A God can be a mere theory, nothing more

Naomba nikusahihishe kidogo,

Alafu unapokuwa unataja,kutamka au hata kuandika jina la MWENYEZI MUNGU jaribu kuwa na staha kidogo maana bado hujaujua ukweli kiasi cha kuweza kulichukulia jina la MWENYEZI MUNGU kama unavyolichukulia.
Kwani tofauti ya kusema MUNGU na mungu ni nini?
 

Hoja zangu ni kwamba
1. Mimi ninafahamu kuwa kila chenye mwanzo au ukomo kina kilichokifanya kuwapo. Ulimwengu Una mwanzo nini au nani aliufanya ulimwengu ?

Nini au nani akiyeanzisha uhai ?

Nini sababu au madhumuni ya binadamu kuwapo au kuishi ?

Hiyo Genesis yliyoinukuu Mimi sijui unataka msaada gani au unaelewa nini maana ya "heaven and earth " au kwako neno Heaven au Earth yapo katika umoja au uwingi.
Nitashukuru Sana kupata majibu.
 
Kwani tofauti ya kusema MUNGU na mungu ni nini?

Unapoandika Mungu ukianza na herufi kubwa Una maanisha aliyeumba dunia na vyote vilivyomo lakini unapoandika mungu Una maana ni yule wa kusadikika Kama yule wa atheist god of gaps
 

Mimi najadili Mungu kwa mapana yake sijifungwi kwenye vitabu vya dini Mkuu.
Hivyo unapojadili nami ujiandae kwa hoja zenye mantiki tu.
Tungekuwa tunajadili habari ya dini Mimi ni Mkristo nawajibika kujibu hoja zote kuhusu tumaini langu.
 
Hiyo Genesis yliyoinukuu Mimi sijui unataka msaada gani au unaelewa nini maana ya "heaven and earth " au kwako neno Heaven au Earth yapo katika umoja au uwingi.
Nitashukuru Sana kupata majibu
.
Hii ya Genesisi ni msingi wa kila kitu kuhusu biblia. (Thus why we say at the real beginning bible was wrong)
Huwezi ukasema mungu muumba wa vitu vyote halafu useme yeye kaumba mbingu na dunia (Vipi kuhusu Mars, Venus na sayari zingine?. Vipi kuhusu galaxies zingine?)

Mimi ninafahamu kuwa kila chenye mwanzo au ukomo kina kilichokifanya kuwapo. Ulimwengu Una mwanzo nini au nani aliufanya ulimwengu ?

Kuna nadharia nyingi sana kuhusu chanzo cha dunia. Mimi nitajikita katika ukweli kulingana na proofs za dark energy science na meditation point of view.
Tukija kwenye Science utakuja kugundua kuwa source ya dunia ni big bang
Siwezi nikatoa maelezo yote kuhusu big bang
Naomba usome hapa:
Big Bang - Wikipedia, the free encyclopedia

Angalia na hii video


Kuhusu Meditation:
Unapofanya meditation unakuwa kwenye realization unajua what is.
Utajua ukweli na utajua kitu gani sio kweli.
Sina mda wa kuweza kuelezea kila kitu hapa.

Nini au nani akiyeanzisha uhai ?
Hapa napo kuna nadhalia nyingi sana kuhusu uhai wa hapa duniani
Lakini kama nilivyoeleza hapa juu. Kuwa source of the physical universe ni big bang (Illusion)
Lakini asili halisi ya mtu ni consciousness. The evolution of consciousness ndio chanzo kikubwa cha uhai.

Nini sababu au madhumuni ya binadamu kuwapo au kuishi ?
Madhuni ya binadamu hususani hapa duniani ni kufanya adventure, kupata experience kwenye physical realm
But we have our home (7th Realm) The bodies is the physical then stay in the physical only but our consciousness or our soul live forever. We are immortals.


Kwa kujibu maswali yako turudi kwenye swali langu la Genesis 1:1 je mungu wenu aliumba mbingu na dunia je ni nani aliyeumba sayari zingine na galaxies zingine?
 
Last edited by a moderator:
Ninaanza katika somo lako unalolijua (Geograph)
Unamuongeleaje huyo mungu wako anayeongelewa kwenye biblia

Mungu ndiye Muumba wa Ulimwengu, nikimaanisha na Geographical features zote zilizopo Ulimwenguni ambapo Geographia ipo ndani yake.

