Ok, Nimefanikiwa kuyaona maswali yako.
Kwanza Amua kweli katika Moyo wako kutaka kumjua MUNGU wa kweli.
Anza kufikiri kuhusu Dunia, Nyota zisizo kuwa na Idadi, JUA, Mbala mwezi, Bahari yenye mawimbi makubwa, Milima mirefu, Misitu minene, Species mbalimbali za wanyama wa kupendeza,Ndege wengi wa aina mbalimbali wa kupendeza,Majangwa, Mawingu, Mabonde makubwa, mito, Maporomoko ya maji, Matetemeko ya Ardhi, Volcanic eruption, Hurricanes, Vimbunga alafu jiulize swali moja NI NANI ALIYEVIFANYA VYOTE HIVYO?? najua hutopata jibu. (kama utakuwa umeweka elimu yako ya Darasani pembeni)
Jaribu kuzunguka Duniani kama uberikiwa kupata kipato kitakacho kuwezesha kusafiri..., Jaribu kutembelea sehemu mbalimbali Duniani Anzia Israel, Nenda Italy,China,Russia,SA,Thailand,Canada Bila kusahau nchi za Uarabuni kama Pakistani, Irani, Iraq, Kazakistan, Libya, Egypt nenda Australia, Cuba, Denmark n.k at least tembelea robo tatu ya nchi sehemu mbalimbali za Duniani.
KUMBUKA tembelea sehemu hizo ukiwa na nia ya kutaka kumjua MUNGU MWENYEZI, Utaona watu wengi maelfu kwa maelfu wakifanya Ibada mbalimbali kwa dini tofauti tofauti tembelea sehemu zao za Ibada.
Then kaa chini jiulize wewe ni nani na una nini cha ziada kuzidi watu wote mamia kwa maelfu utakao waona wakifanya ibada kumwomba MUNGU MKUU WA VIUMBE VYOTE ULIMWENGUNI.
Jitengenezee IMANI (kumbuka imani huja kwa kuamini na kuwa na uhakika na jambo unalolitarajia) Anza kuuambia MOYO wako ''nataka kumjua na kumfahamu MWENYEZI MUNGU MKUU, MKAMILIFU, MUUMBA MBINGU NA ULIMWENGU NA VITU VYOTE VINAVYOKAA NDANI YAKE'' jaribu kujiambia hivyo mara kwa mara na kwa muda mwingi.
Iset akili yako kutaka kumjua MWENYEZI MUNGU kumbuka hapo umeshajishusha na kujiondoa uthamani wako ambao ulifikiri mwanzoni unao., Utaanza kuona mambo madogo madogo tuu yakikudhihirishia uwepo wa MWENYEZI MUNGU ambayo naamini kwako Yatakuwa ni makubwa sana.
Kumbuka hutoweza kumwona MWENYEZI MUNGU (kama akili zako umeziset ivyo) kwani hakuna kiumbe chini ya JUA kinachoweza kumtazama MWENYEZI MUNGU kutokana na UKUU na UTUKUFU alionao.
MWENYEZI MUNGU NI MKUU NA MTUKUFU NA UKUU WAKE HAKUNA ANAYEWEZA KUUELEZEA.