Ubuddha kama dini ni mfumo wa maisha. Lakini ubuddha hasa ni kuishi kwa mwenendo na mwongozo wa 'Buddha'...
Buddha ni mwalimu na kiongozi wa namna/mafundisho/njia ya Buddha--Aliyepata kuishi wakati fulani na mahala fulani nyuma huko India. Buddha ni mtu aliyetaamulika na kufanya chachu ya kueneza na kusambaza uhalisia wa 'taamuli' katika mtu.
Mafundisho ya Buddha ni ndiyo yanafanya 'Dhamapada' -- njia ya Buddha, kwamba katika kila mtu kuna mpango timamu, kamili na wenye kheri lakini huwa hukadirika katika mtu 'mwenye wongofu' ama mwenye kuishi kadiri ya kufuta njia ya kati kati kuelekea 'wongofu kamili'.
Ndivyo basi ndivyo gurudumu la spoku nane la dhama ni kadiri idhihirishayo njia ya Buddha ilipatwa kufundishwa na mwenyewe Buddha, mwenyekheri sana, kama mwongozo kuelekea 'wokovu' ulikokatika ama ujao na mtu aliyetaamulika.
Kinyume na wokovu ni basi hali yote ya mtu kuwa katika ulimwengu usiokuwa na nuru ya 'kibuddha' kusema kwamba, Mtu aliyekatika hali isiyo ya kutaamulika ni mtu mwenyekuishi katika ulimwengu wa masumbuko na kuathiriwa na kweli athimu ya 'Dhuka' -- adha nne za kuonwa kwa jicho la mali sana -- ambazo ni asili ya masumbuko yote, kutoridhisha kwa maisha ya muda hapa duniani: (i) kuishi ni safari isiyo na kinga ya adha zote za jasho, maradhi, uzee nk... (ii) Chanzo cha taabu zote kuwa ni mshikamano na muambatano wa hisia za fahamu ya mtu na mali/amari za dunia / ulimwengu na mambo yake. (iii) Kwamba muda ndiyo adui ama mwamuzi asiye epukwa kuhakikisha marefu ya mambo ya mtu na hata uhai wake, japo hata mauti si mwisho wa safari ya mtu kwa kuwa kuzaliwa tena na tena kwa mtu humtupa yeye kurudi katika yale yale kila awapo hapa duniani kwa sura hii ama ile, hapa ama kule (iv) Kwamba namna pekee ya kumkomboa mtu ni pasi kuifuata njia ya mali sana ya Buddha--Gurudumu la kufanyikia namna nane ili kumpeleka mtu katika 'Taamuli' ... kuishi namna ya kati, (kuwa na nidhamu ya kati/sahihi), kutizama yote namna ya kati, kauli ya katikati/sahihi, dhamira sahihi/kati, vitendo sahihi, jitihada sahihi, utiaaji akili sahihi, uweka ufahamu katika pahala sahihi...
Ndivyo basi Buddha alisisitiza katika kila mtu kuna 'buddha' ndani yake... na katika kila kilichofanyika na kuchukua sura kina 'dhama' ndani yake. Ni dhama pekee inayoweza kutibu maradhi ya mtu kujaribu moja hata jingine lakini kamwe asijekupata ridhiko la ndani hasa na maisha yake...
Na zaidi Buddha alifundisha maisha ya kudumu katika miditisha kama njia ya mtu kuongeza umakini juu ya yote yanayotawala akili yake na kumfunga na mengine yote ayapayo maana ama utambuzi kuhusu mapenzi yake ama hatima yake katika 'uzima' wote...
Miditisha katika mtu hukua na kumea na kumuongoza yeye katika ukombozi kamili wa 'nafsi' ili kuishia katika 'uto-nafsi' ulio ni 'Buddha' kamili. Safari ambayo huweza kuchukua mtu jitihada ya isho moja hata jingine mpaka siku yake kuamka na kuifikia 'moksha', ukombozi mbali ya mwili, akili na hisia fahamu. Katika Ubuddha hufundishwa kwamba nafsi ya mtu na viumbe vyote hujidhirisha kwa namna ya mizunguruko inayofanyika kwa kuzaliwa na kufa na huku 'nafsi' ikiwa ni kiungo chenye kudumisha ukweli wa maisha katika sura iliyofichika lakini ikawa dhahiri kwa buddha ama msafiri wa njia ya kibuddha mwenye kudumu katika maelekezo ya vitendo vya ufunguo ndani 'utiaaji akili sahihi' na pia 'uweka ufahamu katika pahala sahihi'...
Unaweza kujifunza mengi kuhusu Ubuddha kama namna ya visomo fananishi vya dini, lakini dini ni zao la utamaduni na azma ya watu wakiwa kama jamii yenye taasisi zenye kutawala mashauri juu ya miongozo ya stawi zao husika. Ualimu wa Kibuddha na tamaduni za kibuddha ni matokeo mifumo ijayo na taasisi--na kama ilivyokuwa juu ya taasisi yeyote, kusudi hasa huwa ni kueneza sura ya ustawi ama ustaarabu kwa nguvu za fikra na hisia juu ya jambo lake na basi kutafuta kujenga ama kudumisha ushawishi wake katika maisha ya watu.
Ubuddha ni dini ambayo misingi yake yapitiliza dhana na mapokeo ya 'mtu' na 'mungu' ama 'nafsi' na 'mungu'...
Katika mafundisho ya ubuddha nafsi hukanushwa, na mungu vile vile... lakini hapo hapo hujakuwa dhahiri kuwa mwenye kufuata maelekezo ya nidhamu ya kuutafuta wokovu, kukombolewa na 'dhuka'--mtu huja kuijua nafsi yake na kuimaliza; hujua yote ambayo mtu angeliweza kudhani ni 'tawala' ya kimungu lakini hatafungamana la lolote ila kuridhika kuwa mmoja na kweli inayopitiliza yote yaliyodhahirika, naam, ni kama kusema, hata kuacha mungu kuwa mungu kwa maana kwamba kila kitu tayari ni yote mtu awezayo kudhania ni 'mkono' wa mungu na mashauri mengine yote yenye kuambatana na hilo.
Ubuddha kama imani isiyojihusisha na fikra adilifu za mashauri ya 'mungu' katika ulimwengu wa leo utatuletea kung'amua na kuelewa vizuri ukweli na mashauri juu ya 'Meritokrasia'.
Dini kama Ukristo na Uislamu, zinatuletea kung'amua ukweli na mashauri zaidi juu ya 'Tekinokrasia'...
Ila ufundi wa mambo ya muingiliano wa mwili, akili na hisia--Maarifa ya Yoga na nidhamu za vitendo na upeo wa kutambua/kung'amua, utatulea ukweli na mashauri zaidi kuhusu 'Usanisi'--jinsi ambavyo 'umungu' na 'uzima' vyachakata kama moja katika kila kitu kilichofanyika, kilichodhahiri ama kisicho dhahiri.
Nuru ya Ufahamu katika mtu ndiyo msingi wa kheri yote.
Na ndivyo Buddha alifundisha, ni kheri kila mtu kuja kuwa nuru kwa yeye mwenyewe...