Genesis 1:1 In the beginning God created the heaven and the earth.
Je unaongelea nini kuhusu sayari zingine? unaongelea nini kuhusu other Galaxies? Je hiyo Geography inakusaidia nini kuhusu kumjua huyo mungu wako?

Ninasikitika kwasababu maswali yako yanaonesha ni jinsi gani ulivyo na weledi mdogo na unachokiuliza,thats why nikasema mwanzoni kubali kwanza moyoni mwako kwamba akili zako ni finyu kiasi cha kutaka kuzitumia kumjua MWENYEZI MUNGU MUUMBA MBINGU NA NCHI.

issue iko hivi inapotamkwa Heaven and Earth inamaanisha Ulimwengu kwa ujumla yaani UNIVERSE. Ninaposema Universe ninajumuisha Mbingu na vilivyomo pamoma na Dunia ikiwemo ndani yake.

Sasa usije ukaibua hoja kwamba kwanini waandishi wa BIBLIA hawakutumia neno ''Universe'' badala ya ''Heaven and Earth'' nitakudharau na nitathibitisha una udogo wa kifikra.

Ulimwengu (UNIVERSE) ni mjumuiko wa vitu vyote vya angani na anga kwa ujumla ikiwemo Galaxies unazozisema na Sayari nyingine ikiwemo Dunia.., Kwa kifupi Biblia imetumia neno HEAVEN and EARTH.

Geography inanisaidia kuujua UTUKUFU wa MWENYEZI MUNGU kwani kinadharia bado inashindikana kufafanua na ku-proof Asili ya Ulimwengu Mzima.Hii inanipa nguvu ya kuzidi kumwabudu MWENYEZI MUNGU na kumweshimu zaidi. Geography inafundisha jinsi uso wa Dunia na Anga ulivyo na sababu za kuufanya uwepo kama ulivyo, Inanijengea Picha kidogo sana ya kwamba huyu MWENYEZI MUNGU ninaye mwabudu ni MTUKUFU na MKUU kwa amefanya mambo ambayo hayawezi kufikirika kwa urahisi na mtu yeyote.

 
Kwani tofauti ya kusema MUNGU na mungu ni nini?

Unapotamka mungu inaonesha dharau kwake, inaonesha unamchukulia MWENYEZI MUNGU kama kitu chochote kile like Jiwe, Ng'ombe n.k.

Lakini unasema MWENYEZI MUNGU inaonesha unaliheshimu jina lake na kumweshimu yeye, Unatambua UKUU NA UTUKUFU wake.

Ndio maana nikakwambia jaribu kuliheshimu Jina lake kwani bado haujatambua Ukweli wa kwamba yeye ni nani na anaMAMLAKA zipi, hadi siku ambapo utautambua ukweli ndipo uliite kama unavyoliita.

Kubishana kwako Kupinga imani za wengine na kujenga hoja kunaonesha Hofu tosha uliyokuwa nayo ya njia uliyochagua kuifata kwamba sio sahihi.
 

Nimekuukiza kuhusu Heaven and Earth hayo maneno yako kwenye umoja au uwingi.
Halafu habari ya multiverse ni just a tale.
Hujatoa jibu hata moja kwenye maswali yangu.
Genesis baada ya Genesis 1:1 kuna muendelezo kwenye Genesis 1:2... Namna uumbaji wa vitu vingine ulivyofanyika. Matatizo yako ya kuelewa isiwe ndiyo uyaite makosa ya maandiko.

Sitaki nadharia nyingi au moja nataka jibu lako wewe ambalo umelipata baada ya kusoma nadharia nyingi na kuchanganya na yako.
Habari ya bing bang sihitaji link nimeisoma haielezi chanzo Bali inaeleza process Kama wewe process waona ndicho chanzo hayo ni matatizo.
What banged my brother ?
Nataka unijibu chanzo cha universe ....
Dark energy science and meditation has nothing to do with my question.
Mimi sitaki kujua hoja zako nimetokana nadark energy au science au meditation Mkuu.
Nahitaji jibu kadri ya swali langu.
Mimi nikikwambia kutokana na ufunuo wa Roho mtakatifu hivi ndivyo ulivyo unaweza kunielewa ? Nami nataka unieleze wewe huyo dark energy sio member wa JF. Fikiri.

Evolution inaeeza process my brother mimi nimekuuliza kuhusu chanzo cha Uhai. Hayo mambo ya cell mutations and selection ni kwa faida yako.
Soma swali lielewe jibu kadri ya ulivyoulizwa.

