G'taxi
JF-Expert Member
- Sep 15, 2013
- 6,625
- 8,639
.....niliponyanyuka pale chini silaha nikiwa nayo mkononi nilikimbia upande wa chooni huku watu wakigongana na kupiga kelele sana
Ndani ya dakika kumi nilikuwa nimesharuka ukuta niko mtaani kuku defender zenye mijibwa na polisi zikiwa zimeshatake cover pale ukumbini
Nilikimbia mtaa kwa mtaa lakini kwa nyuma umbali wa kilometer moja nilipopata tax iliyonipeleka Zithobeni B, pale ilikuwa ni A naumbali wake ilikuwa kama km 3 hv
Nilifika kule salama lakini nikakuta bar ha uswazi hasa yenye virugu zote
Pale nikampata kijana ambaye nilimnunulia bangi na pombe ya kienyeji kama gongo halafu nikamwomba anitafutie usafiri wa kwenda chuoni hiyo sasa ilikuwa saa saba usiku
Kila dereva aliyetajiwa chuo chetu aligoma kwenda palikuwa panaogopeka mno
Ilipofika saa nane usiku kilikuja kigari nissan dutsun mbele kikiwa na watu wawili lakini kwenye canopy kuko tupu
Yule kijana alienda akaongea nao cha ajabu wakakubali wakati ni kama wamekuja kwenye starehe tena kwa rand kumi tu mpaka chuoni
Nikapanda kwenye canopy kigari kikaondoshwa kwa kasi ya ajabu, mmh nikashtuka ...kunchungulia kwenye kioo nyuma ya cabin ni wale vijana wapambe wa wale wabaya wangu, nikajua nimekwisha
Tunaondoka Zithobeni B kuelekea A lakini tulipokaribia A ghafla mwelekeo ukabadilika kuelekea highway..nikajua leo ama zangu ama zao
Ile kutaka tu kuingia high way ikawa unakuja semi trailer ambapo ilibidi jamaa asimame ghafla la sivyo rungeishia palepale
Kitendo cha kusimama ghafla ndio kilinipa mwanya wa kufungua mlango wa canopy na kuruka,
Nafatilia kwa makini...






