Uchaguzi 2020 A coincidence or a highly calculated move? Bernard Membe kupeperusha bendera ya upinzani kwenye uchaguzi

Uchaguzi 2020 A coincidence or a highly calculated move? Bernard Membe kupeperusha bendera ya upinzani kwenye uchaguzi

Sesten Zakazaka

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2017
Posts
10,559
Reaction score
19,101
Hakuna grand coalition ya wapinzani, hakuna makubaliano rasmi kwa maana ya MOU kwa sababu sheria na kanuni mpya za uchaguzi zimeshawapiga stop kua wamechelewa

Lakini kuna Gentlemens' Agreement miongoni mwa vyama vikuu viwili vikubwa vya upinzani. Haisemwi, haiandikwi, haiwekwi wazi lakini ndio itakavyokua huku ikionekana kama ni sudfa tu (coincidence)

Tundu Lissu kashapitishwa na CHADEMA kuwania Urais kwa tiketi yao, Bernard Membe hatimaye atapitishwa na ACT Wazalendo. Na hapo ndio mchezo unaanza

Kwa vikwazo atakavyowekewa Lissu, viwe vya halali au kinyume chake, hatoboi!!! Vinaonekana ni viunzi vyepesi kisheria lakini wenye maamuzi wakishasema ndio ishatoka hiyo tena! Dhana ya kwamba ni calculated move inajionyesha hata kwenye kauli za hivi karibuni za Bwana Tindu Lissu mwenyewe

Ameanza kutumia lugha za ku provoke mamlaka! Kutamka uwezekano wa kuingiza watu barabarani au hata hilo la ku temper na wimbo wa taifa. Yote hayo ni katika kuwapatia sababu wenye mamlaka ya kuteuwa wagombea wa vyama wafanye maamuzi dhidi yake kisha lawama ziwaangukie wao hali ya kua kiuhalisia upinzani ulishakubaliana Membe ndio mpeperusha bendera. Kimya kimya na ili isionekane kua Chadema wali compromise kwenye hilo. Kwa hali hiyo tutaendelea kusikia kauli tata na kuwachokaza wahusika kutoka kwa Lisu ili asipitishwe kugombea iwe kwa kuwekewa pingamizi au kwa kuadhibiwa na msajili au NEC au hata mahakama

Muda ni muamuzi mzuri, basi na tusubiri kuyaona haya katika kipindi kifupi kijacho. Yetu macho hasa sisi tusio na vyama
 
Kama Kuna ka ukweli flani kwa mbaali....kwa kauli zile wenye upeo tumeanza kustuka.Ila ikiwa hivyo hatutakuwa tayari kumsapoti membe.....na sisi tutamwaga ugali.
Muda si mrefu kila kitu kitakua hadharani. Ni siku chache zimebaki kabda ya uteuzi wa Tume ya Uchaguzi
 
Back
Top Bottom