Meditation and the like go and talk to your likes.
 
Last edited by a moderator:
Nina shangaa jinsi gani biblia yako huisomi na nina uhakika unayoyaongea yanatoka kichwani mwako jinsi unavyofikiri na si jinsi biblia ilivyo andikwa.
Hivi hujasoma mungu aliumba jua? hujui mungu aliumba na mwezi? pia hujui kuwa mbinguni ni mungu alipo!!? Je unataka kuniaminisha kuwa mbinguni ni kwenye sayari ya Jupita? au Mars? nk?
Hebu soma biblia na ulete uthibitisho.
Ninakupa maadhishi kadhaa yaliyopo kwenye kitabu chenu na mungu wenu muone jinsi gani mungu wenu aliumba dunia.
Naomba usibadilishe ulichokiandika baada ya kukupa huu ushahidi.
Shangaa haya mambo haya.
Genesis 1:1 Tayari mbingu na nchi imeumbwa sawa?(Kwa mujibu wako hii ndio universe)
Siku ya kwanza mungu anaumba mwanga kabla ya jua na mwezi (Ina shangaza unaumba mwanga lakini chanzo cha mwanga hakijaumbwa)
Genesisi 1:3-5
Siku ya nne utashangaa mungu wenu ndio anaumba sasa Jua, mwezi na nyota. Genesis 1:14-17

14And God said, Let there be lights in the firmament of the heaven to divide the day from the night; and let them be for signs, and for seasons, and for days, and years:


15And let them be for lights in the firmament of the heaven to give light upon the earth: and it was so.


16And God made two great lights; the greater light to rule the day, and the lesser light to rule the night: he made the stars also.


17And God set them in the firmament of the heaven to give light upon the earth,

Ukiangalia kwa umakini utagundua kabisa hiyo biblia iliandikwa kwa ajili ya utamaduni na uelewa wa watu wa utamaduni huo haina uhalisia wowote kuhusu hali halisi.

Hebu ninakuomba bila kujitoa ufahamu apply Geograph yako kufafanua hapa. Na kumbuka umesema mbingu na nchi ni universe.
 

Kama kila kitu kina mwanzo je Mungu mwanzo wake ni upoi kama yeye hahitaji kuletwa au kuumbwa kwanini unafikiri ulimwengu unahitaji kuumbwa.
 
Wewe unajichanya kidogo maana mara unaiamini biblia mara hutaki. Nipe jibu moja unaiamini au huiamini ili nikupe elimu tosha?
Halafu unapoongelea mambo ya kwenye biblia yenu lete mandishi hapa ili na wale wasio na hicho kitabu waweze kusoma.
Nikianza kukuchambulia Genesis 1 na Genesis 2 utashangaa kuona namna gani hicho kitabu kinavyo jichanganya. Ila ninachokuomba kimoja tu ni hakikishie kuwa wewe ni muumini wa biblia au la.

Nataka unijibu chanzo cha universe ...
Ndio maana mwanzo kabisa nilikuuliza chanzo cha mungu ni nini? Ukaruka ruka eti hana mwanzo wala hana mwisho.
Halafu nime kuwekea kwenye mabano kwamba (All physical world is illusion hujahoji kuhusu hicho)

Kama ukiondoa Time hakuna uwepo wa dunia au nyota utakutana na void.
Vibration ya molecules vinacreate frequency ambayo inatufanya tuone kama kitu.
Hebu nakuomba ufikirie kibiology na kichemistry kidogo.
Mtu ni multsystems (Reprodction system, Digestion System etc)
After System utapata Organ, From Organ Tissue, Form Tissue Utapata Cell From Cell Utapata Chromosomes from Chromosomes utapata DNA from DNA utapata Compound (Chemistry inaanza) baada ya Compound unapa element, Atom, Proton and Neuton unaenda mpaka kwenye particles zinazohusiana na Quantum Theorem ukiendelea zaidi utakutana na frequency na baada ya hapo utapa void. So the void created the complex human body (Consciousness/soul)

Mantiki ya hapa ni kwamba the consciousness is the one which created the universe. Our Consciousness evolution are the ones which created the universe. Thus why I said Big bang in the illusion of the physical world.

Naomba niishie hapa kwa sasa. Ila tujibiane taaratibu.
 
Mkuu kwani vitabu vinasomwaje?
Ikiwa mimi sikuelewa maana wewe usi utatoa maana halisi!!!!

