Temple tour na safari ya kwenda kuhudhuria ibada ya waabuduo shetani
Chuo chetu kila Jumapili kilikuwa kinapokea wageni wengi sana kutoka maeneo tofauti ya South Africa... Wengi walikuja temple kwa ajili ya ibada za chanting, meditation, masomo ya Buddhism lakini pia temple tour
Mimi nilikuwa mmoja wa ma tour guide, kazi ambayo niliipenda sana
Siku moja Jumapili mchana tukiwa karibia kabisa kumaliza shughuli za temple walikuja wazungu wanne wakiwa kwenye mavazi meusi full kuanzia miwani mpaka viatu
Wenzangu walikataa kuwahudumia lakini mimi nikakubali hivyo nikawachukua temple tour, wakawa watu wa maswali mengi sana kiasi kwamba tour iliisha karibia saa kumi na moja jioni
Baada ya tour ile ambayo waliipenda sana wakanipa ofa ya kwenda kwenye synagogue lao lililoko mji wa New Castle, mwendo wa zaidi ya masaa matatu toka chuoni, na kwamba nao wangependa mno nione ibada zao na usiku ule kulikuwa na ibada kubwa
Mpaka leo sijui ninini kilinifanya nikubali kwenda, tena kwa kutoroka kwakuwa nisingeruhusiwa katu na uongozi wa chuo
Nilicheza michezo yangu baada ya dinner na saa moja kasoro nilikuwa njiani kwenda New Castle na wale jamaa kwenye Cadillac jeusi tii, kuhudhuria ibada nisiyojua
Tukafika mwendo wa saa tatu usiku hivi nakumbuka huko njiani tulichepuka na kuingia rough road ya msitu na mashamba kwa zaidi ya nususaaa hivi
Kama kuna siku nilifika kuzimu basi ilikuwa siku hii, mbele yetu kulikuwa na jengo refu jeusi tii likisimama gizani ndani kulikuwa na taa za rangi zilizofifia
Jengo lilikuwa refu la grorofa tatu