Dah!Nimeipenda sana hii kitu.
Nilinusurika kifo mara nne
Naweza kukiri kwamba meditation, martial arts na mazingira ya chuo yalinijengea uwezo fulani wa nguvu fulani, nguvu zenye uwezo wa kukuepusha au kujua hatari ijayo
Leo hii ningekuwa marehemu niliyeoza siku nyingi sana lakini kw namna ya ajabu kabisa nikakikwepa kifo mara nne
mara ya kwanza kwanza kwenye chumba fulani mtaani self container nilitorokea dirisha la bafuni/chooni..wakati jamaa, wakivunja mlango ili waingie wanimalize
Mara ya pili ilikuwa ni kama kilometer tatu tu kutoka chuoni wakaniotea niliwazidi maarifa nikatoka nduki mbio ambazo nafikiri nilimzidi Bolt
Mara ya tatu ilikuwa sumu kwenye pombe, nikategesha chupa mdomoni kama sekunde tano, nikaishusha mezani nikasepa
Mara ya nne ilikuwa na mambo mengi sana
Nilitoka chuoni saa nne usiku nikiwa na bastola( nilikuja kununua silaha) na hii yote ilikuwa kwa ajili ya kujilinda, nikafika mpaka Sambonani kwaito likiwa ndio kwanza linakolea
Mtu niliyemfuata akanipa signal kuwa pale hapakuwa penyewe wale wagomvi wangu walikuwepo kwahiyo tukachukua tax kwenda Zithobeni km kama tano hivi toka pale mjini
Tukafika kwenye bar moja kubwa na ukumbi wa disco, sasa ukifika pale unakabidhi silaha mlangoni kisha unasachiwa ndio unaruhusiwa kuindia ndani, mimi silaha niliichomeka chini y kitovu na nikanuia jamaa wasiione kweli haikuonekana nikaingia
Tukiwa tunakunywa kwenye dimlights za ukumbini nikawaona wabaya wangu meza kama ya nne hivi, palepale yakanicheza, lakini wakati huohuo mmoja wao akaenda chooni
Nilikaa tayari kwa lolote, nikiwa nawaangalia jamaa niliona mmoja ananyanyua chupa, na umeme ukakatika nilimrukia mtu wangu tukaanguka chini, kilichofuatia ni kishindo cha chupa ukutani nilisikia upepo wakati inapita juu ya kichwa changu