Kama unakubali kuwa huko kusema kwako kuwa vitabu vya dini ni udanganyifu pengine yaweza kuwa ni kutokuelewa tu maana,sasa huoni kuwa ni bora ukasome vizuri hivyo vitabu na kupata maana halisi iliyokusudiwa kuliko kukurupuka na kuja kusema vitabu vya dini ni udanganyifu?

Bora ungesema unahitaji ufafanuzi ktk hivyo vitabu, lakini wewe unataka kuproof hivyo nitakapokuwa najaribu kukupa maana iliyokusudiwa wewe pia utaanza kutetea ulichokieleza matokeo yake itakuwa ubishi usio na mwisho.
 

Mkuu asiyeeleweka ni wewe,kumbuka mwanzo nilikwambia kuwa research yako nina mashaka nayo na ndipo tulipoanza kuangalia ulifanyaje hiyo research. Haueleweka, unakosowa mambo ya watu bila kueleza msimamo wako wewe ni upi?
 
Kama kila kitu kina mwanzo je Mungu mwanzo wake ni upoi kama yeye hahitaji kuletwa au kuumbwa kwanini unafikiri ulimwengu unahitaji kuumbwa.

Huo ni utoto perse. Biblia imeandima kuna mwanzo, sayansi miegundua ulimwengu Una mwanzo na hata nyakati zina mwanzo. Unapohoji hilo nikueleweje ? Nimesema kila kitu chenye mwanzo au ukomo au vyote lazima kiwe na chanzo. Universe Ina mwanzo hivyo lazima iwe na chanzo.
Mungu Hana mwanzo wala mwisho.
Swali lako limekosa uhalali
 

Namwamini Yesu Kristo.
 

Mimi sitaki vitu ulivyokariri au kukaririshwa
Kuhusu Biblia naomba kukuhakikishia kwamba Mimi Kama Mkristo naifahamu na kuielewa na kuamini ujumbe wake. Wewe ndiye mwenye matatizo na nimegundua kuna fallacy of definition inakwandama
Wewe kwako MTU akisema Nuru Ana maanisha jua ?
Huwezi kueleza chanzo cha uhai hadi uweke kariri zako ? Ambazo zinahitaji mjuzi wa aina yako kuunganisha na kupata maana
Jibu Kama unavyojibiwa nataka maelezo na sio nadharia za wengine
 
Mpaka hapa umeshindwa kumtetea mungu wako zaidi ya kujigamba majigambo ambayo hayana hata reference yeyote. Nimekusihi ulete reference zako za kibibilia tuweze kuzichambua hujaleta chochote.

Hapa unajigamba gamba tu pasipo hata reference yeyote. Mimi ninakupa facts wewe unaleta siasa za kidini
Ninataka ulete maelezo yaliyonyooka kuhusu uumbaji na ulete reference ya kuhusu jinsi gani mungu wenu aliumba universe (Stella, Galaxies, Stars, Planets etc.)
Usipoleta maandishi yeyote kutoka kwenye kitabu chenu kinacho support maelezo yako nitakuona kama unatoa maelezo yasio na proof ni kutoka kwenye kichwa chako tu na imani yako haba ya kuogopa mungu asiye umba universe. Ni sawa na mungu wa kichaga au wa kizanaki.

Swali la kizushi kwanini unaabudu mungu wa israel na sio mungu wa africa?
 
Nimekwambia biblia Nina iamini lakini sihitaji Biblia kujua uwepo wa Mungu, Biblia kwa anayejua kufikiri inaeleza ukuu wa Mungu na haikutegemea kuwa iwe kitabu cha kufundishia Jiografia wala fizikia.
Wewe unauliza na kutaka ujibiwe kana kwamba biblia ni kitabu cha jiografia na fizikia.
Wewe ndiwe wajidai kwa kuweka ulivyokaririshwa pasipo kuweka na kujibu maswali...
Nimekwambia niambie chanzo cha Universe na Uhai unaongea habari za process kwenye evolution na big bang nani alifanya hivyo vilivyo bang ?
Acha kushusha kariri zako lete majibu
 
Ninaweza kukuuliza kitu kidogo tu. Hivi tofauti ya kuwa kwenye ndoto na sasa hivi ni nini? Je hujui sasa hivi uko kwenye ndoto katika consciousness?

Nakuuliza tofauti ya MTU mwenye kichaa na wewe ni nini maana MTU mwenye kichaa hujiona na kusema yupo hrwani wakati anatembea ardhini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…