MUNGU, DINI!! Dah, mkuu umegusa pabaya sana ... umegusa sehemu ambayo wengi wanaogopa hata tu kupaona but naamini kabisa kwa utashi, maendeleo na elimu tulizonazo, Dini na Mungu ni vitu vinavyoweza kuongeleka as ni vitu tulivyovikuta na kufundishwa mara tu baada ya kuingia hapa duniani na pengine tutaviacha.
Mashaxizo binafsi naamini hoja na maswali yako yote ni ya msingi, na bandiko lako lina uwakilishi wa wengi, kwa mtu yeyote mwenye akili timamu maswali yote uliyouliza na mengine mengi ni aina ya mkanganyiko wa kimawazo ambao umewahi kuwapitia wengi wetu. Pamoja na kwamba sijajiandaa vema kushiriki mtazamo kutoka kwenye ubongo wangu ni kama ifuatavyo;
1. UWEPO WA MUNGU KAMA MUNGU: Kwanza nitoe msimamo wangu, binafsi kama maana ya MUNGU ilivyo, naamini uwepo wa MUNGU kwa maana ifuatayo [only as (GOD - A spirit worshipped as having power over nature or human fortunes; a deity.)] yupo.
Source:
https://www.google.co.tz/search?q=G...urceid=chrome&es_sm=93&ie=UTF-8#q=Define:+God
Na sababu za mimi kukubali na kuamini kuwa MUNGU huyu yupo ni zile zile ambazo
Mashaxizo unaamini MUNGU yupo kama ifuatavyo;
- Bahati : Uwepo wa bahati kwangu ni ishara tosha kabisa kuwa MUNGU yupo coz knows nothing, bahati haimjui yeyote wala chochote na ni kwa yeyote. Elimu, Nguvu, Umakini, Uzuri, Utajiri haukuhakikishii furaha na mafanikio mbeleni
- Origin of life: Ukweli ni kwamba sayansi na wanasayansi wamefanikiwa kwa mengi sana lakini kushindwa kwa sayansi na elimu kuelezea origin of life kumeendea kuacha mwanya mkubwa kuwa MUNGU ninayemwamini mimi yupo.
2.UWEPO WA MUNGU ANAYETAJWA KWENYE DINI: Hapa ndipo tatizo langu la kuamini uwepo wake(Mungu wa Dini) na Biblia linapokuja; Kama maswali yako yote uliyouliza, nimeshindwa kuwa mtu wa kuitikia tu ninachoelezwa na wachungaji/Waliookoka na Biblia. Kubwa hapa imekua ni saikolojia na kujiamini na hili sihitaji kulitolea mifano coz hiyo ndiyo hali halisi. Kwa kuongezea pale ambapo
Mashaxizo ulipoishia naomba niongeze yafuatayo:
- DINI NA UTUMWA - Ushiriki wa hizi dini kwenye biashara ya utumwa na ukoloni, ni kitu cha kwanza ambacho kimekuwa kikinitia wasiwasi mkubwa, makanisa na misikiti yote ya awali ilijengwa na watumwa kwa ''mkono wa chuma'' bila ujira wala huruma then hapo hapo later wanatolea mafundisho kuhusu MUNGU ... pengine kuna mengi yamejificha.
- TOFAUTI YA BIBLIA - Nasikia kuna aina tofauti ya biblia, kuna baadhi ya vitabu vya biblia vipo kwa madhehebu fulani na havipo kwa madhehebu mengine...Kwanini?
- MSAMAHA - Hoja ya msamaha kama inavyozungumziwa na dini esp. Christian imekuwa na ujanjaujanja na utata mwingi hasa kuhusu-kosa gani linasamehewa ama halisamehewi. Inaonekana kwamba makosa yote duniani yanasamehewa bila kujali ukubwa ama urefu wa kosa lenyewe ilimradi tu-... akiomba msamaha wa kweli kabla ya kufa. Hii binafsi, naona haijakaa sawa ...
- HYBRID ANIMALS - Hapa napo pananipa maswali mengi, wametoka wapi hawa; LIGERS=LION+TIGERS, MULES=DONKEY+HORSE na aina nyingi za mbwa wa kizungu ... -je, nao wameumbwa na MUNGU ama SCIENCE?
- UWEPO WA DINI NA MADHEHEBU - Uwepo wa dini nyingi zinazokinzana kwa kirefu sana ni swali gumu. Kwa mfano Hindus don't eat beef wakati wengine tunakula kila kitu, hii imekaaje?Nani yupo sawa?
- SADAKA - Mfumo wa sadaka wa dini za sasa umekwenda na wakati kutoka vitu na sadaka binafsi mpaka fedha na nyumba za ibada, kwa hii enzi yetu anayetoa sadaka nyingi nyiye mtakatifu bila kujali hiyo sadaka imetoka wapi-... hapa pana tatizo kubwa na pananifanya nijiulize maswali yasiyo na majibu.
- UADILIFU WA VIONGOZI WETU WA DINI/MASISTA - Uwepo wa waalamu wengi waliobobea wa huyo MUNGU wa dini ambao wenyewe ndio wala rushwa, wachoyo, wezi, wauwaji, waongo na wazinzi kunanipa pia maswali, je uwepo wa huyo MUNGU wanaye muubiri ni wa kweli au ulaghai?
- RELIGION INSTITUTIONALIZATION - Kitendo cha dini kuwa taasisi ambapo huna hiyari ya kukaa nje na ukikaa nje utaadhibiwa ni tatizo kubwa...uwepo wa dayosisi na majimbo, mfumo wa ibada na jumuia umekaa kikukusanya mapazo zaidi badala ya kushibisha watu imani, hapa napo sina majibu yake!
Si vibaya kwa wenye majibu sahihi mkaja kutuondolea wasiwasi wetu kwa upole kama ambavyo mafundisho yenu yanavyosema, muwe na kiasi ... msiwe wakali sana.
(Ni mtazamo binafsi)