wa Zanzibar (bofya na soma habari zake) alikuwa mtumwa kutoka Georgia aliyenunuliwa na Sultani wa Zanzibar.

Watumwa kutoka Ulaya wa jumla walibaki upande wa kaskazini wa jangwa Sahara.
Lakini tangu Wazungu wa Ulaya Magharibi kuvamia Amerika (baada ya 1500) walianza kutafuta watumwa kwa mashamba makubwa kule. Maana walishindwa kuwatumia wenyeji wa huko, waliokufa tu kutokana na magonjwa ya Ulaya - Asia. Hivyo walitafuta wafayakazi watumwa.
Chanzo kikuu kilikuwa Afrika penye watumwa tele na watawala waliokuwa tayari kuwauza.
 
Waafrika weusi chini ya Jangwa la Sahara (Sub-Saharan Africa) ni tofauti kabisa na hao wa Afrika kaskazini ambao bado nasisitiza hawakuwa weusi.
 
Ni kweli kuwa makundi yaliyoshiriki kumpindua Haile Selassie ni mengi likiwamo la Mengistu, lakini kilichomuibua Mengistu ni ubaguzi ambao weusi walikuwa wakifanyiwa huko Ethiopia.
 
Hee nani kakwambia mungu aliyachagua maeneo yale bro?si kweli wangu wala sidhani Kama mungu ana wivu wao wametupotosha kuamini mungu wao na wala mungu hakuchagua maeneo yale mungu yupo popote na ukimuomba popote anakusikia sio lazima uende huko!km angewachagua wao angewaweka ktk eneo lililo zuri na kila kitu.angalia hali ya hewa ya huko na africa wapi bomba kisha ujijibu mwenyewe wapi ni wapendwa wake cc au wao?tunaishi nao km wenzetu pamoja na mabaya yoote waliotufanyia km sio hekima ni nini wao wangewezaa?sisi sio wajinga kamwe ila hatujui uovu tunafundishwa na wao kilazima so many things to talk about hii mada ila the good thing is waafrica tumeanza kuamka look at u for eg
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…